Amos Msuli
JUHUDI za serikali za katazo la uuzaji wa pombe za viroba nchini huenda likakwama kutokana na baadhi ya wamiliki wa baa na grocer wilayani Rungwe mkoani Mbeya kuendelea kuuza pombe hizo kwa kificho huku wakivibatiza jina la ‘Dawa au Samaki mchanga.
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania,imepiga marufuku uuzaji na usambazaji wa pombe hizo,kwenye karatasi za naironi ikihitaji pombe hizo ziuzwe kwenye chupa,hali ambayo imeleta Taharuki kwa wafanyabiashara huku wengine wakijipiga risasi hadi kufa.
Siku ya tarehe 1/3/2017 gazeti hili lilishuhudia fuso moja likiwa na shehena za viroba likitua wilayani humo,lengo likiwa ni kuviuza maeneo ya grocer zilizopo vijijini na kwenye maeneo ya mipakani.
Baada ya katazo hilo,gazeti hili lilifanya uchunguzi kwa siku kadhaa katika wilaya mbili ambapo kwa wilaya ya Kyela wamekuwa wakiuza kwa kificho na kubatiza jina la ‘’Chapati’’kwa viroba vya Malawi na vya Tanzania wakiviita ‘’Kichwa’’ambavyo wamekuwa wakiuza kwa kificho kwa wateja wanao wafahamu.
Kwa Upande wa wilaya ya Rungwe gazeti hili lilipita katika baa nne na groser sita na kushuhudia pombe hizo zikiuzwa kwa majina ya ‘’Ng’ombe’’ kwa viroba vya Malawi na’’Dawa’’ au ‘Dagaa mchanga’’kwa viroba vya Tanzania.
Akizungumzia hali hiyo,mwenyekiti wa wamiliki wa nyumba za kulala wageni yaani hotel.gest na baa wilayani Rungwe,Christopher Mwakanyamale,alisema huenda uuzaji huo unafanyika kweli kutokana na serikali kutoa muda mfupi na kuwa ipo haja ya kuongeza siku 30 mbela ili waviondoe.
Alisema zoezi ni zuri lakini serikali ilitoa muda mfupi huku ikijua wajasilia mali wengi wakiwemo wanawake wamekopa fedha kwenye taasisi mbalimbali ambazo wanarejesha kila baada ya siku saba na biashara waliyokuwa wakiitegeme ni viroba na ndiyo maana wanauza kwa kificho.
‘’Ndugu mwandishi,wafanyabiashara wengi walinunua mzigo mkubwa wa viroba na kulipia mapato yote ya serikali ikiwemo,TRA na bidhaa yenyewe inanembo ya TBS,ilitakiwa serikali isitishe kwenye viwanda na kutoa muda kwa walionavyo ili waviuze na kuanza kununua vya kwenye chupa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara wilayani humo,Lumage Mwivaha,alisema kitendo cha serikali kuviondoa viroba hivyo ni jambo la kupongezwa licha ya kuwa walitoa muda mfupi uliopelekea hasara kubwa kwa wafanyabiashara.
Alisema vijana wengi kutokana na bei kuwa ndogo ya viroba walikuwa wakinywa hovyo huku afya zao zikidhorota na kuwa kitendo cha kubadirisha jina la viroba hivyo halina tija na kuwa suala la kupambana na wauzaji hao wanaiachia serikali
Click here to claim your Sponsored Listing.
Telephone
Website
Address
Mbeya
95