Health Insurance

Health Insurance

Share

16/01/2022

CHANZO CHA MAGONJWA YA MOYO

✍🏻Magonjwa ya moyo hutokea pale ambapo moyo huathiriwa na kuharibiwa kwa vitenda kazi vyake. Kuna mitindo ya maisha inayoweza kukuweka hatarini kupata magonjwa ya moyo nayo ni pamoja na;

👉🏿Kuwa na halemu (Cholesterol) na Shinikizo la damu (B.P)
Kuvuta sigala
👉🏿Uzito kupita kiasi na unene uliozidi
👉🏿Kisukari
Kukaa sehemu kwa mda mrefu bila kuufanyisha kazi mwili
👉🏿Umri
👉🏿Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
👉🏿Utumiaji wa vinywaji vinavyobadili hali ya mwili
👉🏿Historia magonjwa yanayoambatana na moyo katika familiaAINA ZA MAGONJWA YA MOYO

✍🏻Zipo aina mbalimbali za magonjwa ya moyo hutofautiana japo yote huathiri moyo, nayo ni;

1️⃣Ugonjwa wa moyo unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu (Coronary artery disease)

Hili ni tatizo linalowakuta watu wengi, mishipa ya damu hupasuka na kuharibika hii hutokana na mishipa ya damu kuwa na uchafu na mafuta mengi na kufanya damu isipite vizuri

2️⃣Mapigo ya moyo kwenda tofauti (Heart Arrhythmias)

Hii hutokea pale mapigo ya moyo kwenda taratibu isivyo kawaida au kwenda haraka isivyo kawaisda, pia mapigo ya moyo kwenda ovyo. Hii ni hatari sana na huua sana

3️⃣Moyo kushindwa kufanya kazi (Heart Failure)

Hii ni hali moyo hushindwa kufanya kazi yake k**a kupampu na kusambaza damu, kusambaza oxygen. Hii inaweza kutokea kwa mtu mwenye magonjwa k**a ugonjwa wa moyo wa misipa kuathirika, Shinikizo la damu, na magonjwa mengine

4️⃣Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa (Congenital heart disease)

Haya ni magonjwa ambayo wengi huzaliwa nayo, yanaweza kuwa ni baadhi ya kasoro katika mwili k**a baadhi ya chemba za moyo kuziba au kupasuka, oxygen kupita kwa shida na vinginevyo.
5️⃣Ugonjwa wa valvu na misuli ya moyo (Heart Valve Disease & Cardiomyopathy (Heart Muscle Disease))

Katika moyo kuna chema nne nazo zinapitisha damu na oxygen kutoka kwenye mapafu, valvu hufunguka na kufunga. Valvu na misuli ikiwa imepasuka na kuharibika husababisha tatizo la moyo.

6️⃣Moyo kutanuka.

Hii hutokea pale damu ikiingia ndani ya moyo harafu mishipa ya kutoa damu ikiwa na tatizo ikashindwa kutoa damu nje ya moyo moyo utaanza kutanuka siku hadi siku. Kutanuka kwa moyo kunatokea usipotibu baadhi ya matatizo k**a shinikizo la damu, moyo kwenda mbio, valvu na misuli ya moyo n.k.

7️⃣Shinikizo la damu (B.P) ni shinikizo la damu yako kwenye kuta za mishipa yako kwani moyo wako unasukuma karibu na mwili wako. Unaweza kuwa na shinikizo la damu (shinikizo la damu) kwa miaka bila dalili yoyote.

8️⃣Mshtuko/ Shambulio la moyo (Heart Attack).

Ni kifo cha sehemu ya misuli ya moyo inayosababishwa na kuzuiwa wa usambazaji wa damu. Amana zilizo na mafuta huunda kwa wakati, na kutengeneza alama katika mishipa ya moyo wakoIkiwa baadhi ya misuli ya moyo inakufa, mtu hupata maumivu ya kifua na kukosekana kwa umeme kwa tishu za misuli ya moyo.

9️⃣Chembe ya Moyo.

Hii ni maumivu ya upande wa moyo maeneo ya kifua hutokea wakati unafanya kazi au hata k**a umekaa k**a ni yenye kukubuhu. Maumivu haya huambatana na kutokwa jasho na kukosa hewa. Hutokana na moyo kukosa damu ya kutosha.

12/12/2021

UJUE UGONJWA WA SARATAN YA SHINGO YA KIZAZI
Saratani ya mlango wa kizazi ni aina ya saratani inayoshambulia seli/chembechembe zilizomo ndani ya ngozi laini inayozunguka shingo ya kizazi.

