RhapsodyMan

RhapsodyMan

Share

16/02/2023

_*Jipatie BURE Nakala yako ya mwezi FEBRUARI kwa LUGHA YA KISWAHILI na nyingine nyingi ikusaidie kukua kiroho:*_ http://rhapsodyofrealities.tniglobal.org

*KUACHILIA MISIMBO SAHIHI*

Alhamis, 16

Mchungaji Chris Oyakhilome, PhD

_*Maana yeye anenaye kwa lugha, hasemi na watu, bali husema na Mungu; maana hakuna asikiaye (anayemwelewa); lakini anena mambo ya siri katika roho yake*_ 1 Wakorintho 14:2

Kuna vitu ambavyo havitatendeka kwa ajili yako maishani mwako na katika dunia hii mpaka utakapojifunza kutumia maneno ya misimbo. Paulo aliita hekima, mafumbo na siri za kiroho (1 Wakorintho 2:7).

Kwa mfano, unavyoanza kuomba katika roho, utafika mahali ambapo unapoanza kuviita vitu kutoka ulimwengu wa roho vije kwenye ulimwengu wa kawaida. Maisha ni ya kiroho na tunashinda kwa Roho.

Kupitia Roho Mtakatifu, unaweza kujua maneno sahihi ya kutumia katika sala. Maneno hayo ni misimbo ya kiroho. Anaweza atake urudie neno au kutoa sauti kwa kurudiarudia; hilo ni kwa sababu Anajua maelezo ya “msimbo.”

Roho Mtakatifu anajua mara unazoweza kuwa unahitaji kurudia maneno hayo ili yaunde msimbo sahihi. Katika sala, unaweza kuwa unazungumza maneno fulani au kutoa sauti fulani ambazo zinaweza kuhitaji ishirini na tano kati ya sauti hizo ili msimbo uwe kamili au umeunganika. Lakini ukiishia kwenye sauti ya ishirini na nne, haitafanya kazi, kwa sababu msimbo hautakuwa umekamilika.

Ni k**a kujaribu kuingia kwenye mfumo wa maneno ya siri au akaunti; huwezi kuingia kwa misimbo isiyo sahihi hata k**a ni herufi au alama moja iliyokosewa. Hivyo katika kuomba na kuviita vitu katika Roho, endelea hadi Roho aende kiwango kingine. Kumbuka, Yeye ndiye Anayekupa usemi.

Kuna mambo ambayo watu huyapitia maishani na hata k**a wamekuwa wakinena kwa lugha, kumeonekana kutokuwa na matokeo. Ni kwa sababu kuna msimbo kwenye ulimwengu wa roho ambao bado unakosekana. Tumia misimbo na utakuwa na mtoto uliyetamani kwa muda mrefu. Tumia misimbo na fedha zitakuja; utakuwa na ukumbi kwa ajili ya kanisa au biashara.

Nyumba unayoitamani iko ndani ya lugha hiyo ya msimbo; tumia misimbo sahihi na utakuwa nayo. Jibu la tatizo hilo liko kwenye “msimbo” lakini Roho Mtakatifu anaujua msimbo. Nena kwa lugha hadi upate misimbo kamili kutoka kwa Roho Mtakatifu na uiachilie.

*| SALA*

*Mpendwa Baba, ninaponena kwa lugha leo, mwangaza hunijia rohoni mwangu. Ninajua hatua za kuchukua kuhusiana na hali mahususi kuhusu maisha yangu; ninajua cha kufanya, wakati wa kukifanya, na jinsi ya kukifanya, kwa sifa na utukufu wa Jina Lako. Amina.*

*Jifunze Zaidi:*

** 1 Wakorintho 14:2 AMPC; 1 Wakorintho 2:11-13 **

*SOMA MAANDIKO KILA SIKU*

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MWAKA-1:*_

Marko 2:1-22 & Walawi 9-10

_*MPANGO WA KUSOMA BIBLIA MIAKA-2:*_

Mathayo 14:34-15:1-9 & Mwanzo 47

*Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional*

*Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye* _*www.rhapsodyofrealities.org*_

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Chunya District
Mbeya