HEALTH PLANET
22/08/2022
, NINI CHANZO.
Tatizo la kupata haja kubwa iliyochanganyika na damu linasumbua watu wengi kwenye jamii.
Health Planet tunakuandikia Sababu kubwa 4 zinazopelekea mtu kupata hali hiyo;
1. Ugonjwa wa maambukizi ya Amiba, minyoo ya tumbo na kichocho kwenye njia ya chakula,
2. Ugonjwa wa Bawasili, ambao hutokea endapo mishipa midogo ya damu kwenye njia ya haja kubwa hujaa damu na kuvimba (hali hii huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia, maumivu ukiwa umekaa, na kuhisi kitu k**a kidole kwenye njia ya haja kubwa)
3. Kuchanika kwenye njia ya haja kubwa, hutokea kwa sababu ya kujisaidia choo kigumu ambacho huchana na kusabisha damu kutoka ikiwa imechanganyika kwenye haja kubwa.
4. Saratani ya Utumbo mpana pia inahusika na kupata haja kubwa iliyochanganyika na damu
Je unapata tatizo hili, HEALTH PLANET tunakupa ushauri na elimu zaidi kuhusu tatizo ulilonalo.
Karibu tuandikie kwenye page yetu kwenye kitufe kilichoandikwa 'Message'
21/03/2022
NAMNA YA KUTUMIA KUPANGA UZAZI NA KUEPUKA KUPATA MIMBA ZISIZOTARAJIWA.
wa mpango ni muhimu kwa wale wanaotaka kufanikisha malengo yao kabla ya kuamua kupata ujauzito na kuzaa mtoto/watoto. Pia ni muhimu kwa wenza au yule anaetaka kuzaa watoto wenye afya njema kwa kuweka nafasi ya kutosha kati ya mtoto na mkubwa wake, humpa nafasi mwanamke kurejea katika hali ya kawaida kiafya baada ya uzazi na kupata mda wa kufanya majukumu mengine.
ya kupanga uzazi kwa kutumia Kalenda, ni njia ya asili bora na salama inayoweza kumkinga binti au mwanamke asipate ujauzito katika kipindi ambacho haitaji,
👉Haina athari kwenye mfumo wa homoni za mwanamke au njia ya uzazi k**a zilivyo njia zingine za homoni au kitanzi.
👉Wenza au mtumiaji huitaji kutambua na kukwepa siku zenye uwezekano mkubwa wa kupata ujauzito(Siku za hatari).
👉Ni njia inayohitaji ushirikiano kati ya wenza ili kukubaliana na kuepuka kufanya tendo wakati wa siku za hatari.
kutumia njia hii kwa usahihi ni muhimu mwanamke awe na
👉Mzunguko wa hedhi unaoeleweka, unaoweza kuhesabika mwanzo na mwisho wake.
👉Awe na mzunguko wa hedhi ulio kati ya siku 21, 28,hadi 35.
👉Awe na uelewa angalau wa kujua kusoma namba.
👉Awe na Kalenda ya ukutani au kwenye simu.
wanaochukua mda mrefu sana kuona siku zao, wasioingia au wanaoingia hedhi kwa kuruka mwezi/miezi au kuona matone kidogo sana ya damu kwa masaa machache ni vigumu kufanikiwa kutumia njia hii.
vya msingi kujua kabla ya kuanza kutumia kalenda
👉Mzunguko wa hedhi ni kipindi ambacho mbegu ya k**e hutengenezwa kwenye ovari na hupevuka pia maandalizi ya kupokea ujauzito hufanyika ndani ya mfuko wa uzazi na kuharibiwa k**a ujauzito haukutungwa.
👉Kipindi cha kwanza cha mzunguko ni wakati ambao mbegu ya k**e hutengenezwa kwenye ovari na kukomaa-huchukua takribani muda wa wiki 2(siku 14)
👉Kipindi cha pili cha mzunguko ni wakati ambao mbegu iliyokomaa hurutubishwa na mbegu ya kiume na muunganiko wake kusafiri hadi kwenye mji wa mimba ili kutunga ujauzito, 💥Pia ni kipindi ambacho k**a mbegu haikurutubishwa huandaliwa pamoja na ukuta wa ziada kwenye mji wa mimba( ulioandaliwa kupokea ujauzito) hutolewa nje ya mwili k**a damu kipindi cha hedhi. Kipindi hiki huchukua siku 14(kwa wenye mzunguko wa siku 28), siku 7(kwa wenye mzunguko wa siku 21(siku 21 kwa wenye mzunguko wa siku 35)
👉Siku za hedhi-ni siku ambazo mwanamke hutoka damu, kwa kawaida huchukua kati ya siku 3 hadi 7, Idadi ya siku za hedhi haina athari kwenye kuhesabu kufikia siku za hatari.
