ELCT - ELVD
03/06/2026
Leo Juni 03, 2026 watumishi wa kituo cha ushauri wa kisaikolojia-Nyakato wamewajengea uwezo wanafunzi wa Mwanza Lutheran Secondary School kuhusu afya ya akili.
28/05/2026
ZIARA YA KAZI YA KATIBU MKUU KKKT-DMZV
Katibu Mkuu wa KKKT-Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria akishirikiana na Mkuu wa Idara ya Mipango na Uwekezaji na Huduma za Jamii leo tarehe 28, Mei wamefanya ziara katika Usharika wa Emanueli-Sengerema ya kukutana na watumishi wa jimbo, usharika na mradi wa ACHIEVE Pamoja na kukagua shughuli za uhitimishaji wa mradi.
Pia ziara hii imefika katika Usharika wa Tumaini-Kasamwa kuona shughuli mbalimbali zinazoendelea pamoja na utekelezaji wa mpango mkakati. Vilevile ziara iliendelea mpaka mtaa wa Penueli-Nampalahala kuona na kukagua kazi mbalimbali ikiwemo mpango kazi wa mtaa, uendelevu wa shughuli za mradi wa utunzaji mazingira (CCAP), mradi wa uchimbaji wa visima, mradi wa uwekaji vioo na vigae katika usharikani na mradi wa ufugaji nyuki unaoendelea.
Ziara hii imekua na matokeo makubwa sana baada ya vikao vya mrejesho na majadiliano ya namna ya kuboresha kazi hizi za taasisi.
25/05/2026
Idara ya Huduma za Jamii kupitia Kituo cha afya Nyakato Leo Mei 25, 2026 imepokea ugeni toka Makao Makuu ya Kanisa(KKKT), Kurugenzi ya Afya na Diakonia. Ziara hii imeangazia namna bora ya Kanisa kuihudumia jamii kupitia Huduma shufaa (Palliative Care),utekelezaji na ubora wa huduma mbalimbali zinazotolewa katika
kituo hicho, kuimarisha mifumo ya rufaa, ukusanyaji wa taarifa, ufuatiliaji wa huduma na ushirikiano kati ya hospitali na jamii. Kwa kutambua umuhimu wa ubora wa huduma katika mchakato wa utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote, ziara hii pia imelenga kufanya tathmini ya kina ya utayari wa vituo vya huduma za afya, pamoja na kuandaa mikakati shirikishi ya uboreshaji itakayowezesha kufikia malengo ya utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote kwa ufanisi na uendelevu.
24/05/2026
MAANDALIZI YA KUZALIWA DAYOSISI MPYA YAANZA MKOANI GEITA.
Katibu Mkuu wa Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria Bwana Joshua Kyelekule Amemtambulisha Mkuu wa Jimbo la Magharibi kati Mchungaji
Daniel Kaijunga kuwa mratibu wa shughuli zote za uanzishwaji wa Dayosisi mpya mkoani Geita.
Ibada ya utambulisho huo imefanyika jumapili hii ya tarehe 24/05/2026 katika usharika wa Upendo-Geita uliopo Jimbo la Magharibi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali .
Akifanya utambulisho huo Katibu Mkuu Bwana Kyelekule amewaomba wajumbe wa k**ati ya kuratibu uanzishwaji wa Dayosisi mpya,Wachungaji pamoja na washarika wote kumuunga mkono Mchungaji Kaijunga ili kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa viwango vya juu zaidi.
Ikumbukwe kuwa kikao cha Halmashauri Kuu ya Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria (DMZV) kilichokaa Aprili 29 na 30 mwaka 2026 kilipitisha jina la Mchg.Daniel Kaijunga kuwa Mratiibu wa shughuli zote za kuanzishwa kwa dayosisi mpya ambayo inatarajiwa kuanza Mwaka 2029.
Aidha zoezi la utambulisho huo limeambatana na kukagua ujenzi wa Kanisa Kuu la Dayosisi hiyo mpya linalojengwa katika usharika wa Upendo pamoja na maeneo mengine ya kujengwa Ofisi za Dayosisi na nyumba ya Askofu.
Kwa sasa Dayosisi .ashariki ya Ziwa Victoria DMZV ina jumla ya mikoa miwili ambayo ni Mwanza na Geita na kukamilika kwa Dayosisi mpya kutaufanya mkoa wa Mwanza ujitegemee na Geita itajitegemea.
12/05/2026
Halmashauri ya Wachungaji imefanya kikao chake cha kikatiba kuanzia tarehe 11 na 12 Mei 2026, katika Chuo cha Kilutheri Nyakato.
Leo katika kikao hicho kimehudhuriwa na watumishi kutoka KKKT-Makao Makuu Bi Patricia Mwaikenda kwaajili ya kukusanya maoni ya mradi mpya utakao jikita na vijana watakao tekeleza mradi huu katika Dayosisi Mashariki ya Ziwa Victoria.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the place of worship
Website
Address
P. O. Box 423
Mwanza