Kiwandanitz
13/08/2025
Je, Mchele Unao Kula ni Bora, Salama na Safi ?
Kwa mujibu wa Tanzania Bureau of Standards (TBS), TFDA, na tafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA), mchele bora hujulikana kwa sifa zifuatazo:-
🔍 1️⃣. Muonekano wa Chembe za Mchele
Mchele bora kwa mlaji ni lazima chembe zake ziwe sawa kwa umbo, siyo zilizopasuka pasuka.
Hauna uchafu k**a changarawe, unga mwingi au mabaki ya maganda.
🔬 2️⃣. Harufu ya Asili
Mchele bora hauna harufu ya kemikali, ukungu au mafuta mafuta.
Mchele wa aina ya aromatic k**a wa Kilombero au Mbeya una harufu ya kupendeza hata kabla ya kupikwa.
🌾 3️⃣. Usafi na Usalama wa Afya
Umetuzwa kwenye ghala safi, kavu, lenye uingizaji hewa wa kutosha.
Unathibitishwa na nembo ya TBS au una cheti cha ubora kutoka bodi husika.
📦 4️⃣. Ufungaji Sahihi
Mchele wa kifungashio una taarifa sahihi za:-
1. Jina la kampuni au mkulima
2. Mahali kilimo kilipofanyika
3. Tarehe ya kusindika na mwisho wa matumizi
4. Alama ya ubora (TBS/TMQ)
📊 TAKWIMU :-
Tanzania huzalisha zaidi ya tani milioni 2.6 za mpunga kwa mwaka, lakini bado baadhi ya mikoa huagiza mchele kutoka nje kutokana na ukosefu wa taarifa sahihi kwa walaji kuhusu mchele bora wa ndani.
Zaidi ya asilimia 38 ya walaji wa mijini hununua mchele wa bei ya juu kwa dhana kuwa ndio bora, wakati mikoa ya uzalishaji hutoa mchele mzuri kwa gharama ya chini hadi 30% – 40%.
💬 Dkt. Hadija Mwakalukwa – Mtafiti Kutoka SUA Anasema:-
“Wateja wanatakiwa kuchagua mchele uliopitia usindikaji rasmi na uliofungwa vizuri. Harufu, rangi na usafi vinaweza kuashiria ubora, lakini muhimu zaidi ni kufuatilia alama za ubora na maeneo ya uzalishaji”
Kwa kufanya hivyo, utalinda afya ya familia yako, kuokoa gharama, na kuchangia katika kuinua wakulima wa ndani.
14/02/2025
Fahamu Kwanini Kila February 14 Huadhimishwa ni Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day) ?
Tumaini langu upo poa.............
Karibu tufahamu kwanini kila ifikapo February 14 Dunia huadhimisha ni siku ya wapendanao (Valentine’s Day) ?
Twendeeeee tufahamu 👇
Siku ya wapendanao, au Valentine’s Day, huadhimishwa kila mwaka tarehe 14 Februari duniani kote k**a siku ya kuonesha upendo, hasa kati ya wapenzi.
Kumbukizi ya siku hii imechochewa na historia ya kidini na tamaduni za Kirumi.
Asili ya Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day)
Asili ya Valentine’s Day inamhusu Mtakatifu Valentine, ambaye alikuwa Padri wa Kirumi katika karne ya 3.
Mfalme Claudius II wa Roma aliamua kuwa askari wa kijeshi hawapaswi kuoa, akiamini kuwa ndoa huwafanya kuwa dhaifu vitani. Lakini Padre Valentine alikaidi agizo hilo na akaendelea kuwaoza/kufungisha ndoa askari hao kwa siri.
Alipogunduliwa, alik**atwa na kuhukumiwa kifo.
Alipokuwa gerezani, aliandika barua ya kuaga kwa binti wa mlinzi wa gereza, ak**alizia na maneno "From your Valentine", ambayo bado hutumika mpaka leo.
Valentine aliuawa tarehe 14 Februari, mwaka 269 BK, na hivyo jina lake likahusishwa na upendo wa kimapenzi.
Mila za Kirumi (Lupercalia)
Kabla ya Ukristo, Warumi walikuwa na sherehe ya Lupercalia, iliyofanyika Februari 13-15, kusherehekea uzazi na ndoa. Wakati Ukristo ulipoenea, Kanisa Katoliki lilitaka kuondoa mila za kipagani na badala yake likaifanya Siku ya Mtakatifu Valentine rasmi mnamo karne ya 5 chini ya Papa Gelasius I.
Hamasa ya Valentine’s Day Duniani
Katika enzi za kati (Middle Ages), watu walianza kuihusisha siku hii na upendo wa kimapenzi.
Mshairi Geoffrey Chaucer wa Uingereza aliandika mashairi yanayohusisha Valentine’s Day na upendo wa wapenzi.
Hii ilichochea kuenea kwa kumbukizi ya siku ya Valentine’s Day.
Pia mnamo Mwaka 1840, mwanamke aitwaye Esther Howland kutoka Marekani alianzisha biashara ya kadi za Valentine's Day 💌 na kuzifanya kuwa maarufu sana.
Katika Karne ya Leo................
Valentine’s Day ni siku kubwa kwa kumbukizi ya upendo (Siku ya Wapendanao) ambapo watu hununua maua, chokoleti, kadi za upendo kwa ajili ya wapendwa wao.
Happy Valentine's Day 💞
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Address
SUA
Morogoro