Mlewa Electronics

Mlewa Electronics

Share

25/11/2022

HII NDO QATAR NA UCHUMI WAKE:

WANASEMA ni nchi ya mfalme na mwanawe. Hawapotezi muda kwenye malumbano ya siasa!

QATAR ilipata uhuru mwaka 1971 kutoka kwa mwingereza. Ni nchi inayoongozwa na mfalme. Kumbe mambo yasipoenda hata mfalme hutumbuliwa. Alianza Ahmad Al Thani baada ya uhuru. Mwaka 1972 alipinduliwa na mjomba wake Khalifa Al Thani. Huyu alipinduliwa na mwanawe prince Hamad Al Thani mnamo mwaka 1995. Prince Hamad aliachia madaraka kwa Tamim Hamad Al Thani mnamo mwaka 2013. Ukoo huo wa Al Thani hauruhusu ukoo mwingine kuchukua madaraka na hakuna chama cha siasa hata kimoja. Baraza la mawaziri huchaguliwa na kutumbuliwa wakati wowote mfalme akiamua.

UCHUMI wa Qatar unategemea mafuta. Kampuni ya serikali ya Qatar Petroleum (QP) inasimamia utafiti, uchimbaji, usafishaji, usafirishaji na kuhifadhi mafuta. Mwenyekiti wa kampuni hiyo pia ni waziri wa nishati na viwanda. Mafuta na gesi vinatoa asilimia 60 ya kipato cha Qatar.

MAISHA ya waqatari yanategemea kipato cha mafuta ya Qatar. Serikali inaweza kuwapa waqatari huduma za maji, afya, mpaka nyumba bila ya malipo. Elimu ni bure. Wanafunzi wanapata chakula shuleni. Wanasafiri bure, hata nguo wanapewa bila ya malipo. Vilevile serikali inalipia wanafunzi wasomao nje ya nchi. Kuna habari kutoka kwa wenyeji kuwa mqatari hata akiwa hana kazi analipwa mshahara kila mwezi.

ZOEZI hilo linawawezesha waqatari kuachia wageni kazi nyingi huku wenyewe wakiwa wanashikilia nyadhifa muhimu hasa kwenye kazi za serikali. Waafrika hasa kutoka Misri, waasia, wazungu ni katika orodha kubwa ya wafanyakazi wa kigeni nchini humo. Wakenya wanajiona tamu sana Doha airport, k**a vile wako Nairobi. Waajiri ni wakali kwenye mikataba na kubana wafanyakazi hasa kwenye masuala ya kubadilisha kazi.

UTAIFISHAJI wa mafuta ulifanywa kwa awamu. Mafuta yaligunduliwa kwenye miaka ya 1950. Mwanzoni mafuta yalimilikiwa na kampuni ya British Petroleum (BP) na baadhi ya makampuni ya Iran. Wakati huo serikali ilikuwa ikimiliki asilimia 25, huku hisa zikiongezeka kidogo kidogo kila mwaka. Kufikia mwaka 1975 serikali ilishavunja mikataba ya awali. (kwa staili ile ya Acacia) Na kuanzia mwaka 1976 kampuni ya Qatar Petroleum imekuwa ikimiliki mafuta ya Qatar kwa *asilimia 100.* Sambamba na utaifishaji huo vituo vya kuuzia mafuta, teksi, mabasi na treni vinamilikiwa na serikali. Uber na teksi bubu zipo lakini ni marufuku kufika maeneo muhimu k**a uwanja wa ndege.

UTALIPENDA jengo la makao makuu ya kampuni ya QP. Ni mnara mrefu sana wa bluu uliopanda ki-New York. Chini kuna k**a tufe kubwa lenye maandishi ya Qatar Petroleum na juu ya gorofa hilo kuna kibaraza kinachozunguka usiku huku kikiwa na maandishi ya bluu yanayosomeka *QATAR PETROLEUM .* Ikiwa ni uthibitisho tosha kuwa kinachoendelea ndani ya jengo hilo ni mafuta ya Qatar tu.

