MBUKE TIMES

MBUKE TIMES

Share

11/05/2021

JINSI YA KUWAFANYA WATEJA WAKUTAFUTE BADALA YA WEWE KUWATAFUTA
Kuna njia ya kisasa na bora ya kutafuta wateja ambayo k**a ukiifahamu, ukaifanyia kazi kwa kuzingatia miongozo yake utafaidika sana kupata wateja haswa kupata wateja mtandaoni.
Njia hiyo tunaiita Inbound Marketing.
Wazo kuu katika njia hii ni kuwapa walengwa wako machapisho yenye thamani kwao - yaani yenye kuwatoa sehemu fulani kuwaweka sehemu nyingine bora zaidi.
Machapisho yatakua na thamani kwa walengwa wako pale yatakapojibu kero zao, shauku zao, kuwapa miongozo na kuboresha ufahamu wao.
Unapowapa watu machapisho ya thamani unachofanya ni kuwachuja akina nani haswa unapaswa kuwasiliana nao, maana k**a sio walengwa wako, hawatoona yathamani. Pia wewe mwenyewe utajituma kufikiria yale muhimu tuu kwa aina ya watu unaowalenga.
Mfano wewe unauza samaki. mapisho la thamani kwa walengwa wako yaweza kuwa faida za samaki, jinsi ya kuwaandaa samaki, mapishi tofauti ya samaki, jinsi ya kujua k**a samaki wameharibika au la, n.k
Hivyo basi jikite kuchapisha mambo ambayo yanawagusa walengwa wako. Shida ya wajasiriamali wengi wamekua watu wa kufuata mkumbo, kupost kila kitu au kupost wanayoyapenda wao na sio yanayowalenga wateja wao watarajiwa.
Usipopost yanayowalenga wateja wako unaweza jikuta unawavuta kwako watu wengi ambao, kweli wanaweza kulike na kucomment kwenye posts zako, lakini wasije nunua bidhaa zako siku ukitangaza kwakua hao sio watu wenye 'interest' au uwezo wa kununua bidhaa zako.
Lingine la kusisitiza katika njia hii ya kupata wateja ni kuwa na subira. Unahitaji kuweka machapisho mengi, kwa muda mrefu ili ujenge kukubalika, kupendwa na kutegeemewa, kabla watu wenyewe hawajaanza kukutafuta kuuliza unauza nini au wakuulize watapataje bidhaa zako.
Hii ni njia bora sana ya kupata wateja hasa huku mtandaoni ambapo watu wamejaa wasiwasi wa kutapeliwa na kukosa imani na ubora wa bidhaa zinazouzwa.
Machapisho yako bora yatakusaidia pia kujenga brand bora ambayo itakusaidia kuwafanya watu wakuamini, na hata wewe pia uweze kuwa na bei zenye maslahi.
BOFYA LINK uendelee kujifunza mambo ya ujasiriamali kupitia WhatsApp https://chat.whatsapp.com/K3x6eo7Ri9g4TXrEPr6ed7

29/12/2020

Wengi wanatumia mitandao kutangaza bidhaa au huduma zao, lakini hawaoni matokeo mazuri wanayotarajia.

Siri ya mafanikio ipo kwenye matumizi sahihi ya mitandao katika kujenga imani na brand ya biashara yako na wewe kwanza kabla ya kuwaza kuuza.

Soma points hizi na karibu kwa masomo zaidi na ushauri kupitia WhatsApp 0623 029 683.

30/07/2020

HIKI NDICHO CHA KUUZA K**A WEWE NI MJASIRIAMALI
Ukitambua mbinu hii basi unaweza uza chochote kile na ukapata faida. Acha kujiuliza ufanye biashara gani, badala yake anza kujiuliza watu wanahitaji nini, watu wana changamoto gani , utoaji mzima wa huduma na uuzaji wa bidhaa zilizopo una changamoto gani.

Siri ya kuuza chochote, ni kutambua changamoto na mahitaji ya watu, ukajua namna bora ya kuwaeleza na kuwaonyesha, na wakaamini unacho cha kutimiza mahitaji yao au kutatua changamoto zao. Unachohitaji sio tuu kumuuzia mteja leo, unahitaji uweze kumuuzia na kesho , na siku zijazo.Unahitaji wateja ambao wataambiana .

Mfano wewe ni fundi seremala, mtu anakuja kukuambia umtengenezee meza ya bei kubwa tuu, tena meza yenyewe sio ya kulia chakula wa kusomea, ni meza tuu itakayokua k**a pambo sebuleni (sitting room) kwake. Ila wewe unaitengeneza bila umakini mkubwa , na kweli unaitoa meza ila haina ubora mzuri wa mtu kuiangalia akaona fahari.

Hapo wewe ulichoangalia ni kuwa mteja anataka tuu meza, haukuwaza hivi kwanini haswa anataka meza. Ila ungejua kuwa anachotafuta mteja ni ufahari na sio tuu meza, usingempatia meza ili mradi, ungejikita kuifanya meza hiyo iwe ya kifahari pia.

Want your business to be the top-listed Business in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Soweto
Moshi
00255