CBE GRAM

CBE GRAM

Share

16/03/2024

Misa Takatifu ya kumuombea Rais wa awamu ya Tano Hayati Dkt. John Magufuli itafanyika kesho Machi 17, 2024 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yohana Maria Muzeyi wilayani Chato mkoa wa Geita.

Kaimu mkuu wa mkoa wa Geita, Said Nkumba amewaambia waandishi wa habari kuwa Misa hiyo itahudhuriwa na watu mbalimbali akiwemo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko, mke wa Hayati Dkt. Magufuli Mama Janeth Magufuli, viongozi, Wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki.

Misa hiyo Takatifu ya kumuombea Rais wa awamu ya Tano Dkt. John Magufuli inafanyika Machi 17, 2024, ikiwa imetimia miaka mitatu tangu alipofariki dunia Machi 17, 2021.

Baada ya Misa hiyo Takatifu wageni mbalimbali watakaribishwa katika viwanja vya hoteli ya JS kwa ajili ya kupata chakula ambapo pia baadhi ya viongozi watapata fursa ya kuzungumza.

29/07/2022

Rais mstaafu wa serikali ya wanafunzi CBESO MWANZA CAMPUS Mh.Salum mtaturu anawatakia jummah mubarak⭐🌙

Jummah (Arabic: جمعة‎) (also known as Friday prayer) is a congregational prayer (salaat) that Muslims hold every Friday around noontime. It is mentioned in the Qur’an as:
“O you who believe! when the call is made for prayer on Friday, then hasten to the remembrance of Allah and leave off trading; that is better for you if you know. And when the prayer is ended, then disperse in the land and seek of Allah’s bounty, and remember Allah much, that ye may be successful.” (Qur’an 62: 9-10)



#جمعة مباركة #

03/05/2022

مجتمع عيد مبارك CBE

Heart is heavy as I bid farewell to a precious month that no one is guaranteed to experience next year. But full of joy that perhaps, out of the 30 days we were asked to give up things; one of those days is one that our sins were wiped cleaned and we were all forgiven by the most compassionate ❤️

May Allah reward us all for our ibaadat. 😘💫

عيد مبارك

Photos from CBE GRAM's post 01/04/2022

Je 'Siku ya Wajinga' duniani ilianzaje?

Siku ya wajinga duniani -inayoadhimishwa Aprili 1 kila mwaka - imekuwa ikiadhimishwa kwa karne kadhaa na tamaduni tofauti, ingawa asili yake halisi bado ni siri.

Mila ya Siku ya wajinga ni pamoja na kuwadanganya watu au kuwafanyia au utani wa vitendo mbalimbali.

Wakati historia yake halisi imeghubikwa na siri, kukumbatiwa kwa utani wa Siku ya Wajinga ya Aprili Mosi na vyombo vya habari kumehakikisha maisha marefu ya likizo hii isiyo rasmi.

Je siku hii iliasisiwa lini na kwa madhumuni gani?

Siku hii ilianzaje?

Baadhi ya wanahistoria wanakadiria kwamba ya Siku ya Wajinga ilianza mwaka 1582 wakati ambapo Ufaransa ilibadili kalenda ya Julian na kuhamia kwenye kalenda ya Gregorian.

Kubadilika huku kwa kalenda kulibadilisha tarehe za mwaka na hivyo nchi hiyo ikaanza kusherehekea mwaka mpya Januari Mosi badala ya Aprili.

Lakini kwa bahati mbaya maamuzi hayo ya kubadili kalenda ya mwaka yaliyofanywa na Papa Gregory wa 13, hayakuwafikia wananchi wote wa Ufaransa na badala yake baadhi wakaendelea kusherehekea mwaka mpya Aprili Mosi. Hivyo basi waliosherehekea mwaka mpya Aprili Mosi, waliitwa wajinga na siku hiyo ikaitwa ya wajinga.

Watu ambao walichelewa kupata habari au walishindwa kutambua kuwa mwanzo wa mwaka mpya ulikuwa umehamia Januari 1 na waliendelea kuusherehekea katika wiki ya mwisho ya Machi hadi Aprili 1 wakawa wanafanyiwa utani na wongo wakiitwa "Wajinga wa Aprili.

"Mizaha hiyo ilikuwa ni pamoja na kuwekewa karatasi zilizochongwa kwa muundo wa samaki migongoni mwao na akiitwa "poisson d'avril" (samaki wa Aprili), iliyosemekana kuashiria samaki wachanga, waliovuliwa kwa urahisi na mtu anayeweza kuhadaiwa kwa urahisi.

Wengine wanaihusisha siku hii na sherehe za Warumi zilizoadhimishwa Aprili Mosi ambapo watu walivaa nguo za ajabu na za kuchekesha wakati huo, ilianza kusherehekewa Machi 25 na kumalizika Aprili Mosi.

Baadhi ya wanahistoria wa Uingereza wameihusisha sikukuu hii na sherehe zinazofanywa kila Aprili Mosi nchini India ambapo watu walirushiana vitu na kuchafuana kwa keki au rangi k**a sehemu ya utani.

Source:BBC SWAHILI,

19/02/2022

Kimeishaanza kubamba ndani ya Arena, maeneo ya hapa Nyasaka Centre, fanya k**a unasogea kupata vibe la kutosha kwa damage ya sh000 yani zero kiingilio na utapata serengeti lite moja bure getini. Hujachelewa vibe liko k**a lote.



youthvibing

03/02/2022

JIUNGE NA PROGRAMU MPYA.

Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) tumeanzisha programu mpya za masomo ambazo mitaala yake imefanyiwa utafiti wa kina na Wataalamu wabobezi kwenye nyanja ya Biashara na kuhakikisha zinaendana na soko la ajira kwa sasa na hapo baadae.

Programu hizi zitakuwa zinapatikana kwenye kampasi zetu (Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza na Mbeya) kwa mwaka wa masomo 2022/2023 karibu sana.

Kwa elimu hii inayotolewa na cbe nimeamini kweli elimu haina mwisho. Unaachaje sasa kwa mfano kurudi masters k**a umemaliza Bach kuisoma hilo likozi lizuri hapo la entrepreneurship and innovation.

In the comment section below niambie ni kozi gani ungependa kuisoma k**a una nafasi,

Waweza ni dm k**a Kuna kozi ungependa kuifahamu zaidi au unataka kujua inahusiana na nini!
NB:course hizi zimeongezwa,course zilizokuwa zikitolewa hapa chuoni bado zipo.

Want your university to be the top-listed University in Mwanza?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Mwanza
33201