Isaiah The JUDGE
21/04/2026
Miaka 40 ya kutembea jangwani, wana wa Israeli waliishi kwa kula manna, waliishi kwa miujiza !
Lakini mara tu walipoikanyaga Nchi ya kanaani, ile mana ilikoma, kutokea hapo waliendelea kuishi kwa kanuni
Yoshua 5:12 Ndipo ile mana ikakoma siku ya pili yake, baada ya wao kuyala hayo mazao ya nchi; na hao wana wa Israeli hawakuwa na mana tena; lakini wakala katika viliwa vya nchi ya Kanaani mwaka huo.
Walipoanza kuyala mazao ya nchi, basi muujiza unaitwa mana ulikoma; Kutokea hapo iliwapasa, walime, wafuge, watunze mizabibu n.k ili waendelee kufurahia uheri wa nchi ile
NATAKA UELEWE NINI HAPA
Mtumishi wa Mungu anaweza kukuombea kwa Ufunuo ; Akachukua maji akayaombea akakupa ukanywa na ukapona SASA HII HAINA MAANA KWAMBA, BAADA YA KUPONA UANZE KUISHI KWA KUNYWA YALE MAJI.
AU UANZE KUYACHUKUA MAJI NA KUYAPELEKA YAGUSE MADHABAHU HALAFU UANZE KUTEMBEA NAYO; HUU SIO UFUNUO NI UTOTO.
Ukipona kwa ufunuo, ulipaswa sasa kuanza kuishi kwa Neno la Mungu, kwa kanuni za ufalme
Wewe unafikiri
Hilo tumbo litakombolewa mara ngapi
Hiyo miguu itafunguliwa mara ngapi
Hiko kichwa kitaombewa mara ngapi
Kumbuka kwamba
FEDHA haiwezi kununua mchakato wa ukuaji wa kiroho ; Fedha haiwezi kuwa mbadala wa kanuni
NA NINYI WAKRISTO
Muache uvivu, hili suala la ukombozi linakua sana siku hizi; mpaka inakupa shida, kujua hawa ni wakristo kweli
Yaani kila siku ni ukombozi na kukombelewa; Kila siku wanavuka
UKIFIKA KANAANI ANZA KUFANYIA KAZI KANUNI, ACHA KUANGALIA JUU
UKIFIKA NDANI YA KRISTO ANZA KUFANYIA KAZI KANUNI ZA NENO LA KRISTO KWA UJUMLA.
Ni muhimu sana
Pastor Ibrahimu Amasi
12/12/2025
KUHUSU USEJA (SINGLEHOOD).
Useja ni hali ya mtu kutokuwa katika agano la ndoa.
Kwenye kizazi cha sasa ni k**a tatizo kuwa mseja, jambo ambalo si sahihi.
Na hii ni kwa sababu watu wameaminishwa kuwa bila kuoa au kuolewa ni tatizo, ni kupungukiwa au kutokuwa na thamani nk. Huo wote ni mtazamo wa jamii na wanadamu, lakini si mtazamo wa Mungu!!
Hivyo si kweli kabisa, kwamba Useja ni tatizo maana hata kwa asili Mwanadamu wa Kwanza kabisa alikuwa mseja (asiye na ndoa).
Maana yake chaguo la kwanza la Mungu lilikuwa useja. Hii ni kusema kwamba ndoa ilikuja kuboresha kazi ya adamu na si maisha yake, (maana yake unaweza kuwa na maisha Bora hata ukiwa single) ndiyo maana mpaka leo ndoa haiwezi kuwa mkakati wa kuboresha maisha ya mtu Bali (ni chombo cha kubebea kusudi la Mungu).
Hivyo ni hakikisho kuwa unaweza kuwa bora bado ukiwa mseja bila kutarajia ndoa ndiyo iwe suluhu ya matatizo yako.
Ndiyo maana hata Yesu mwenyewe alikuwa mseja, na hakupungukiwa kitu vivyo hivyo Paulo naye. Hivyo si sawa kujiona mnyonge kwa vile hujaolewa / hujaoa, maana bado hujapungukiwa kitu Usiogope!
Na kwanza, tangiapo utoshelevu wetu hautegemei vitu au watu bali humtegemea Yesu k**a chanzo cha utoshelevu. Hivyo naweza kuishi maisha ya furaha na amani bado nikiwa singo!