👉Siku ya mbegu ya k**e kupevuka na - ni siku ambayo mbegu ya k**e iliyokomaa hutoka kwenye ovari, ndio mda ambao k**a mbegu ya k**e itakutana na ya kiume hurutubishwa na kutunga ujauzito, ni kipindi muhimu ambacho wasiopenda kupata ujauzito huitaji kujua ili wakwepe kufanya tendo kwenye siku chache kabla, ndani ya siku yenyewe na siku chache baada. Kipindi hiki huitwa siku za hatari kwa wasiopenda kupata ujauzito.
đź’ĄSiku ya 14 ndio ambayo mbegu ya k**e hupevuka, kwa sababu ya uwezekano wa kuwahi kupevuka siku chache kabla au kuchelewa siku chache baada ya siku ya 14 kipindi cha siku za hatari huongezwa kutoka siku chache kabla ya siku ya 14 hadi siku chache baada ya siku ya 14. Kwa sababu hiyo siku za hatari huanzia siku ya 12 hadi ya 16 ya mzunguko, kwa sababu za kuongeza uwezekano zaidi wa kukwepa ujauzito siku za hatari zinaweza kuongezwa zaidi kuanzia siku ya 10 au 11 hadi ya 18 au 19.
đź’ĄKipindi hiki pia huambatana na viashiria vingine k**a joto la mwili kuongezeka kidogo, kuwa na uteute mzito kwenye uke, kuongezeka kwa hamu ya kufanya tendo la ndoa.
$Ili kutumia kalenda kupanga uzazi, Mwanamke anapoona damu za hedhi siku ya kwanza
👉Weka alama kwenye kalenda ya mwezi, mfano kwenye mchoro wetu siku za hedhi, period au bleed ni tar 23 hadi 26, hapa tarehe 23 ni siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi.
👉Hesabu kwa kufuata kalenda kuanzia siku ya kwanza ambayo ni tar 23, k**a mwezi utaisha endelea tu kwenye mwezi mwingine.
👉Weka alama X kuanzia siku ya 12 hadi ya 16 ya mzunguko, Hizi ndo siku ambazo wenza watatakiwa kujua ili waepuke kufanya tendo la ndoa au kutumia vizuizi k**a kondom na kukwepa kupata ujauzito.
tunatoa huduma ya kupitia mzunguko wa hedhi na kufundisha namna ya kujua siku za hatari kwa mtu mmoja mmoja kwa kuzingatia siku alizoingia kipindi cha hedhi na kalenda ya mwezi husika.
Ili kupata huduma hii karibu inbox whattsap no yetu 0752354147.
29/01/2022
đź’ĄLEO TUANGAZE KUHUSUđź’Ą
UMRI SAHIHI KWA MWANAMKE KUPATA UJAUZITO, MADHARA YA MIMBA ZA UTOTONI NA MIMBA BAADA YA UMRI SAHIHI!!!
Karibu!!
👉Tamaa ya kutaka kufanikiwa maishani imeenea duniani kote. Hali imebadilika sana, jinsia ya k**e inataka kujitosheleza kwa kila kitu. Lakini mabadiliko ya kibaiolojia yanabaki vile vile mfano kuzeeka nk.
👉Mafanikio wanayowaza wengi ni utajiri wa pesa na elimu kubwa. Hii imesababisha wanawake wengi kusoma sana na kufanya kazi kupita kiasi, hata kupuuzia suala la kuzaa mapema.
👉Wengi wanashtuka ikiwa umri wao ni zaidi ya miaka 30, ndio wanakuwa na tamaa ya kuzaa. Kuchelewa kwao kuzaa kunaweza kuwa kwa taabu ama kuzaa watoto wenye matatizo mengi ya kiafya.
👉Kwa miaka mingi, wataalamu wengi wa afya ya uzazi bado wanaamini miaka 20-35 ndio umri sahihi kushika mimba na kuzaa.
👉Pia, wengi wakifikiri matatizo mengi ya uzazi huongezeka baada ya miaka 35 na huwa zaidi baada ya miaka 40.
👉Kwa wenzi wawili wanaoishi pamoja, kuchelewa kuzaa huathiri pia wenza wa kiume, ambapo mbegu za uzazi za mwanaume hudhorota kila mwaka upitao na watoto wamaotokana na wanaume wazee huwa na hatari zaidi ya kupata matatizo ya akili na matatizo ya chembe za urithi.
