Twibbu herbal

Twibbu herbal

Share

TWIBBU HERBAL 🥒🥑 04/12/2022

*🌱CHAKULA CHENYE AFYA🌱*

Elimu ya chakula chenye afya ni elimu inayotafiti viambata vya chakula anachokila binadamu na athari zake kwenye afya ya mwili, chakula tunachokila kinabeba virutubisho maarufu ambavyo ni :
1-Proteins
2-Carbohydrates
3-Fat

Virutubisho hivi vitatu ndio nguzo mama za kuzalisha nishati na kujenga mwili na seli zake, lakini pia kuna virutubisho vingine vinavyopatikana kwenye chakula kazi yake ni kukamilisha kazi ya virutubisho vitatu vilivyotangulia na virutubisho hivyo ni :
1-vitamins
2-Minerals
3-Fiber

Tambua kwamba maji ndio kirutubisho muhimu zaidi na hiyo ni kwasababu virutubisho vyote tulivyovitaja haviwezi kufanya kazi yake isipokua kwa kuwepo maji.

Basi itoshe kujua kwamba maji ni nguzo ya uhai, na mwili hauwezi kufanya kazi yake bila maji.

Sasa turudi kuuangalia mwili unahitaji nini? Mwili unahitajika :
1-Maji.
2-wanga.
3-Mafuta.
4-Vitamin.
5-madini
6-nyuzinyuzi.

Kwa hiyo chakula kizuri ni muhimu kwa ajili ya kuhifadhi virutubisho hivi ndani ya mwili ili mwili ubaki salama na wenye afya, na kukisemwa chakula kizuri hakumaanishwi kitamu mdomoni, kunakusudiwa chenye virutubisho sahihi vinavyohitajiwa na mwili.

Na hakuna mjadala kwamba magonjwa mengi yanatokana na upungufu wa virutubisho, kila kirutubisho kina kazi yake mwilini hivyo kuzidi au kupungua kwa kirutubisho kunapelekea kupata tatizo mwilini.
--------
Imeletwa na :Abuu Khaythama Swabuni.

*TWIBBU HERBAL*
+255674916068
______
https://chat.whatsapp.com/BIQf62xvjtXBF0kRgdcLOl
_____
https://www.facebook.com/twibbuherbal
____
https://t.me/twibbu_herbal

TWIBBU HERBAL 🥒🥑 WhatsApp Group Invite

04/12/2022
Want your practice to be the top-listed Clinic in Moshi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Moshi