Usiruhusu hisia za upweke zikudanganye, na udhani kuwa ndoa pekee ndiyo suluhisho, jambo ambalo wakati fulani ndio hupelekea ndoa zenye matatizo kuzaliwa—Hii ni kwa sababu Upweke si sababu ya kuwa na ndoa. Mimi naamini mtu mwenye sifa za kuingia kwenye ndoa ni yule aliyeshinda upweke kwa kuwa na ukaribu na Mungu, ili aishi kwa furaha.
Ndoa ni chombo cha kubebea kusudi la Mungu, na SI mkakati wa kukwamua maisha binafsi ya MTU, Bali maisha ya watu wengi zaidi!
You're loved & blessed
[Pastor Isaiah Imani]
12/12/2025
MAMBO 5 YA KUJIFUNZA KWA MWANAMKE REBEKA (Mwanzo 24:1-67)
01. REBEKA ALIKUWA WA KIROHO kiasi kwamba wakati akiwa mjamzito, tumbo lake lilipomtatiza alikuwa na uwezo wa kukaa na Mungu kibinafsi na akamsikia.
Mwanzo 25:22
"Watoto wakashindana tumboni mwake. Naye akasema, Ikiwa ni hivi, kuishi kwanifaa nini? Akaenda kumwuliza BWANA."
[And the children struggled together within her; and she said, If it be so, why am I thus? And she went to enquire of the LORD.]
Na kabla ya hapo Alikuwa na uwezo wa kuyatambua MAJIRA ya kiroho ya kujiliwa kwake, jambo lililomwezesha kujua wakati sahihi wa kwenda kisimani Ili akutane na MTU sahihi kwa hatima yake.
Hii inatufundisha kuwa bila ukiroho unaweza kupishana na wasaidizi wako wa HATIMA Kila siku. Ndiyo maana unaweza kuwa unachelewa kuolewa kumbe unapishana na uongozi' wa Mungu wa majira.
Mwanzo 24:15
___"Ikawa, kabla hajaisha kunena, tazama, Rebeka anatokea, binti wa Bethueli mwana wa Milka, mkewe Nahori, ndugu wa Ibrahimu, naye ana mtungi begani pake."
Wanawake wengi Leo hii hawawezi kusikia sauti ya Mungu na hiyo ni zao la kutokuwa wa kiroho. Ndiyo maana ni wepesi kudanganywa na Mitume au manabii matapeli wa kizazi hiki. Kwa sababu Kila kitu anataka kuuliza watu maana Hana madhabahu binafsi inayoongea.
Ni muhimu mno mwanamke uwe na madhabahu hai inayoongea na wewe kibinafsi, mahali pa Siri unapoweza kukutana na Mungu na ukauliza habari za maisha Yako.
Binafsi naamini Rebeka alikuwa na uwekezaji mkubwa sana katika maarifa ya Mungu wa kweli kiasi kwamba aliweza kusikia na kujitambua sauti ya Mungu.
Maana Usikivu wa kiroho hufungulia kupitia Maarifa ya kiroho (Neno la Kristo).
Kwako mwanamke wa KIZAZI hiki, unalojukumu kubwa la kumjua Mungu kibinafsi Kwa kukaa mahali pa Siri na kujenga madhabahu Yako Kwa Mungu kwaajili ya watoto wako, mume wako, na hata jamii Yako.
Danieli 11:32 ___"lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu."
Lazima UWE na mahali unapoweza kuwasiliana na Mungu Kwa njia ya kuomba, kufunga, kuishi utakatifu, na kujifunza Neno la Mungu.
02. REBEKA ALIKUWA NA IMANI kiasi kuweza kumwona Mume ndani ya mtumwa.
Mwanzo 24:57-58
____"Wakasema, Na tumwite huyo msichana, tumwulize mwenyewe. Wakamwita Rebeka wakamwuliza, Je! Utakwenda na mtu huyu? Akasema, Nitakwenda."
Sivyo ilivyo Kwa mabinti wengi wa nyakati zetu, ambao huamini kuwa mtu wa kuwaoa ni mwenye Kila kitu, bosi wa makampuni, au MTU mmoja MKUU, Kwa Sababu hawana jicho la Imani la kumwona mwanaume mwenye kipato kidogo, anayejitafuta bado k**a MTU anayeweza kuwa MKUU baadaye.
