Kitambo Inspiration

Kitambo Inspiration

Share

10/06/2026

UMEDANGANYWA NA WA SDA NAOMBA NIKUSAIDIE RAFIKI YANGU

Shalom wapendwa

Kwa Leo naomba nimsaidie rafiki yangu huyu na yeyote mwenye fikra k**a hizi..

Katika ujumbe wake alioutoa ameeleza kwamba Bwana wa sabato anakuja na ili tuwe salama tunapaswa kushika sabato ndo mhuri wake..

Akatoa maandiko ..Ezekieli 20:20, kum31:15-18, isaya58:13-14 nk

SASA TWENDE SAWA

1.kosa kubwa ambalo linawatesa wasabato na litaendelea kuwatesa ni kushindwa kutafsiri mkutadha ..yaani ujumbe mkuu , lini? Kwetu tufanye nini nk

Kwahiyo wao wanachukua kamstari kamoja tu na kutembea nako ...Imesalia raha ya sabato... Au sabato imefanyika kwa wanadamu...

2.katika maandiko hayo aliyotaja hakuna hata moja la agano la jipya..ndio maana nilisema hawa wasabato wanajifanya kumtukuza Kristo lakini ihalisia wamefungamana na mafundisho ya misa

3.Agano jipya limeweka wazi kwamba mhuri wetu ni Roho mtakatifu...

Sasa hawa jamaa unaweza kujiuliza kwanini hawataki kumnadi Roho mtakatifu?? Ilihali Yesu anaondoka atakuja msaidizi ROho mtakatifu ...yohana14:26

Na pia paulo natuweka bayana kwamba mhuri wetu tunaupata kwa Roho mtakatifu..si kwa kusali siku ya jumamosi..AMKENI

Waefeso 4:30
[30]Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi.

4.Jambo la kujiuliza dogo sana ..kwamba k**a sabato ingekuwa lazima au mhimu kiasi hicho k**a wanavyotuelezea ndugu zetu wasabayo ...

Kwanini Yesu hakuna mahali aliagiza au kusiaktiza wafuasi wake kuishika sabato??

Baada ya ukristo kuanza nyaraka nyingi zilizoandikwa na mitume ...za Paulo, yo ha na, petro ,yuda nk kwanini hakuna hata mmoja aliyewakumbusha au kuwasisitiza kuishika ??

K**a ingekuwa mhimu au lazima kwa wakristo naamini wangesisitiza ...

Mbona sheria zingine au amri zingine k**a :usiibe , usiabudu sanamu, usizini nk zimeagizwa kwa wakristo na Yesu au nyaraka za mitume lakini hakuna agizo la kuendelea kushika sabato?? Je Walijisahau ? Walipuuza??

AMKENI AMKENI AMKENI

Mungu awabariki

04/06/2026

KIGOMA MWAKEYE TUMEWAFIKIA

04/06/2026

Usihukumu watu kwa makosa yao ya jana ,watu hubadilika ,watu huinuka tena upya na kufanya vizuri

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address


Isamilo
Mwanza