Tanmark Co.Ltd

Tanmark Co.Ltd

Share

12/06/2023

Kazi yetu nyingine ya consultation iliyokuja na matokeo makubwa! We are now in Babati! Tunaendelea kukudumia sasa kuna viwanja 3,250! Matumizi mbalimbali; makazi; biashara; shule; shopping malls; petrol stations nk!
Wasiliana na ofisi za Babati kwa namba hizo hapo; 0754426403! Ni hivi sqm tshs 2,500 ni kwamba kiwanja cha mita 20 kwa 30! Sqm 600 utapata kwa Tshs 1,500,00/= na kwa Tshs 3,000 kwa sqm unapata kiwanja kwa Tshs 1,800,000/= hakuna udalali biashara zote zitafanyika kupitia ofisi za halmashauri ya mji wa Babati! Wekeza sasa 1.5-1.8mil ni hela ya simu kwa sasa ila itaweza kumfaa sana mwanao! karibuni sana๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ฟ @ Tanmark we consult: we sell (hii ni kanda ya kaskazini) kila kanda tutafika) stay tuned kanda ya ziwa

28/05/2023

Tuzungumze "Faida za Uwekezaji kwenye Mali isiyohamishika" au Real Estate kwa Kiingereza.

Uwekezaji kwenye "Mali isiyohamishika" k**a ilivyo kwenye aina nyinginezo za uwekezaji, huja na changamoto nyingi ikiwamo kushuka thamani ikiwa makadirio na hesabu hazikufuatwa sawasawa. Hilo tutakuchanganulia ukitutumia sms, WhatsApp ama DM kwa maswali.

REITs (Real Estate Investment Trusts), ni amana za uwekezaji wa mali isiyohamishika, na ni mojawapo ya njia rahisi zaidi za kuwekeza katika mali isiyohamishika. Kwa nini? Ukiwa na REIT, unawekeza katika mali isiyohamishika bila kuwa na wasiwasi kuhusu kutunza, kuendesha au kusimamia majengo husika, kazi hiyo hufanywa na kampuni zinazomiliki mali isiyohamishika, kitu chochote kuanzia fremu za Biashara ya rejareja hadi majengo ya ghorofa, hoteli, ofisi au maghala.

Unaponunua katika REIT, unanunua sehemu ya mali hizi. Ni kidogo k**a kuwekeza kwenye hazina za kawaida (mutual funds), au Biashara ya hisa, isipokuwa REIT inahusika na mali isiyohamishika. Unaweza kupata pesa kutoka REIT kwa njia mbili: Kwanza, REIT hufanya malipo ya gawio ya kawaida kwa wawekezaji. Pili, ikiwa thamani ya jengo ama mradi husika itaongezeka, unaweza kuuza uwekezaji wako kwa faida. Unaweza kuwekeza kwenye REIT k**a kuwekeza kwenye hisa: REIT huweza hata kuorodheshwa kwenye soko kuu la hisa kupitia "Uwekezaji wa Majengo", biashara ambayo haijawa kubwa hapa Tanzania.

Faida zake huonekana kupitia malipo ya kila mwezi kupitia makusanyo ya Kodi, gawio kutokana na faida za jumla, na pia uhakika wa faida ikiwa thamani ya jengo hupanda na kuuzwa kwa faida zaidi ya makadirio.

Kwa maswali, maoni na ushauri. Tutumie sms, WhatsApp au DM kwenye mitandao ya kijamii.

TanMark, njoo tuzungumze

10/05/2023

Kabla ya kununua nyumba, lazima uwe na uwezo wa kuthamini gharama ya uwekezaji wa nyumba hiyo ili kuamua faida inayoweza kupatikana kwenye uwekezaji wako.

Utahitaji kuzingatia mambo kadhaa ikiwamo;
1. Kutafiti thamani ya nyumba/makazi kwenye eneo husika. Elewa maeneo ambayo yanapanda ama kushuka thamani (na haya yapo kwenye kila mji), na kwanini, yaani elewa "trend" ya soko. Unashauriwa kununua nyumba kwenye maeneo yenye ukaribu na taasisi za umma k**a shule, hospitali, na pia yenye uhakika wa huduma za jamii k**a maji, Umeme na barabara za mitaani, hii itasaidia kuongeza thamani ya jengo. Ulizia ikiwa kuna mradi wowote mpya (k**a ujenzi wa Hotel na kadhalika) kwenye huo mtaa na kadhalika.

2. Tafuta kujua nyumba/makazi yanayouzwa kwa bei nafuu zaidi ya mengine ili kupata unafuu kwenye gharama zako za jumla. Pia hakikisha hakuna mgogoro kwenye nyuma/makazi hayo kwa namna yoyote.
3. Tembelea na ukague nyumba/makazi hata mtaa husika kabla ya kufikia maamuzi. Tumia Wataalamu wa ukadiriaji kujua thamani ya jengo, wastani wa gharama za ukarabati na kadhalika ili ikusaidie kulinganisha na bei ya soko na kukadiria faida.

4. Ni vyema ikiwa utakuwa na mteja kibindoni ama unaye wakala wa kuuza majengo yako ili pesa yako isikae mahala pamoja muda mrefu.

TanMark, njoo tuzungumze Mali isiyohamishika (Real Estate).

08/05/2023

Moja ya biashara zinazokua kwa kasi kwenye miji inayokua, ni kununua na kukarabati nyumba za zamani kabla ya kuziuza tena. Ingawa hii ni biashara inayoweza kuwa na faida kubwa na ya haraka, yako mambo kadhaa ya kuzingatia na hapa tutakutajia machache!

Kwanza fuatilia kujua kwanini nyumba husika inauzwa. Nyumba nyingi za zamani hapa Tanzania ni za urithi na zina migogoro ya mirathi na kadhalika.

Jihakikishie mnunuzi/mpangaji wa nyumba husika kabla hujawekeza fedha zako. Hii ni muhimu kwa vile ikikaa muda mrefu bila kutumika itaanza kuchakaa na utalazimika kuendelea kuweka pesa kuitunza.

Zingatia kununua eneo ambalo huduma za jamii zimefika na hata limekwishafikiwa na miundombinu yote ikiwamo barabara za lami. Hii ni kwa vile thamani ya nyuma iliyokarabatiwa kwa mteja wako ni pamoja na ufikikaji wake wa haraka na ukaribu wake kutoka shughuli za mteja wako.

TanMark, njoo tuzungumze

Want your business to be the top-listed Realtor/realty Service in Morogoro?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Dodoma Road
Morogoro