Adrix Media
25/04/2026
BODI YA KAHAWA TANZANIA ( TCB) IMETANGAZA TAREHE YA UFUNGUZI WA MSINGI WA KAHAWA KATIKA MIKOA YOTE TANZANIA INAYOLIMA ZAO LA KAHAWA.
Katika taarifa yao iliyochapishwa kwenye tovuti yao rasmi wameweka wazi kuwa kwa mkoa wa Kagera msimu utafunguliwa kuanzia tarehe 1/05/2026
15/04/2026
BRRH YAENDELEA KUIMARISHA MAPAMBANO DHIDI YA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI
Idara ya Uzazi na Kizazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba (BRRH) leo Aprili 14, 2026 imefanya kikao muhimu cha MPDSR (Maternal and Perinatal Death Surveillance and Response) chenye lengo la kujadili kwa kina vifo vitokanavyo na uzazi, kubadilishana uzoefu, kuelekezana kitaalamu na kuweka mikakati madhubuti ya kuokoa maisha ya mama na mtoto.
Akiongoza kikao hicho, Mkuu wa Idara ya Uzazi na Kizazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba, Dkt. Timon Theophil, amesisitiza umuhimu wa uwajibikaji, ufuataji wa miongozo ya afya pamoja na ushirikiano wa karibu miongoni mwa wataalamu wa afya katika utoaji wa huduma bora kwa mama na mtoto, ili kukomesha vifo vitokanavyo na uzazi vinavyoweza kuzuilika. Kikao hicho kimewakutanisha wataalamu kutoka Idara ya Uzazi na Kizazi, ICU, Idara ya Dawa za Usingizi, Magonjwa ya Ndani, Idara ya Upasuaji pamoja na wataalamu wengine kwa mujibu wa muongozo wa kitaifa, hatua inayolenga kuimarisha mshik**ano wa kitaalamu katika kushughulikia changamoto za uzazi kwa ufanisi zaidi.
Kupitia kikao hiki, BRRH inaendelea kuonesha dhamira yake ya kuchambua changamoto za kitabibu, kuimarisha ushirikiano wa kitaalamu, kuboresha ubora wa huduma za uzazi na kupunguza, hatimaye kutokomeza vifo vitokanavyo na uzazi ambavyo vinaweza kuzuilika, k**a sehemu ya juhudi za kuimarisha afya ya mama na mtoto katika Mkoa wa Kagera.
โ๏ธAfisa habari Brrh Kagera
02/04/2026
Baraza la Biashara la Wilaya ya Kyerwa limefanyika Aprili 2, 2026 katika Ukumbi wa Halmashauri ambalo limewakutanisha wadau mbalimbali wa biashara kutoka katika taasisi za umma na binafsi zilizopo wilayani Kyerwa.
โ
โWafanyabiashara Wilaya ya Kyerwa, kupitia kwa Mwenyekiti wa wafanyabiashara wilaya Kyerwa Bw. Yesau Mstapha, wameomba Serikali kushughulikia changamoto zinazowakabili wafanyabiashara ikiwemo miundombinu ya barabara, umeme na mawasiliano ili kuwawezesha kutoa huduma bora kwa Wanakyerwa.
โ
โ
โAkiongea na wadau hao, Mhe. Msofe ametoa onyo kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na uuzaji wa bidhaa bandia, akieleza kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria na kinaathiri afya za watumiaji huku akitoa rai kwa wataalamu wa Halmashauri kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kudhibiti vitendo hivyo.
Aliyoyasema Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa kwenye mkutano wa vyama vya Ushirika vya kahawa kwa Wilaya ya Kyerwa na Karagwe
Imebakia takribani miezi 2 na nusu msimu wa kahwa kufunguliwa, hivyo vyama tayari vimewmza kujipanga kufanya ukusanyaji na ununuzi wa kihistoria Part 9
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Nyamagana
Mwanza