Hadithi

Hadithi

Share

13/01/2026

MAMA ANAMSALITI BABA

Habari za usiku huu kaka? Nakuja mbele ya group lako kuomba ushauri.

Nimegundua mama yangu si mtu mwema kwa baba yangu. Nilikuwa nampenda sana mama yangu, nilimuamini na kumheshimu sana, lakini kinyume na matarajio yangu mama si mtu mwaminifu kabisa ameniangusha na kuiumiza nafsi yangu.

Mama aliaga amesafiri kikazi kwenda Morogoro kwa wiki moja. Alituacha na baba. Siku iliyofuata niligundua kuwa mama anamsaliti baba yangu tena na mfanyakazi wake.

Niligundua hili baada ya kuwa nimetoka na rafiki zangu kwenda kwenye mghahawa mmoja maarufu wa chakula mbali kidogo na tunapoishi ndipo nilipowakuta, mama akiwa na kajana mmoja niliyemtambua k**a mfanyakazi wake pale ofisini, wakila na kunywa kwa mahaba.

Ile Hali ilinikasirisha sana, binafsi nilijua mama kasafiri inakuwaje yuko ndani ya mji huu tena akivinjari na kivulana vidogo? Kifupi nilighadhabika mno.

Niliondoka eneo lile haraka na kuwaacha. Nilifika nyumbani nikiwa na maumivu makali, hata baba aliporudi jioni kutoka kwenye majukumu yake nilijizuia nisimwambie maana nilijua maumivu yake iwapo atapata habari hizi.

Siku tano zenye uchungu na hasira ya kutunza Siri iliyoniumiza hatimaye mama anarejea akijifanya katoka safari na mibegi yake akijichekesha k**a mwenda_wazimu Kwa unafiki anamkumbatia baba na kumwambia kamumiss sana. Nilitamani kutapika.

Binafsi nashindwa kukaa na hili swala moyoni ila najua nikimwambia baba hizi habari yatatokea haya, moja ndoa itakuwa imekwisha maana baba yangu namjua vyema. Pili Sina hakika na usalama wa hawa wawili mama na huyo ki Ben 10 wake. Sasa nishaurini lipi bora nikae na huu mzigo rohoni au nimfikishe baba yangu? Nasoma ushauri wapendwa.

10/01/2026

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Taus Sued Juma, Ma Abdul, Jacob Salasu, Raphael Michael Nusuhela, Mapinduzi Lunyungu, Julius Mlay, Joyce Mbunza, Evod Rabo, Jamila Fadhil Jamila, Patrisia Creopatra, Mwanaidi M***a, Leticia Gervas, Ishah Salum, Happy Daud, Sabitina Khamis, Pauleth Saileni, Mjelwa Jackson, Rose Adam, Sancho Amour, Annastasia Maingi, Mbaraq Eriq, Veelaw Paul, Mary Hassan, Bint Juma, Raphael Redempitius, Rachel Rashid, Shaban Wagara, Sheila Nyamalila, Noel Mhami, James Mhagama, Renalda Kirway, Rose William Makungu, Yusuph Faustino, Leah A Kizanye, James Alex, Nyash Erick Mlachake, Salome Emanuel, Devotha Thomas, Chripha Kusimba, Asid Myombe, Willium Samo, Rama Botswe, Jumaa Issa, Joseph Thoyaa, Christine Walubengo, Mamu Kassim, Emmanuel Fungamalie, Cureen Cureen, Hamsallah Sallah, Onesmas Mitau

02/01/2026

HATAKI MWANAMKE MWENYE MTOTO

Habri za mwaka mpya! Kaka nimekuja ukurasani kwako kuomba ushauri.

Ninamahusiano na jamaa mmoja. Tunapendana sana. Anajitoa, anajali na nimkarimu kwangu.

Changamoto inayonileta kwako kuomba ushauri ni kwamba, hapendi kabisa mwanamke aliyezaa. Amekuwa akilirudia hili mara Kwa mara kuwa hawezi kuwa kwenye mahusiano na mwanake mwenye mtoto.

Haogopi kuweka chuki zake wazi juu ya wanawake wenye watoto ambao hawajaolewa. Anawasema vibaya na unaona dhahiri kuwa hawezi kuishi na mwanamke mwenye mtoto.

Tangu tumefahamiana nimejitahidi sana kuficha kuwa Nina mtoto mkubwa tu niliyempata mapema zaidi tena kipindi Cha balehe.

Nina muhitaji sana huyu jamaa awe mume wangu. Ila siwezi kuendelea kuficha Siri juu ya Binti yangu maana huenda ikanigharimu baadae.

Nisaidieni ushauri nifanyeje ili nisimpoteze mchumba wangu na Binti yangu atambulike bila kificho.

Want your establishment to be the top-listed Arts & Entertainment in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


IGOMA, MWANZA
Mwanza