KUBALEHE
👉Kubalehe ni hatua muhimu sana lupotia ili kuweza kuzaa. Wastani wa kubalehe na kuvunja ungo kwa wasichana ni miaka 9-12 kwa sasa, ingawa miaka ya zamani ilikuwa kuanzia miaka 12-14.
👉Baada ya kubalehe binti anakuwa na uwezo wa kushika mimba, japokuwa uwezekano huongezeka zaidi kati ya miaka 20-30, baada ya hapa uwezekano huanza kupungua.
👉Kulingana na The American College of Obstricians & Gynecologists uwezo wa wanawake kuzaa hupungua katika umri wa miaka 32 na hupungua kwa kasi zaidi katika umri wa miaka 37.
👉Uwezo wa wanawake kuzaa hupungua vile umri unaongezeka kwa kuwa wanawake wanapobalehe wanakuwa na idadi kamili ya mayai katika ovari zao. Namba hii hupungua vile mwanamke anavyozeeka. Pia mayai hayazalishwi kiurahisi kwa wanawake wenye umri mkubwa ukilinganisha na mabinti wadogo.
👉Kulingana na National Institute for Health & Clinical Excellence (NICE) ya Umoja wa madola (UK), kwa wanawake wenye miaka 35, ni wanawake 94 kati ya 100 wanaweza kupata ujauzito wakifanya ngono kwa ukawaida ndani ya miaka 38, ni wanawake 77 kati ya 100 wanaweza kushika ujauzito.
👉Magonjwa ya njia za uzazi k**a Endometriosis na Uterine fibroids yanawatokea zaidi wanawake wenye umri mkubwa ambayo husababisha mwanamke kutoshika mimba.
👉Wanawake wenye umri zaidi ya miaka 35 wanaoamua kushika ujauzito wanakabili hatari ya kupanda kwa shinikizo la damu. Kupanda kwa shinikizo la damu wakati wa ujauzito huathiri kondo la nyuma (Placenta) ambalo hutoa lishe kwa kijusi (kitoto kilicho tumboni) hali ambayo huathiri moja kwa moja ukuaji wake.
👉Pia, hatari ya kupata kisukari kwa wanawake wanaoshika ujauzito wakiwa na miaka 35 na zaidi, huongezeka sana. Kisukari kipindi cha ujauzito huongeza hatari ya kutoka mimba (Miscarriage), kuzaa mtoto mwenye kasoro au kuzaa mtoto mkubwa kupita kiasi.
TAFITI YA HIVI KARIBUNI
👉Jambo la kushtusha, ni matokeo ya utafiti uliofanyika Sweden, watafiti wanadai hatari ya matatizo ya uzazi huanza mapema tu pale mwanamke anapofikisha miaka 30.
👉Utafiti uliochapishwa kwenye jarida la magonjwa ya uzazi (Journal of Obstetrics & Gynacology) uliofanywa na watafiti kutoka Taasisi ya Karolinska ya nchini Sweden umegundua katika nchi tajiri duniani wanawake huzaa wakiwa na umri mkubwa kitu kinachopelekea kuongezeka kwa hatari ya kuzaa watoto njiti (Preterm birth), ukuaji hafifu wa vichanga na kuzaa watoto wafu (Stillbirth).
👉Ili kubainisha hatari kati ya makundi tofauti ya umri ya wanawake wanaozaa kwa mara ya kwanza, watafiti walitumia takwimu za vizazi toka hospitali za Sweden na Norway, zilizokusanya taarifa za karibu wanawake milioni moja, kati ya mwaka 1990 na 2010.
👉Hatari ya kuzaa watoto njiti (Premature birth) na kuzaa watoto wafu huongezeka kuanzia miaka ya 30 ingawa toka zamani, miaka 35 ndio ilitambulika kuwa mwanzo wa hatari kwa wanawake kupata watoto, lakini utafiti huu mpya unataja mwanzo tu wa miaka 30 hatari ya kupata matatizo katika uzazi huanza.
👉Kwa kulinganisha kati ya kundi la umri wa miaka 25-29 na 30-34, wanawake wa miaka 30-34 wenye mimba za kwanza walikuwa na hatari ya kuzaa watoto njiti kwenye wiki 22-31 za ujauzito au kuzaa watoto wafu.
👉Kikosi cha watafiti kiligundua pia sababu zingine zinazoweza kuleta matatizo ya uzazi mfano wa sababu hizo ni k**a kuvuta sigara au kuwa mnene kuliko kawaida.