Lazima k**a Mwanamke ufahamu kuwa, ULIUMBWA KWAAJILI YA MFALME, LAKINI WEWE NDIYE UNAYEJITENGENEZEA MFALME WAKO.
Kila mwanaume aliyekamilika hakuhitaji wewe uwe mkewe! Uko Ili kumuongezea mumeo ubora. Na hivyo ndivyo wanaume waoaji wa kweli huja wakiwa k**a watumwa ambao usipokuwa na Imani huwezi kuona ukuu ambao Mungu amewawekea mbele Yao.
Na mara nyingi hii huja Kwa Sababu mabinti wengi hawajijui wenyewe Wala hawafahamu kile walichobeba kinavyoweza kugeuza maisha Yao na ya watu wao wa karibu.
Ni kwamba hawafahamu pia mchango wao KATIKA kuboresha maisha ya waume zao. Ndiyo maana k**a unasoma hapa ukiwa Binti au mwanamke yeyote lazima ufahamu kuwa unamchango mkubwa sana katika kukwama au kuhakikisha mume wako anafanikiwa Kwa kiwango kikubwa.
Mtu yeyote mwenye maono, na ushirika mzuri na Mungu ni mtu mwenye hatima ya utukufu hata k**a ni mtumwa Sasa, ni wazi kuwa ni mkuu mno baadaye.
Ukiamua kuwa mtu sahihi Kwa mume wako, basi utarahisisha maisha na mafanikio yake duniani.
Kumbuka wewe ni kibali cha mumeo mbele za Mungu, watu, na mafanikio Yako yote!
Mithali 18:22
____"Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa BWANA."
03. REBEKA ALIKUWA MREMBO MWENYE BIDII.
Unapomsoma humwoni k**a mtu anayesukumwa au kulazimishwa kufanya kazi na kuwajibika.
Mwanzo 24:19-20
_____"Hata alipokwisha kumnywesha akasema, Na ngamia zako nitawatekea, hata watakapokwisha kunywa. Akafanya haraka, akamwaga maji ya mtungi wake katika birika, akapiga mbio kisimani ateke, akawatekea ngamia zake wote."
Huoni mwanamke anayesubiri ndoa imuokoe kutoka kwenye maisha magumu Bali ni MTU anayeshughulika na kujituma Kwa bidii mno.
Hebu fikiria ameombwa maji ya kunywa na mgeni anampatia Kwa ukarimu mkubwa, na zaidi ya hayo Kwa moyo mkunjufu kabisa anaamua kuwanywesha na ngamia ambao kiuhalisia hunywa maji mengi mno. Bila shaka unaweza kuona bidii ndani yake. Ni mtu mwenye jicho la kuona mapungufu na kuyashughulikia.
Hii ni tofauti na WANAWAKE wengi Leo ambao wanaweza kukaa Mazingira yasiyosawa bila kutambua UHITAJI, na wengine wanaweza kuona changamoto badala ya kurekebisha wanalalamikia au kunung'unika badala ya kutatua. Haifai kabisa Kwa mwanamke kuokaa kwenye Mazingira ovyo ya nyumbani, kanisani, au popote! Ni lazima uwe na uwezo wa kuona mapungufu na kuyarekebisha.
Mithali 31:15-16
____"Tena huamka, kabla haujaisha usiku;
Huwapa watu wa nyumbani mwake chakula; Na wajakazi wake sehemu zao. Huangalia shamba, akalinunua; Kwa mapato ya mikono yake hupanda mizabibu."
Lazima ufahamu k**a mwanamke, Sifa na heshima Yako kubwa Iko kwenye mambo ya ziada unayofanya na SI kwenye mambo ya kawaida.
Je Uko tayari kufanya jambo Kwa ubora wa ziada? Hii ndiyo hufanya watu waseme umewazidi wote. Na huwezi kuwazidi wote k**a huna moyo mkunjufu na wa utayari katika kufanya mambo.
Mithali 31:28-29 "Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote."
