Mbeya Fm Redio

Mbeya Fm Redio

Share

28/05/2026

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, amemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camilius Wambura, kuangalia namna jeshi hilo litakavyojenga imani yake kwa wananchi, sekta binafsi na jumuiya za kimataifa zilizopo hapa nchini.

Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo, akirejea utafiti uliochapishwa na Shirika la Afrobarometer hivi karibuni, ukihusisha wananchi wa Afrika na imani kwa Jeshi la Polisi.

Kupitia utafiti huo, wananchi hao walihojiwa endapo watapata shida ya kisheria, imani yao ikoje kwa Jeshi la Polisi na ripoti imeonyesha asilimia 12 pekee ya Watanzania waliohojiwa walisema watakimbilia polisi.

Katika nchi 38 za Afrika zilizohusishwa kwenye utafiti huo, moja pekee ndiyo ilikuwa na alama za juu yaani asilimia 25, kwamba raia wakipata shida watakimbilia polisi.

Rais Samia ametoa maelekezo hayo kwa IGP Wambura, leo Mei 28, 2026 wakati akihitimisha Mafunzo ya Maofisa na Wakaguzi Wasaidizi wa Polisi, Kurasini, Dar es Salaam leo Mei 28, 2026.

Amesema taarifa hizo si za kuzibeza, bali ni kuangalia changamoto zilipo hadi wananchi wajibu hivyo na zifanyiwe kazi.

“Tunataka kuona namna Jeshi la Polisi linavyojenga imani yake kwa wananchi na sekta binafsi na jumuiya za kimataifa zilizopo nchini. Hapa tunaangalia legitimacy (uhalali) ya polisi,” amesema.

📻Tufuatilie Mbeya Fm kupitia 89.3 Mhz au online kwenye Radio Box kwa jina la Mbeya FM Radio. Like, comment na share ili kupata updates za kila siku!

📌 Mbeya Fm – Radio yako, Radio yangu, Radio yetu.

Want your business to be the top-listed Media Company in Mbeya?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Mbeya