Professor Jay
09/04/2026
"JAY ALIVYOTUNUKIWA UPROFESA WA BONGO FLAVA!
MIEZI ya utawala wa Funga Kazi 2000 ilikoma mwaka 2001 ulipowasili. Jay hakutaka kingdom itetereke. Aliikabidhi domain albamu “Machozi, Jasho na Damu”, ikiwa solo project nje ya HBC. Introduction single ni “Bongo Dar es Salaam”. Again, storyteller N***a Jay, aliweza kuifanya Afrika Mashariki i-bow kulielekea jina lake, kwa jinsi alivyoisimulia Dar es Salaam na visanga vyake ndani ya beti tatu kwa ufundi wa hali ya juu. Lady Jaydee akanogesha hook.
Unauza cheni bandia, unalipwa pesa feki, mitaa ya Dar unakutana na bibi vizee wanafanya ukahaba, unapita Mwananyamala kizembe, unapigwa roba ya mbao, viwanjani unadata warembo wote bien, unashindwa kumtofautisha changudoa na mtoto wa kishua, katikati ya jiji unagongewa hadi mhuri wa Ikulu, halafu watu wanaendesha exotic cars, wakati maisha ya Mbongo ni danga-chee. Jay aliua kila line, beti kwa beti, visa na matukio yote, ndani ya Bongo Dar es Salaam.
“Jina Langu”, ni release namba mbili ya Machozi, Jasho na Damu. K**a kulikuwa na mtu aliyekuwa bado na shaka kuhusu utaalamu wa Jay kwenye mbanga za Hip Hop, basi Jina Langu ilimnyoosha. Kisha, bila huruma, Jay akaachia “Ndio Mzee” ft Juma Nature na Babu Ayubu. Jay alitumia sanaa kuionesha jamii kamba za wanasiasa vipindi vya uchaguzi.
Ndio Mzee ni pini lingine lililowalazimisha wazee kumpenda Jay. Alikuwa kijana mdogo, lakini akili na maarifa vilizidi umri. Ni hapo the everlasting DJ, John Dilinga Matlou, akahoji for what reason aendelee kuitwa “N***a Jay”, wakati kazi yake ina hadhi ya kiprofesa?
Pwani ya Mashariki hadi Lake Tanganyika. Kanda ya Ziwa mpaka Nyanda za Juu Kusini. Kilimanjaro na Meru, himaya za katani na korosho. Maskani za alizeti na zabibu, Unyanyembe na East Africa yote. Kauli ya DJ JD ilipokelewa unanimously. Mitaa ikanyoosha mikono kumtunuku Jay Uprofesa. Ni profesa wa muziki. Profesa wa Hip Hop. Profesa wa Bongo Flava. Fupisha, tamka Profesa Jay.
Jay ni foundational lifter of Bongo Flava. Do you still defy that? Mei Mosi, 2026, ni siku ya Bongo Flava Honors kudhihirisha kwa nini Jay anaitwa Profesa. Curator Sugu the Jongwe ataongoza shughuli. Makutano ni 710 Garden, Kawe Beach.
Ndimi
29/03/2026
"PROF JAY; THE FOUNDATIONAL LIFTER OF BONGO FLAVA
Nyerereland ilikuwa tambarare utadhani uwanda wa chumvi wa Salar de Uyuni. Laini mithili ya jiwe la Talc. Mserereko k**a kutembea juu ya polished marble yenye povu la sabuni. Tanzania was beautiful, utamu wake ni saresare na Thaumatin.
Ukimwi ndiyo tu ulileta sokomoko, lakini raia walichagua kuishi nao. Ugonjwa hatari ulikuwa Malaria. Siyo sasa mabalaa ya magonjwa yasiyoambukiza, saratani, vifo vya ini na figo hadi kwa infants. Aisee, naimiss Bongoland ile, iliyokuwa na mguso halisi wa Kitanzania. Ukarimu, ushirikiano, mshik**ano, vilikuwa jadi. Mapenzi yalikuwa ya moyoni. Siyo sasa pesa ndiyo inaamua upendwe au utendwe.
Late Gen X na early Gen Y (Millennials), ndiyo makundi rika yaliyotengeneza vijana kwenye mzunguko. Ni kizazi cha mapinduzi ya sanaa na ajira. Wateule wachache walitambua mapema kuwa dunia inakwenda kasi, na sound mpya ya muziki ilihitajika kuhudumia kaumu.
Wape heshima yao. Ni business-minded cohort. Walikuwa mbele ya muda kung’amua kuwa sound mpya ingevutia halaiki, na hivyo ndivyo pesa hutegwa. Mchakato haukuwa rahisi. Kenge walijimiksi kwenye mishemishe za mamba. Kila kitongoji kikawa na underground rappers.
Jamii ikaacha kuwatafsiri wavuta bangi kwa moshi, kipimo kikawa Rap. Kila aliyerap, alitiwa hatiani kijamii kuwa mtumia mihadarati. Halafu sasa, vipaji vikachanganyika na vioja. Wenye vipaji wanarap, wa vioja wanatukana na kufokea watu. Haikuwa kazi rahisi kuifikisha Swahili Rap mainstream.
Stiff boycott ya wazazi. Hawakutaka watoto wao wafanye Rap. Waliorap walionekana broke dreamers. Hawakuwa na kitu, ila waliyaota maisha ya successful American rappers. Wapo waliotabiri wimbi la wagonjwa wa akili kupitia vuguvugu la Hip Hop Tanzania.
It takes a genius to make the impossible possible. Kijana mteule, aliyebarikiwa karama kubwa, jina lake Joseph Leonard Haule. Akitembea na monikers za Jay Hustle na N***a Jay. Kwa tungo moja tu, “Chemsha Bongo”, aliyeyusha kila neno lililotokana na fikra hasi kuhusu Swahili Rap.
Mei Mosi, 2026, Jay atatunukiwa hadhi ya Bongo Flava Honors, kutambua mchango wake wa thamani. Sugu the Jongwe will host. 710 Garden, Kawe, ndiyo spot.
Ndimi Luqman MALOTO".
03/03/2025
Tukiwa kwenye mwezi wa Figo duniani, K**a Mwenyekiti wa taasisi ya inayotekeleza programu ya AFYA AWARENESS CORPORATE itafayofanyika March 14, nimekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Masoko , Elimu ya afya kwa umma ni kipaumbele 2025/26
duniani.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the establishment
Website
Address
Morogoro