Mashujaa FM
VIDEO: Miradi 159 ya maendeleo yenye thamani ya zaidi ya Sh bilioni 300 iliyotekelezwa mkoani Lindi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2024/2025 hadi 2025/2026 imekaguliwa na TAKUKURU, huku miradi 22 ikibainika kuwa na kasoro kubwa zilizosababisha kuanzishwa kwa uchunguzi, na mingine 137 ikikutwa na mapungufu yaliyoelekezwa kurekebishwa au kutekelezwa upya.
Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoani humo, Stephen Mafipa, wakati akizungumza kuhusu majukumu ya kisheria ya taasisi hiyo katika warsha ya wadau wa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Follow Us
Instagram
Facebook
Twitter
YouTube
HABARI: Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Dkt.Victorina Ludovick, ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi na kuwaona wagonjwa mbalimbali wakiwemo wagonjwa wa macho zaidi ya 180 waliokuwa wakipatiwa huduma za matibabu kutoka kwa madaktari bingwa wa macho.
Dkt. Victorina amesisitiza kuendelea kuwafuatilia wagonjwa hao kwa karibu na ndani ya wiki mbili waweze kurejea hospitalini kwa uchunguzi zaidi na tathmini ya maendeleo ya matibabu yao
Kwa upande wa wananchi waliojitokeza kupata huduma hiyo wameshukuru kwa kuwasogezea huduma za kibingwa karibu, kwani imewapunguzia gharama za kwenda mbali zaidi kufuata huduma hiyo.
Follow Us
Instagram
Facebook
Twitter
YouTube
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Wailes
Lindi