CHANZO & SABABU ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Wanawake wengi wanaopata ugonjwa huu huwa na kisababishi kimoja au zaidi kinachojulikana ambacho huongeza hatari ya kuupata. Vifuatavyo ni visababishi vikuu:

1.Kuanza vitendo vya ngono katika umri mdogo (chini ya miaka 16)
2.Kuwa na mahusiano ya kimwili na zaidi ya mwanaume mmoja
3.Maambukizo ya virusi vya HPV (Human papilloma virus)
4.Maambukizo ya magonjwa ya zinaa
5.Umri zaidi ya miaka 30
6.Upungufu wa kinga mwilini (VVU/UKIMWI)
7.Uvutaji wa sigara
8.Kupata mimba katika umri mdogo
9.Idadi kubwa ya watoto na kuzaa mara kwa mara
10.Hali duni ya kiuchumi
11.Kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume ambaye mkewe alikufa kwa saratani ya shingo ya kizazi
12.Kuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume ambaye hajatahiriwa
Historia ya saratani ya shingo ya kizazi katika familia

DALILI NA VIASHIRIA VYA KUWA NA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.

Saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote.

1.Kutokwa na damu katika tupu ya mwanamke (va**na) ambayo sio ya kawaida. 2.Damu hii inaweza kuwa matone, au damu inayotoka katikati ya mzunguko wa hedhi (yaani baada ya hedhi kabla ya hedhi inayofuata) au damu itokayo kwa mwanamke ambae ameacha kupata hedhi.
3.Kutokwa na damu baada ya kujamiana baada ya tendo la ndoa.
Maumivu wakati wa kujamiana.

Dalili za saratani iliyosambaa ni k**a zifuatavyo

🕳️Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida yenye harufu na maumivu ya tumbo chini ya kitovu.
🕳️Kupungua kwa hamu ya kula
🕳️Kupungua uzito
🕳️Kuhisi uchovu
🕳️Maumivu ya nyonga
🕳️Maumivu kwenye mgongo
🕳️Maumivu ya mguu
🕳️Mguu mmoja kuvimba
🕳️Kutokwa na damu nyingi kwenye tupu ya mwanamke
🕳️Kuvunjika mifupa (bone fractures)
🕳️Kutokwa na mkojo au kinyesi kwenye tupu ya mbele ya mwanamke.

27/11/2021

MAUMIVU YA NYONGA NI NINI?
Kwa ujumla hakuna njia moja inayoweza kuelezea maumivu haya, ni maumivu yanayotokea sehemu katikati ya tumbo na eneo la hips. Baadhi ya watu maumivu yanaweza kuanzia kwenye eneo la chini ya mgongo na kusambaa hadi kwenye eneo la nyonga.

Kwa upande wa mwanamke maumivu yanaweza kutokana na shida kwenye uzazi sababu mfumo wa uzazi wa mwanamke upo kwenye nyonga. Maumivu haya ya nyonga yanaweza kumpata mwanamke, mwanaume na hata watoto pia.

DALILI YA MAUMIVU YA NYONGA
Maumivu ya nyonga siyo ugonjwa bali ni dalili ya uwepo wa tatizo la kiafya. Maumivu haya yanaweza kuwa ya muda mfupi au ya muda mrefu na hutokea kweye nyonga na chini ya tumbo.

Dalili za maumivu ya nyonga hutofautiana kwa wagonjwa. Wengine hupata maumivu mepesi na wengine hupata maumivu makali. Kwa baadhi ya watu maumivu huweza kuwa makali hadi kupelekea kukwamisha shughuli za kimaisha k**a mazoezi, kutembea na tendo la ndoa. Kwa ujumla maumivu ya nyonga huambatana na matatizo mengine k**a kushindwa kufanya tendo la ndoa
NINI KINASABABISHA MAUMIVU YA NYONGA?
Kuna sababu nyingi zinazopelekea maumivu ya nyonga kwa wanawake na wanaume. Inaweza kuwa ni maambukizi, ama athari kwenye viungo vya ndani k**a kibofu cha mkojo, utumbo mpana, kwa wanawake yaweza kuwa ni shida kwenye uzazi. Hapa chini ni maelezo sababu kuu zinazopelekea maumivu ya nyonga.

🕳️Constipation
Kukosa choo ama kupata choo kigumu kwa muda mrefu husababisha maumivu ya nyonga kutokana na presha na kujaa gesi kwa tumbo. Constipation yaweza kusababishwa na lishe mbaya, msongo wa mawazo, matatizo ya homoni, upungufu wa madini ya magnesium, kupungua kwa bakteria wazuri tumboni na kutoshugulisha mwili.