SHIRIKA la ndege la Qatar pia linamilikiwa na serikali. Lina ndege kubwa za aina ya Boeing na Airbus zaidi ya 320. Ni ndege mpya za kisasa nyingine zina uwezo wa kuweka na kuondoa kivuli kwenye madirisha. Qatar hawana vivutio vingi vya utalii lakini ndege hizi hubeba watalii wengi waendao Afrika ya mashariki. Wanajaza ndege ya watalii kutoka Doha mpaka Kilimanjaro, halafu wanawarudisha kutoka Kilimanjaro kwenda Doha kwa kupitia Dar-es-salaam. ATCL wajipange vizuri na mtihani huu. Vilevile huduma za shirika hili ni nzuri sana. Achana na mashirika ya ndege za wazungu wanabania chakula. Qatar airways wanakupa mpaka chapati.

MIPANGO miji ya Qatar ni ya kukata na shoka. Si Ulaya si Marekani wanaowafikia. Waarabu hawa wana taa za barabarani zenye mwanga wa maua kwenye mlingoti mzima wa taa. Hakuna mashimo barabarani, na wana magari ya kifahari mno. Sio city k**a Tanga ni Metropole. Wana masoko na maduka ya kisasa likiwemo lile wanaloliita Villagio. Juu ya soko hili wamechora rangi ya mawingu inayofanya mtu akiwa ndani aone k**a anatembea nje. Mjengo wa aina hii hupatikana sehemu chache duniani ikiwemo Las Vegas, Johannesburg na Macau. Mahoteli yao ni ya kimataifa na ya hadhi za juu.

UWANJA wa ndege wa Doha ni mkubwa, unavutia na wa kisasa. Umbali wa kutokea temino mpaka kwenye ndege kuna mama wa kizungu aliuliza k**a safari ni ya basi au ya ndege. Boeing tano au sita za Qatar zinaweza kujipanga mstari zikisubiri zamu ya kuruka. Inawezekana ni uchache wa ardhi lakini huu uwanja huu umejengwa kwa kufukia mchanga baharini.

HALI ya hewa si nzuri k**a ya Tanzania. Waqatari wako jangwani. Joto la nyuzi 108 f, 44 (c) ni kawaida wakati wa majira ya joto. Ukitaka upate uhalisia wake ingiza kichwa kwenye oven. Lakini wanalimudu joto hili. Nyumba zao hata kwenye masoko kuna mizizimo ya viyoyozi usawa wa winter kali.

*KILIMO* kimewatupa mkono kutokana na kuwa jangwani. Wana mashamba machache ya ngano na tende. Lakini hakuna wanachokosa. Ukitaka kujua tofauti ya nyama za plastiki za MacDonald na nyama ya ukweli agizia mpunga na nyama Doha. Halafu kakae bichi ule biriani yao hawa jamaa.

WENYEJI ni waislamu na mavazi ya kiislamu yametawala barabarani. Misikiti huanz kuadhini saa tisa za usiku. Hawana uislamu ule wa kushikana mashati. Wageni wanachotakiwa ni kuzingatia sheria za msingi za nchi. Kwenye ndege zao na maduka yao hasa ya uwanja wa ndege wanauza pombe tena hata zike kali. Hata hivyo ndani ya ndege zao una chaguo la kusikiliza Quran badala ya kuangalia movie au vipindi vya televisheni. Vibaka barabarani wala hofu ya kutapeliwa hakuna.

MAJAHAZI ya kizamani yale ni kivutio kikubwa baharini. Usiku yanawaka mataa na kutembeza watalii baharini kwa malipo.

WANA mafuta na jangwa.

*PENGINE* walianza maendeleo zamani. La hasha, Qatar ni nchi changa kuliko nchi nyingi za Afrika. Ilipata uhuru mwaka 1971. Picha za Doha ya 1970 na picha ya Doha ya leo, tofauti yake ni k**a usiku na mchana.

KUBWA walilolifanya ni kumiliki kikamilifu rasilimali yao moja waliyopewa na Mungu.

