Mwenebato

Mwenebato

Share

Photos from Mwenebato's post 02/08/2019
29/07/2019

Mwanza mwanza ni jpili tu

20/07/2019

SIBWESA, MCHANGANI,
Moja ya kijiji kinachopatikana k**ini mwa Kigoma, kijiji hichi kipo jirani na hifadhi ya taifa ya Mahale, kwa upande wa k**ini kimepakana na Kalya, na pia kipo katika mwambao wa ziwa Tanganyika., kijiji hichi kina rasi ya maajabu iliyozungukwa na majabari ya mawe, rasi hii imechongoka kuelekea mashariki mwa Congo ambapo mabaharia wengi wa ziwa Tanganyika hutumia rasi hii k**a alama moja wapo ya kupata muelekeo waendako, upepo wa k**i unapovuma (Rukuga) mabaharia huegesha vyombo vyao vya usafiri katika kijiji hichi ili kuukwepa upepo kwasababu rasi hiyo haipitiki wakati wa upepo mkali, kutokana na hilo serekali imeamua kujenga bandari ndogo kwenye fukwe ya kijiji hichi ambapo meli kutoka Congo, Zambia na Kigoma zitaweza kuegesha hapo,

Msimulizi anatueleza kwamba kijiji hichi kinaaminika kwa kuwepo na mazindiko ya nguvu za giza kwakuwa kuna moto usiozima nyakati za usiku kutoka upande wa rasi hiyo, ambapo ukijiaribu kuusogelea moto huo hautaukuta lakini ukiwa mbali unauwona. Vilevile msumilizi anaeleza maajabu ya jogoo anaewika katika rasi hiyo jambo ambalo muwiko huo wa jogoo hupelekea wavuvi kuvua samaki na dagaa kwa wingi, Kijiji hichi ndio kinasifika kwa kutoa samaki wa mapambo wenye gharama kubwa, katika miaka ya 1990 meli kongwe ya MV Liemba ilikuwa ikionekana ikifanya safari zake wakati wa usiku maeneo ya kijiji hichi wakati kiuhalisia meli hiyo inakuwa imeegesha bandari ya Kigoma. Wakazi wa kijiji hichi ni kabila la Wagoma-Wamanyema ambao wapo katikati ya kijiji (Mchangani), Waha wanapatikana mashariki (Makola) na Wafipa wanapatikana eneo la rasi hiyo (Rasini)..

Kutokana na uwepo wa Jogoo huyo wakazi wa Mchangani waliipa jina 'Jogoo FC' timu yao mpira, Upande wa Makola ambapo Waha hupatikana wao Timu yao ya Mpira waliipatia jina 'Makola Rangers FC' kwakuwa upande wao ndio unaopakana na msitu wa hifadhi ya taifa ya Mahale, na upande huu wa Rasini kutokana na moto wenye kutoa nuru isiozima waliamua kujiita 'Rasini Stars FC'' Maajabu huonekana uwanjani timu hizi za mpira zinapokuwa zikipambana kijijini hapo,

Want your hotel to be the top-listed Hotel in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


ILEMELA
Mwanza