MOSHI FM online

MOSHI FM online

Share

15/04/2026

Kichanga kilichozikwa siku ya jumamos tarehe 11 Aprili katika Kata ya mbokomu, Kijiji cha korini kusini, kitongoji cha Machadi kusini (Doreen Edward) mwili huo umefukuliwa leo tarehe 15 Aprili chini ya ulinzi wa jeshi la polisi Mkoani Kilimanjaro, Baada ya kugundulika kuwa mwili ulizikwa sio wa Kichanga Emanuel Mrema k**a Familia ya George Mrema ilivyodhani.

27/03/2026

Mlinda mlango wa Klabu ya Yanga, Djigui Diarra amefungiwa mechi tatu (3) pamoja na faini ya shilingi milioni mbili (Tsh. 2,000,000/=) kwa kosa la kumshambulia mwamuzi katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Diarra pia ametozwa faini ya milioni mbili (Tsh. 2,000,000/=) kwa kosa la kuonesha kidole cha kati wakati wa kuondoka katika eneo la uwanja .

_______________________________________
Tunakupa unachostahili Mwanafamilia MOSHI FM

27/03/2026

Zaidi ya wasanii 130 wilayani Mkuranga mkoani Pwani wamepatiwa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo katika fani zao, hatua inayolenga kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Huduma za Taasisi kutoka Bodi ya Filamu Tanzania, Asha Katila, amesema lengo ni kuwajengea uwezo wasanii ili waweze kushindana katika soko la filamu linalokua kwa kasi.

Baadhi ya wasanii pamoja na wadau wa sekta ya filamu wameeleza kuwa mafunzo hayo yana tija kubwa, yakichangia kuboresha ubora wa kazi zao na kuongeza fursa za ajira na kipato.

Kutokana na mwitikio mkubwa wa washiriki, Bodi ya Filamu Tanzania imesema itaendelea kuendesha mafunzo k**a hayo katika mikoa mbalimbali nchini ili kuwafikia wasanii wengi zaidi.

_______________________________________
Tunakupa unachostahili Mwanafamilia MOSHI FM

27/03/2026

Rais Donald Trump wa Marekani amesema Iran ilimwomba asitishe mashambulizi kwa siku saba kwenye viwanda vya nishati, lakini ameipa siku kumi, na Tehran "ikamshukuru sana" kwa hatua hiyo.

Awali, Trump alitangaza kwenye mtandao wa Truth Social kwamba ataongeza muda wa kusitisha mashambulizi katika maeneo ya viwanda vya mafuta vya Iran kutoka siku tano hadi wiki mbili.

Muda wa kusitisha mashambulizi ulipangwa kuisha kesho, lakini hatua hii inamaanisha kuwa usitishaji huo utaendelea kutekelezwa hadi Aprili 6.

Akizungumza kwa njia ya simu na Fox News hivi karibuni, Trump alisema Marekani iko kwenye mazungumzo na Iran ambayo yanaendelea "vizuri".

_______________________________________
Tunakupa unachostahili Mwanafamilia MOSHI FM

Photos from MOSHI FM online's post 27/03/2026

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) chini ya Mwenyekiti wake Ado Shaibu Ado (MB) imetembelea Halmashauri ya Wilaya ya Magu mkoani Mwanza kwa ajili ya kukagua miradi ya Ujenzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Magu na Shule ya Sekondari ya Magu.

Kamati imeiagiza Halmashauri ya Magu kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika ikiwemo kufanyia kazi dosari zilizobainika katika ujenzi.

Kamati imesisitiza pia umuhimu wa Halmashauri kuzingatia taratibu za kisheria na kimkataba katika kuwasimamia wakandarasi.

“Ni lazima tuuvunje utaratibu wa kusubiri Kamati ya LAAC au viongozi waandamizi wa TAMISEMI waje ndio kazi dosari zionekane na kufanyiwa kazi. Wataalam katika Halmashauri wafanye kazi kwa weledi kuhakikisha kuwa wanasimamia viwango vinavyotakiwa kwenye ujenzi,” alisisitiza Ado.

________________________________________
Tunakupa unachostahili Mwanafamilia MOSHI FM

Want your public figure to be the top-listed Public Figure in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


933 Barabara Ya Ndesamburo, KDC
Moshi