0766 1995 64

09/10/2021

UJUE MWISHO WA DIKTETA ALIYEITIKISA LIBERIA, "SAMUEL DOE."_*

Huyu ndiye SAMUEL KANYON DOE rais aliyeuawa kikatili sana nchinii Liberia,,,,,,
Samuel Kanyon Doe alizaliwa May 6, 1951 jijini Tuzon, nchini Liberia...
Alfajiri ya Aprili 12, 1980, kikundi kidogo cha wanajeshi 17 kilijipenyeza ndani ya makazi ya Rais jijini Monrovia... Ikulu walimkuta Rais William Tolbert bado amelala... Wakamuua... Aliyeongoza kikundi hicho alikuwa askari kijana na wa cheo cha chini, Sajenti Samuel Doe...
Na inasemwa kuwa Doe alipoingia Ikulu na wenzake, alidhani watakwenda kumlalamikia Rais juu ya mishahara midogo ya askari wa vyeo vya chini... Lakini jinsi walivyoikuta Ikulu ikiwa nyepesi vile, ndivyo mipango ilipobadilika na kuamua kumuua Rais mwenyewe na kuchukua madaraka...
Samuel Doe alikuwa askari ambaye hata madarasa manne ya shule ya msingi hakuyamaliza... Alitoka kabila dogo la waishio misituni, kabila la Krahn... Ni watu wa kabila k**a lake, masikini na ambao ndio waliotoka vijijini na kukimbilia jijini Monrovia kutafuta vibarua na pesa... Kwa wenye bahati, k**a Samuel Doe, walionekana mitaani na kuitwa kujiunga na Jeshi...
Na k**a ilivyokuwa kwa Idi Amin, Urais ulimdondokea tu Samuel Doe, k**a vile mtu aliyeshinda bahati nasibu...
Ujio wa Samuel Doe uliwafaya WaLiberia waamini kuwepo kwa mabadiliko... Kuondokana na utawala wa kifisadi na kirasimu wa William Tolbert...
Samuel Doe akajitangaza kuwa Rais, April 12, 1980... Haraka sana akawatwanga risasi mawaziri wote wa Tollbert... Ni kwenye pwani ya bahari huku wananchi wakitazama k**a mechi ya mpira...
Sajenti Samuel Doe akatawala kwa kipindi cha miaka kumi... Nchi ikawa k**a imesimama....
Watu wa kabila la Samuel Doe waliogopewa na makabila mengine… Waliweza kufanya lolote lile na hakuna aliyewagusa… Waliua na waliwatisha wengine... Wengi wasio wa kabila la Rais Doe, waliishi kwa hofu kubwa…
Na kile ambacho kila mtu asiye wa kabila la Doe, alikuwa anakisubiri, ni kushuhudia mwisho wa Sajenti Samuel Doe…
Na hapa akatokea Charles Taylor… Huyu alikuwa rafiki wa zamani wa Sajenti Samuel Doe...
Lakini, urafiki wao ulikufa pale Samuel Doe alipodai kuwa Charles Taylor alimtapeli dola milioni moja… Kisha Taylor akatorokea Marekani… Huko akaanza kufanya biashara kwa mtaji wa fedha alizomtapeli Sajenti Samuel Doe…
Charles Taylor naye akaishia gerezani nchini Marekani kwa mashtaka ya utapeli… Lakini akatoroka jela na kukimbilia Ivory Coast... Na akiwa Ivory Coast, Charles Taylor akaanza kujipanga kwenda kuuangusha utawala wa Sajenti Samuel Doe… Charles Taylor akiwa Ivory Coast, alikiandaa kikosi cha wapiganaji 60… Kikosi kilikuwa tayari kwa kuingia Monrovia kumwondoa Samuel Doe madarakani…
Ilikuwa ni mwaka 1989… Wakati huo, wajuzi wa masuala ya kijeshi waliamini kabisa, kuwa Sajenti Samuel Doe angeweza, kirahisi kabisa, kumteketeza kijeshi Charles Taylor na kikosi chake cha watu 60… Sajenti Samuel Doe angeweza kufanya hivyo hata kabla Charles Taylor hajavikaribia viunga vya Monrovia…
