Ujenzi on Point
13/04/2024
FAIDA ZA KUJENGA KWA MATOFALI YA KUCHOMA.
Kuwa na nyumba ni malengo ya watanzania wengi.Iwe ni kwa kuanza maisha, kuanza familia na muenzi wako, au kuweza kuhama katika nyumba ya kupanga na kuwa na mahali utakapoita nyumbani. Nyumba ina umuhimu sana katika maisha ya wanadamu, na kwa wengi ni malengo yao kuu. Kujenga Nyumba bora iliyoimara inahitaji umakini sana katika kujenga na kupanga ujenzi wa nyumba yako ijayo. Hivyo ni muhimu sana kujua aina ya matofali bora katika ujenzi wa Nyumba ya ndoto zako. Hivyo leo nitakueleza faida za kujenga kwa matofali ya kuchoma.
Matofali ya kuchoma hayana gharama.
Ujenzi wa matofali ya kuchoma ni ujenzi wa bei nafuu na hauhitaji kipato kikubwa kujenga nyumba kwa matofali ya kuchoma, gharama hizo huwa ndogo kutokana na gharama ndogo ya matofali hayo ambayo huwa kati ya 150,200 300,400 hadi 600 katika bei ya soko ukilinganisha na gharama ya tofali ya cement ambayo gharama yake huenda hadi sh. 2000 kwa tofali moja katika bei ya soko.Matofali hayo hayahitaji watu wengi kwenye kujenga kwa kuwa hazina uzito mkubwa, ujenzi wake hauitaji watu wengi hivyo gharama ya kujenga hupungua.
Matofali ya kuchoma ni Imara.
Matofali ya kuchoma yanauwezo wa kudumu kwa miaka mingi kuliko matofali ya cement. Kwa kawaida matofali ya kuchoma yanauweza kudumu kwa miaka hadi mia tatu bila kuharibika wala kububujuka. Ulikilinganisha na matofali ya cement ambayo kudumu kwake ni kati ya miaka sitini hadi mia.Hivyo nyumba ya matofali ya kuchoma inauwezo wa kudumu kwa miaka mingi zaidi kuliko ya simenti.
Matofali ya kuchoma yana muonekano mzuri.
Matofali ya kuchoma huwa na muonekano mzuri wa kuvutia,Matofali ya kuchoma hayahitaji rangi wala finishing kufanya eneo la nyumba kupendeza, bali matofali haya yanauwezo mkubwa wakutunza mvuto wake k**a rangi na muundo, kwa miaka mingi bila kupoteza uhalisia na upya wake. Ndio maana eneo lijengwalo kwa matofali ya kuchoma linauwezo wakuonekana kwamba ni mpya ingawa inamiaka mingi.
Hivyo ni vyema kuchanganua na kufahamu ubora na umuhimu wa matofali ya kuchoma katika ujenzi wa nyumba bora na imara. Kwa kuwa wengi wanandoto za kuwa na nyumba iliyo na mvuto,hivyo matofali ya kuchoma ndio suluhisho hilo.
Kwa mahitaji ya Ramani mbalimbali na ushauri kuhusu ujenzi Tuwasiliane 0742295125 Call/WhatsApp na 0676056663 Call/SMS Au Bonyeza link hapo chini 👇https://wa.me/message/I26USNZKJXAVK1
13/04/2024
Pata Huduma ya Ramani na ushauri kuhusu ujenzi
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Moshi