Maswa Digital Network
21/03/2021
UONGOZI wa klabu ya Yanga pamoja na kikosi chao leo Jumapili asubuhi watakuwa miongonj mwa wananchi watakaokuwa katika msafara wa kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli katika uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Yanga jana Jumamosi jioni ilisimamisha kambi yao na kutoa fursa kwa wachezaji wao leo Jumapili kwenda kutoa heshima zao za mwisho kwa Rais huyo aliyeaga Dunia Machi 17 jioni baada ya kuugua ugonjwa wa moyo.
Wachezaji na viongozi wa klabu hiyo watakutana makao makuu ya klabu saa 3:00 asubuhi kisha ndio msafara wao utaanza kwenda katika uwanja wa Uhuru.
Kupitia katika ukurasa wao rasmi wa Instagram ulielezea kuwepo kwa tukio hilo kwa wachezaji na viongozi wao siku ya leo.
Shughuli za kuaga mwili wa marehemu Magufuli zilianza jana kwa kuongozwa na Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mawaziri, viongozi na kufuatiwa na wananchi wa kawaida.
Rais huyo amefariki huku akikumbukwa kwa uwezo wake wa kusimamia kile ambacho ana kiamini mpaka kitimie k**a alivyokuwa anataka.
21/03/2021
Makamu wa Rais wa Marekani, K**ala Harris ametuma ujumbe wa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kuwa kiongozi mkuu wa nchi.
Kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter, K**ala ameahidi kushirikiana na Samia kudumisha ushirikiano wa nchi hizo mbili.
“Ninatuma salamu za pongezi na kumtakia kila la kheri Samia Suluhu baada ya kuapishwa k**a Rais mpya wa Tanzania, mwanamke wa kwanza kushika nafasi hiyo, Marekani inajiandaa kufanya kazi kwa pamoja naye katika kudumisha ushirikiano wa nchi zetu,” amesema K**ala.
K**ala ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo katika historia ya Marekani na aliapishwa Januari 20, 2021 sambamba na Rais Joe Biden.
Samia aliapishwa kuwa Rais wa Tanzania Machi 19, 2021 baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Mwanza