MAMBO MSETO
KAHAMA YAOMBWA KUTENGA ENEO LA KILIMO CHA VANILLA.
MKURUGENZI wa Kampuni ya Vanilla International, Saimon Mkondya, ameipongeza Serikali kuondoa Kodi kwa zao la Vanilla huku akiomba wilaya ya Kahama kutenga eneo la kilimo Cha zao hilo.
KAHAMA KULIMA ZAO LA VANILLA
Wakazi wa wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wameaswa kukuza uchumi wa kaya zao kwa kujikita kulima zao la biashara la Vanilla ambalo lina soko kubwa Duniani.
Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ihusikanayo na zao hilo nchini, Saimoni Mkondya, huku akiwasisitiza kwa ustawi wa vyakula walime mazao mengi ya chakula, huku wakihamasika kulima zao la Vanilla.
15/08/2022
YANGA NI WAFALME WA SIMBA TANZANIA
YANGA wako juu zaidi ya Simba wanapopambana hapa Tanzania bila kujali kuwa kuna wakati huko nyuma wao waliwahi kufungwa mengi na Simba. ANAANDIKA IBRAHIM MKAMBA.
Yanga kwenye mashindano ya ubingwa wa nchi hii wameishinda Simba mechi nyingi na wameifunga jumla ya magoli mengi na kufungwa machache kwenye mechi za wao kwa wao.
Ubingwa wa Tanzania kiuhakika ni wa Yanga. Ukiona Simba au timu nyingine inaubeba ubingwa huo ujue kuwa Yanga wana matatizo fulani. Hata wanapokuwa hivyo, wakikosa ubingwa hawashuki zaidi ya wa pili.
Mara nne za mfululizo ambazo Simba walibeba ubingwa, walifanya hivyo zaidi kwa sare nyingi walizozipata Yanga na si kwa wao Yanga kupata matokeo mabaya dhidi ya Simba.
Kwa ufupi Yanga wanapogombea ubingwa wa Tanzania na wanapopambana na Simba ari yao kimapambano huwa juu sana. Kwangu sikushangazwa na matokeo ya Ngao ya Jamii.
Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wakubwa. Inaweza kufanya makubwa Afrika k**a ari yao ya hapa wataihamishia Afrika. Wanapaswa waanze kujijenga hivyo msimu huu.
Simba wana ari kubwa wanaposhiriki mashindano ya Afrika lakini kwa hapa hufanikiwa kutegemea kudorora kwa Yanga tu. Hawana ari waliyonayo kwenye mashindano ya Afrika.
Simba wanachopaswa kufanya ni kuwa na ari ya ubingwa wa hapa k**a walivyo na ari ya mashindano ya Afrika. Wanapaswa wakumbuke ubingwa wa hapa ndiyo utawapa nafasi ya uwakilishi kimataifa. Si kila wakati tutaingiza timu zaidi ya mbili, moja kila mashindano, kwenye mashindano ya Afrika.Nimeshauri.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Majengo, Kahama
Shinyanga