Unaweza kuona pia Rebeka ni mtu aliyefanya bila kulalamika, Bali Kwa furaha maana k**a isingekuwa hivyo basi asingejipa jukumu la kuwanywesha ngamia wa yule mgeni ambao bila shaka alipowaona alifahamu wamesafiri safari ndefu na wamechoka. Huwezi Fanya hivi k**a wewe ni mvivu au mzembe!
2 Wakorintho 9:7
____"Kila mtu na atende k**a alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu."
Zaidi ya hayo nimeona kwenye maandiko, wanawake wote walioolewa walikuwa kwenye uwajibikaji fulani (utaona wazi hata hawa mwenyewe alikutwa bustanini). Lakini makahaba wengi wamekutwa barabarani, kwenye Kona za njia nk.
Maana yake Kila mwanamke anapaswa kuwa na tabia ya kuwajibika na kupenda kujishughulisha Kwa uaminifu kwenye Kila anachofanya.
Kila mwanamke unapaswa kuwa na bidii itakayofaya uitwe heri na uliyewazidi wote! Kwenye Kila unachofanya hakikisha unaongeza ubora wa ziada utakaokutofautisha na wengine, hii ni sifa njema na itakupa kuinuka.
04. REBEKA ALIKUWA MTII NA MNYENYEKEVU.
Hii utaiona jinsi alivyotenda Kwa akili pindi alipompokea yule mgeni aliyetumwa na Ibrahimu.
Mwanzo 24:28-30
____"Basi yule msichana akapiga mbio, akawaambia watu wa nyumba ya mama yake mambo hayo. Na Rebeka alikuwa na kaka, jina lake Labani. Labani akatoka mbio kumwendea yule mtu kisimani. Ikawa, alipoiona ile pete, na vikuku mikononi mwa nduguye, akasikia maneno ya Rebeka nduguye, akisema, Hivyo ndivyo alivyoniambia mtu huyo, basi akamjia mtu yule, na tazama, amesimama karibu na ngamia kisimani."
Alipovikwa vikuku hakuvificha Bali alikuwa muwazi Kwa wazazi na walezi wake bila kuogopa Ili apate Mashauri na hekima za kumsaidia kuwa Bora. Hii ni tofauti na WANAWAKE wengi Leo ambao Hupenda kufanya vitu kisirisiri bila kushirikisha mamlaka zao zinazowalea. Hapo ndo Kuna wanawake wasiokuwa wa wazi, na hawataki kushauriwa na MTU yeyote kwenye mambo Yao.
Hapo utaona mabinti wengi walianza mahusiano kimyakimya, unakuja kusikia wanatoa taarifa baada ya kuumizwa au kufanyiwa mambo ya hovyo. Hii ni ishara ya kiburi na Hali ya kukosa unyenyekevu!
Ukiwa k**a mwanamke jifunze kunyenyekea chini ya mamlaka na kufanya vitu Kwa uwazi mbele ya walezi wako hasa wale wa kiroho wenye uwezo wa kukupa mwelekeo sahihi na mzuri unaoendana na Neno la Mungu. Kufanya hivyo ni kuonesha unawaheshimu na unawatambua k**a watu muhimu kwenye maisha Yako na unawapokea k**a mamlaka ya Mungu kwako.
05. REBEKA ALIKUWA MKARIMU NA MWENYE MOYO MZURI.
Unaweza kuona NAMNA alivyomtendea mema mgeni asiyemfahamu na kumkaribisha nyumbani kwao. Na kabla ya hapo namna alivyojitambulisha iliyoonesha anavyojitambua na kujithamini pia.
Mwanzo 24:24-25
____"Akasema, Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, aliyemzalia Nahori. Tena akamwambia, Kwetu kuna majani na malisho ya kutosha, na mahali pa kukaa wageni."
Wanawake wengi Leo SI wa karimu hata Kwa ndugu za waume zao, au watu mbalimbali wa karibu Yao na zaidi sana si wa karimu Kwa wageni.
Mwanamke MKARIMU ndiye mwenye uwezo wa kufanya jengo liwe nyumba. Usipokuwa MKARIMU k**a mwanamke, umetia DOA maisha Yako na ya watu waliokuzunguka.
Haipendezi mwanamkechoyo, haipendezi mwanamke mwenye Roho mbaya, haipendezi kabisa!
SHALOM
[Pastor Isaiah Imani]
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Mbalizi
Mbeya