Manispaa ya Lindi

Manispaa ya Lindi

Share

Photos from Manispaa ya Lindi's post 15/07/2026

MILIONI 510.8 ZATOLEWA KUFIDIA WANANCHI WALIOPISHA MAENEO YA VYANZO VYA MAJI MANISPAA YA LINDI

Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Victoria Mwanziva, leo tarehe 15 Julai 2026 ameongoza uzinduzi wa zoezi la ulipaji fidia kwa wananchi wa Kata za Mnazi Mmoja, Rasbura na Mbanja waliopisha maeneo ya vyanzo vya maji.

Jumla ya Shilingi milioni mia tano na kumi na laki nane (510,800,000/=) zimetolewa k**a fidia ya ardhi, mazao na nyumba kwa wanufaika arobaini na tisa (49), hatua inayolenga kuhakikisha uhifadhi na ulinzi wa maeneo muhimu ya vyanzo vya maji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Mwanziva amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwezesha upatikanaji wa fedha hizo ambazo zimewezesha wananchi kupata fidia stahiki.

Amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kutumia fedha hizo kwa malengo yenye tija, ikiwemo kuimarisha maisha yao na kujenga maendeleo endelevu kwa familia zao.

Zoezi hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Mhe. Twahili Mpuluji, Katibu Tawala Wilaya ya Lindi, Ndg. Hudhaifa Rashid, viongozi wa dini na viongozi wa kisiasa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Ndg. Juma Mnwele, amewataka wanufaika kutumia fedha hizo kwa busara na kuzielekeza kwenye shughuli zenye manufaa badala ya matumizi yasiyo na tija.

Naye Mkurugenzi wa LUWASA, Ndg. Mhandisi Tamim Katakweba, amewashauri wananchi kutumia fidia hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili iwe chachu ya maendeleo na ustawi wa maisha yao.

Victoria Mwanziva
Juma Mnwele
Luwasa Maji

Habari BEBO 🦋

13/07/2026

Tupate NENO LA LEO JUMATATU 13/7/2026 kutoka kwa Ndugu Juma Mnwele Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Manispaa.

Juma Mnwele

Photos from Manispaa ya Lindi's post 10/07/2026

MEYA MPULUJI, MKURUGENZI MNWELE WASHUHUDIA MAKABIDHIANO YA ENEO LA UJENZI WA KAMPASI YA NIT MANISPAA YA LINDI

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Mhe. Twahili Mpuluji, na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Ndg. Juma Mnwele, leo Julai 10, 2026, wameshuhudia makabidhiano rasmi ya eneo la ujenzi wa Kampasi ya Usafiri wa Majini ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) iliyopo Kikwetu, ambapo kampuni ya TIL Construction imekabidhiwa rasmi eneo hilo kuanza utekelezaji wa mradi.

Mhe. Twahili Mpuluji amesema utekelezaji wa mradi huo ni fursa muhimu kwa Manispaa ya Lindi kutokana na mchango wake katika kuongeza ajira, kukuza biashara na kuvutia uwekezaji, huku akiielezea kampasi hiyo kuwa kichocheo cha maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wananchi wa Lindi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Ndg. Juma Mnwele, ameahidi ushirikiano wa karibu kati ya Halmashauri na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa ufanisi na kukamilika kwa wakati.

Sambamba na hilo Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Prosper Mgaya, amesema ujenzi wa kampasi hiyo ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha uchumi wa buluu kwa kuzalisha wataalamu wenye ujuzi katika sekta za usafiri wa majini, mafuta na gesi, hatua itakayochochea maendeleo ya kiuchumi nchini.

Kampasi hiyo itajengwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 125 na itakuwa na miundombinu ya kisasa ikiwemo madarasa, warsha, ofisi za wafanyakazi na mkahawa. Mradi huo unatarajiwa kuiweka Manispaa ya Lindi katika nafasi ya kimkakati ya kuzalisha wataalamu wa sekta ya usafiri wa majini na kuwa kitovu cha uchumi wa buluu nchini.

Juma Mnwele

Want your organization to be the top-listed Government Service in Lindi?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


Lindi
255

Opening Hours

Monday 07:30 - 15:30
Tuesday 07:30 - 15:30
Wednesday 07:30 - 15:30
Thursday 07:30 - 15:30
Friday 07:30 - 15:30