👉Ulla Waldenstrom, profesa wa kitengo cha afya ya wanawake na watoto katika taasisi ya Karolinska alisema : 'Tumeshangazwa na kuongezeka kwa hatari za uzazi katika umri mdogo sana.'
👉Prof. Waldenstrom aliendelea ; 'Wanawake wanaweza ona hatari ni ndogo ila kwa jamii kiujumla kuna idadi kubwa ya matatizo yasiyo ya lazima kwao wanawake wanaozaa baada tu ya miaka 30. Hivyo nashauri wanawake na wanaume wapewe taarifa mashuleni juu ya umuhimu wa umri katika uzazi.'
👉Alipoombwa ushauri kwa wanawake wenye umri zaidi ya miaka 30 wanaotaraji kuzaa, Prof. Waldenstrom alisema ; 'Ushauri bora ni kuepuka uvutaji wa tumbaku/sigara na kuepuka unene, k**a inawezekana.''
KIPINDI CHA KUKOMA HEDHI (MENOPAUSE)
👉Wataalamu wa afya wanasema kwamba mwanamke amekoma hedhi anapokosa kupata hedhi kwa miezi 12 mfululizo. Ni wanawake wachache hukoma kupata hedhi ghafula, yaani, wanakosa hedhi mwezi mmoja unakuwa mwisho wa kuipata.
👉Wanawake wengi huanza kipindi hiki wakiwa na umri wa miaka 40 na kitu, lakini kwa wengine huanza wakiwa wamechelewa wakiwa na miaka 60 na kitu.
👉Kutokana na mabadiliko ya kiwango cha homoni kinachotokezwa, huenda mwanamke akakosa kupata hedhi pindi kwa pindi, akapata hedhi wakati ambao hakutarajia au akavuja damu nyingi isivyo kawaida wakati wa hedhi. Pia huenda mwanamke akashuka moyo, hisia zake zikabadilikabadilika na hilo linaweza kumfanya alielie bila sababu, na pia asiwe makini sana na asahau mambo.
👉Kipindi cha kukoma hedhi huwa tofauti kwa kila mwanamke. Dalili zinaweza kuonekana kipindi hicho ni pamoja na joto la ghafula mwilini, ambalo huenda likafuatiwa na kuhisi baridi. Dalili hizo zinaweza kumfanya mtu akose usingizi na kuishiwa na nguvu.
👉Baadhi ya wanawake hupatwa na joto la ghafla mwilini kwa mwaka mmoja au miaka miwili wakati wa kipindi hicho cha kukoma hedhi.
👉Wengine hupatwa na hali hiyo kwa miaka mingi na wachache sana husema kwamba wao hupatwa na joto la ghafula mara kwa mara maisha yao yote.
👉Ni busara mtu afanyiwe uchunguzi wa kiafya kabla ya kuamua kwamba joto la ghafula linasababishwa na kukoma kwa hedhi. Kwa kuwa kuna matatizo mengine ya kiafya yanaweza kuleta joto la ghafula mfano ugonjwa wa dudumio, malaria, homa ya matumbo n.k
JINSI YA KUISHI VIZURI KIPINDI HICHO
👉Mabadiliko ya mtindo wa maisha yanaweza kupunguza baadhi ya matatizo hayo mfano kuacha kuvuta sigara, kupunguza au hata kuacha kunywa vileo, vinywaji vyenye kafeini na vyakula vyenye sukari au vikolezo ambavyo vinaweza kusababisha joto la ghafula mwilini.
👉Kufanya mazoezi husaidia sana kupunguza matatizo yanayohusianishwa na kukoma kwa hedhi. Kwa mfano, mazoezi yanaweza kupunguza kukosa usongizi na kusaidia kuboresha hali ya kihisia na pia huimarisha mifipa na afya ya mtu kwa ujumla.
👉Ili kumsaidia mwanamke kukabiliana vizuri na kipindi hicho cha kukoma kwa hedhi, huenda madaktari wakampa homoni, vitamini na madini, na dawa za kutibu kushuka moyo.
👉Pia ni jambo la busara kuwaambia uwapendao hali unayokabili ili wakuonyeshe upendo na wakupe msaada unaouhitaji wakati wa hali yako.
👉Kipindi hicho kinapokwisha, wanawake ambao hutunza afya yao, wanapata tena nguvu na kuendelea kufurahia maisha.
Asanteni sana kwa kufuatana nami, Karibu HEALTH PLANET
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mwanza