Kwa kutumia package yetu ya digestive care unaweza kupona tatizo lako la constipation na kuimarisha afya ya tumbo.

🕳️Matatizo ya kibofu cha mkojo
Kibofu kinapopata hitilafu hupelekea kuvimba kwa tishu zake na kusababisha maumivu kwenye eneo la nyonga. Ugonjwa wa kibofu uitwao interstitial cystitis, ambao huletekeza dalili za UTI ni moja ya matatizo yanayosababisha maumivu ya nyonga.

🕳️Matatizo ya figo
Matatizo k**a maambukizi kwenye figo au mawe kwenye figo husababisha maumivu ya nyonga. Tatizo la mawe kwenye figo husababisha maumivu ya chini ya mgongo ambayo husambaa mpaka kwenye eneo la nyonga.

🕳️Hernia au ngiri
Hernia/ngiri hutokana na kutofunga kwa eneo la chini ya tumbo na kupelekea kukua kwa tishu kukua kuelekea eneo la uzazi. Ngiri husababisha maumivu makali ya nyonga.

MAUMIVU YA NYONGA KWA MWANAMKE
Maumivu ya nyonga kwa wanawake yanaweza na shida kwenye uzazi. Matatizo haya yanaweza kutokea kwenye viungo k**a uke, shingo ya kizazi, kuziba mirija ya uzazi, mifuko ya mayai au mfuko wa mimba. Inawezekana pia kupata maumivu kutokana na sababu zaidi ya moja, sababu hizi zinaweza kuwa:

1. Endometriosis
Endometriosis ni kitendo cha kukua kwa ukuta wa ndani(endometrium) wa mfuko wa mimba kuelekea nje ya mfuko wa mimba. Pale tishu zinapokua na kuwa nene husababisha dalili k**a maumivu ya nyonga, maumivu kipindi cha hedhi, tumbo kujaa gesi na maumivu ya chini ya mgongo.

2. Fibroids
Fibroids ni uvimbe usio saratani unaotokea ndani ya kuta za mfuko wa mimba. Tafiti zinasema kwamba karibu asilimia 40 mapaka 80 ya wanawake hupata shida ya fibroids katika uzazi kwenye maisha yao.

3. PID
Pid ni maambukizi kwenye njia ya uzazi ambayo kwa kiasi kikubwa husababishwa na magonjwa ya ngono k**a chlamydia au gonorrhea. Dalili kubwa ni maumivu ya nyonga, maumivu wa wa tendo ndoa, maumivu wakati wa kukojoa, na kutokwa na uchafu ukeni kusiko kawaida.

4. Ovarian cysts
Ovarian cysts ni mkusanyiko kwa vimbe ndogo ndogo zilizojaa maji kwenye mifuko ya mayai ya mwanamke. Kwa wanawake wengi vimbe hizi hazileti shida na huweza kupotea baada ya muda. Lakini kwa baadhi ya wanawake vimbe zinapokuwa kubwa huleta maumivu ya nyonga na kuvurugika kwa hedhi.

5. Kutoa mimba
Dalili kubwa zinazotokea baada ya kutoa mimba ni k**a kutokwa na uchafu ukeni usio kawaida, maumivu ya chini ya tumbo, maumivu ya nyonga, kuharisha na wakati mwingine kuzirahi kutokana na kutokwa na damu nyingi.

6. Maumivu kipindi cha hedhi
Baadhi ya wanawake hupata maumivu ya nyonga wakati wa hedhi, maumivu haya huitwa dysmenorrhea kwa kitaalamu. Maumivu kipindi cha hedhi ni kutokana na kutanuka kwa misuli ya mfuko wa mimba.

MAUMIVU YA NYONGA KWA MWANAUME
Ukiacha wanawake, wanaume pia hupata tatizo hili la maumivu ya nyonga, hasa wenye tatizo la tezi dume. Kuvimba kwa tezi dume ama maambukizi kwenye tezi dume husababisha maumivu ya nyonga, eneo la haja kubwa, kwenye tumbo la chini na pia maumivu kwenye kibofu.

Dalili zingine zinazoonesha kuna shida kwenye tezi dume ni kupata maumivu wakati wa kukojoa ama kupata mkojo kidogo sana . Unapoona dalili hizi wahi hospitali mapema ili kupata vipimo na tiba haraka.

Want your business to be the top-listed Finance Company in Morogoro?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Website

Address


Kihonda
Morogoro