SEPRO
05/09/2022
*Wazee wanasema "Usimtese mtu ili umfurahishe rafiki yako unayempenda." Rafiki yako akija kwako akikuambia anamchukia mtu fulani, na ikiwa unayeambiwa una mamlaka na yule anayechukiwa, usiende kumtesa anayechukiwa ili rafiki yako afurahi. Wasaidie wapatane. Usisahau machozi ya anayeteswa hugeuka mafuriko yakukusomba baadae. Kuwa makini na kujaribu kuwazika watu kwenye matope, wengine wanachipua k**a mbegu iliyopandwa kwenye matope. Usisahau wanyonge hutetewa na Mungu. Goliati alikuwa na nguvu lakini hakuwa na Mungu, Daudi hakuwa na nguvu ila Mungu alikuwa nguvu yake. Epuka kupigana na malaika waliowekwa na Mungu kati ya watu.
12/06/2022
HITAJI LA MAFANIKIO
Nini hitaji la mafanikio yako?
Kila mmoja anahitaji la mafanikio yake ya kimaisha lakini kuna hitaji kuu ambalo ni lamsingi katika maisha yetu pale tulikosapo tu basi huwa ndiyo mwisho wa maisha yetu.Wapo wataalamu mbali mbali walioweza kuchunguza na kuchambua maisha ya mwanadamu tangu hatua ya kutunga mimba hadi hatua ya kifo.Mfano wa wachunguzi hao juu ya maisha ya wanadamu ni Abraham Maslow,
Mwana saikolojia Abraham Maslow ameweza kuainisha baadhi ya mahitaji muhimu ambayo ni yamsingi kwa mwanadamu kuyapata.Kuna ngazi kuu tano za mahitaji ya mwanadamuna ngazi hizo zilifanyiwa utafiti na Abraham Maslow mwaka 1907 mpaka mwaka 1970 na kuzipa jina la Maslow Hierarchy of needs, yaani ngazi za mahitaji ya mwanadamu. Lengo kuu ilikuwa ni kutaka kujua ni nini kinachofanya mtu afanye jambo au kitu fulani.Ngazi hizo tano ni :
1. Mahitaji muhimu (Biological and physiological needs) mfano chakula, Malazi, afya na hewa.
2. Hitaji la kiusalama (Safety needs) mfano ulinzi.
3. Hitaji la kijamii (Social needs) mfano upendo nakupendwa.
4. Hitaji la heshima (esteem needs)
5. Hitaji kujitosheleza na kujitambua (Self actualization needs).
Hitaji la mafanikio yetu kwa ujumla ni kwaajili ya kutimiza hitaji kuu la mwili ili uwe imara katika kutekeleza shughuli ya nyingine za uzalishaji mali.Tunatakiwa kuutimizia mwili mahitaji hayo matatu ndipo tuweze kuzalisha ziada kwaa ajili ya kusaidia wengine ambao hawajuwi wapi pakuanzia na wale ambao wanamahitaji maalumu ambayo ni yakuzaliwa nayo yanayowafanya wasiweze kuzalisha chochote.Baada ya kutimiza hitaji la mwili ndipo mahitaji mengine huchukua nafasi ya maisha ya mtu hadi kufikia hatua ya kuwa na familia au kuwa na uwezo wa kumiliki watu kwa ajili ya kutafuta upendo, hadhi na usalama.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Morogoro