Revelation Of Jesus Christ
13/03/2024
Somo la leo
Hakikisha unapotenda wema iwe siri yako wewe na Mungu wako
Soma Mathayo 6:1-4
Wengi leo wanapofanya wema au kusaidia mtu wanapenda watu ndiyo waone ili wao wapate sifa kwa watu lakini hayo yote siyo agizo la Mungu kulingana na maandiko.
Utaona leo watu wanaenda kuona yatima na wajane cha kwanza wanachokumbuka ni kupiga picha na kupost ili watu wajue kuwa wao wanasaidia watu, lakini neno linasema wafanyao hayo wamekwisha kupata thawabu yao kwa kwa hao wanaowasifia.
Ebu fikiri k**a mtu aje akupe msaada alafu akupige picha apost utajiskiaje au mtu anapompa msaada ndugu yako ampige picha amuweke mtandaoni sidhani k**a inapendeza hasa kwa wale wanaotamani kupokea thawabu kwa Mungu wao yaani wana wa Mungu
Mathayo 6
1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya k**a hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, k**a wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Watu wa Mungu tujitahidi kuishi na kuenenda sawa na neno hapo ndipo tutampendeze kuona mkono wa Mungu ukiwa pamoja nasi.
Pastor Isack Mwampondele
Rjc (Revelation Of Jesus Christ)
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Culinary Team
Attire
Contact the place of worship
Website
Address
Mbeya
53000