Maji Safi Group
05/27/2026
Ulimwengu huadhimisha siku ya hedhi salama duniani kila ifikapo Mei 28 ya kila mwaka, sisi MSG si tukio la siku moja pekee tunafikia jamii mara kwa mara na kuwakumbusha kuhusu masuala ya hedhi salama, ni bahati iliyoje kwa wazazi, walimu na wanafunzi kujumuishwa kwa pamoja kupitia jitihada za taasisi yetu ili kujadili masuala haya kwa uwazi, hapa tunavunja ukimya, tunaondoa vikwazo vyote na kuleta tabasamu kwa wanawake na wasichana wote, hedhi salama ni jukumu la jamii nzima.
05/08/2026
Maji Safi Group imefika katika ofisi ya katibu tawala wa Mkoa wa Mara ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake Bi. Rachel Stephen (Aliyeketi kulia) kwa lengo la kutambulisha Mradi wa Afya ya Hedhi Shuleni kwa
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusava (Aliyeketi katikati) tarehe 07 Mei, 2026 ambaye alifungua kikao kazi cha kuutambulisha mradi wa Afya ya Hedhi shuleni (MHH) unaotekelezwa na Taasisi ya Maji Safi Group katika baadhi ya Halmashauri za Mkoa wa Mara
Katibu Tawala Kusava amewataka watumishi katika halmashauri ambazo MSG inafanya mradi huo kutoa ushirikiano ili kutimiza lengo zuri la taasisi hiyo.
Mbali na kikao kazi MSG ilitoa mafunzo kwa vitendo na kuonesha namna inavyofanya shughuli zake moja kwa moja katika klabu zake za makuzi, balehe na hedhi salama shuleni kwa waliyo udhuria kikao hicho, ikiwa ni pamoja na kuonesha vifaa vya kujistiri wakati wa hedhi na namna ya utengenzaji wa vifaa vya dharura.
Kikao hicho kimehudhuriwa na baadhi ya Maafisa kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, Maafisa Elimu, Maafisa Elimu Taaluma, Maafisa Afya kutoka Halmashauri za Wilaya za Tarime Serengeti na Musoma.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the organization
Telephone
Website
Address
455 Marine Street
Boulder, CO
80302