MUST FM Radio - Mbeya

MUST FM Radio - Mbeya

Share

01/06/2023

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewataka Wakuu wa Shule pamoja na Wakurugenzi kuzingatia utaratibu uliotolewa na Kamishna wa Elimu kuhusu muongozo wa kufunga na kufungua shule ili kuwapatia nafasi wanafunzi kupumzika katika kipindi cha likizo.

"na mbaya zaidi kuna baadhi ya malalamiko tumeanza kupokea kwamba kuna shule zinazuia wanafunzi kwenda likizo bila hata kushauriana na wazazi na wengine wazazi wanatakiwa walipe kuwaweka wanafunzi mashuleni" alisema Prof. Mkenda.

23/03/2023

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kinapenda kukukumbusha uwepo wa Dawati la Malalamiko linalolenga kuboresha ubora wa huduma zake kwa kamili.
Hivyo katika kuhakikisha inafikia malengo ya kushughulikia malalamiko Afisa anayehusika na Dawati hili pia anakualika kufika ofisi nambari 18 Administrative Basement ili kutoa maoni yako.
"Kwa pamoja tunaweza kuimairisha ubora wa huduma zinazotolewa na Taasisi yetu"
104.5 MUST FM

01/08/2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Phillip Mpango amevitaka Vyombo vya Habari kuelimisha na kuhamasisha jamii masuala yanayohusu kilimo na ufugaji kwa ajili ya kuchochea maendeleo na uchumi nchini.

Dkt. Mpango ametoa wito huo leo wakati akitembelea mabanda katika ufunguzi wa Maonyesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini viwanja vya John Mwakangale, ambapo amesema lazima kuwepo na vipindi vya elimu kwa ajili ya wakulima pamoja na ufugaji wa aina zote ili kuwawezesha wananchi kufahamu kuhusu faida za sekta hizo.

Want your business to be the top-listed Media Company in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Box 131
Mbeya