Christ Freedom Church - CFC

Christ Freedom Church - CFC

Share

08/05/2026

*Karibu sana Christ Freedom Church*
Nsumba Kiseke, Mwanza Tanzania

*Karibu kwenye ibada ya jumapili*
Tujifunze zaidi kwenye nguvu ya maneno ya Mungu ndani ya mtu binafsi

*Maneno yake kukaa ndani yetu*

*Yohana 15:7 (SUV)*
“Mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.”

~ Maswali mengine ya kujiuliza, je, maneno yake yanakaa ndani yetu kweli?
~ Mtu aliye mtoto kwa Mungu/kanisa hujitahidi maneno ya Mungu/kanisa kukaa ndani yake.
~ Hata hivyo kuna wanaoendeleza uvivu na uzembe ambao baada ya muda vyaweza hata kuwatoa ndani ya Mungu/kanisa.
~ Kuna watu wamo ibadani lakini hawamo ndani ya Mungu/kanisa na maneno ya Mungu hayamo ndani yao kabisa.
~ Lakini kuna watu hawamo ndani ya Mungu/kanisa lakini maneno ya Mungu yanakaa ndani yao. Unakubaliana nami kwenye hilo? Shetani anaangukia kwenye category hiyo. Satan ana uwezo wa kuvuruga mtu kiasi kwamba huyo mtu hakai ndani ya Mungu/kanisa lakini maneno ya Mungu yanakaa ndani yake k**a satan mwenyewe.

19/07/2025

Nguvu ya Shuhuda (The Power of Testimony) ni somo lenye msingi mkubwa katika maisha ya Kikristo. Shuhuda ina nguvu ya:

Kuthibitisha uaminifu wa Mungu

Kuwatia moyo wengine

Kuweka ushindi dhidi ya shetani

Andiko la msingi:
Ufunuo 12:11
“Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-Kondoo, na kwa neno la ushuhuda wao; ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.”

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Nsumba, Kiseke
Mwanza