Badala yake, ‘’Master Sergeant’’ Samuel Doe, aliwatuma mstari wa mbele, wanajeshi kutoka kabila lake la Krahn... Ni wanajeshi wa kuokoteza ambao wengine hawakuwa hata na viatu… Wanajeshi wale wa Samuel Doe, njiani wakitokea mji mkuu Monrovia wakielekea uwanja wa mapambano, wakaanza kufanya wizi wa ngawira, kuiba mali za watu…
Habari za askari ‘’vibaka’’ wa Samuel Doe zikasambaa haraka kwenye vijiji vya msituni…
Huko watu wakajitolea kujiunga na vikosi vya Charles Taylor kukabiliana na askari wa Samuel Doe…
Jeshi la Taylor likakua kwa haraka… Baada ya miezi sita tu, likaingia kwenye viunga vya mji mkuu wa Liberia, Monrovia, June 1990…
Ndipo hapo kwenye kambi ya Charles Taylor ugomvi ukazuka… Nani atakuwa Rais???... Nani atakuwa na mamlaka ya hazina kuu???... Ni ugomvi uliowatenganisha Charles Taylor na Prince Johnson aliyeamua kuachana na Taylor na yeye kuanzisha kikosi chake…
Wote wawili walikuwa na tamaa ya Ikulu. Vita sasa ikawa ya vikosi vitatu kugombania kuingia Ikulu ya Monrovia: Kikosi cha Sajenti Samuel Doe kinachojihami, kikosi cha Charles Taylor na kikosi cha Prince Johnson... Wote wakaanza kupigana wenyewe kwa wenyewe kugombania Ikulu ya Monrovia…
Mitaa ya Monrovia wakaonekana askari wa makundi tofauti wakipigana. Hata watoto waliingizwa kwenye vita vile vya kiwendawazimu…
Hatimaye, mwishoni mwa mwezi August 1990, vikosi kutoka nje viliingilia mgogoro ule... Ni vikosi vya Nigeria chini ya mwavuli wa ECOMOG, ni umoja wa mataifa ya Afrika Magharibi… Ecomog walikuwa na jeshi lilioongozwa na k**anda kutoka Nigeria... Jeshi hilo lilifika Monrovia na meli kubwa ya kijeshi…
Jumapili Septemba 9, 1990, Rais Samuel Doe aliposikia habari za ujio wa ECOMOG, akafanya kosa kubwa la kuamua kutoka Ikulu na kwenda mwenyewe bandarini kuonana na k**anda wa vikosi hivyo vya majeshi ya Nigeria... Samuel Doe hakuwa na msafara mkubwa... Aliwachukua walinzi wake na kuingia kwenye Mercedes Benz kuelekea bandarini…
Masikini, Rais wa nchi akajikuta anapita kwenye mji wenye miba… Akafika bandarini na hapo Prince Johnson alikuwa amewapanga askari wake kumshughulikia Samuel Doe… Zikapigwa risasi na walinzi wote wa Samuel Doe wakapoteza maisha… Samuel Doe mwenyewe risasi ilimpata mguuni na hakuweza kukimbia, akak**atwa…
Akafungwa kitambaa usoni na akapelekwa kwenye kuteswa... Prince Johnson akahakikisha mateso yale yanarekodiwa kwa kamera za filamu... Kwenye filamu hiyo, Prince Johnson anaonekana akipungiwa upepo na mwanadada huku akinywa bia na kumwangalia rafiki yake wa zamani, Samuel Doe akiteswa… Muda mwingi Prince Johnson alikuwa akimtaka Samuel Doe aseme zilipo fedha kwenye hazina…
Kuna wakati alisikika Samuel Doe akimwita rafiki yake wa zamani kwa jina alilozoea kumwita: "Prince, waambie walegeze kamba walizonifunga, nitasema kila kitu, walegeze hizo kamba kwanza!"…
Ukweli, kamba walizomfunga kwenye miguu na mikono zilikaza sana na kumletea maumivu makali… Waliendelea kumpiga huku wakimtaka ataje ilipo hazina. Walimtaka ataje akaunti yake ya benki…
Ndivyo ilivyokuwa barani kwetu Afrika, na labda mpaka leo… Rais dikteta anapopinduliwa, kikubwa kinachotafutwa ni namba ya akaunti ya benki alikoficha fedha… Mara nyingi ni kwenye benki za nje… Ndio, inahusu hazina ya nchi…
"Mkateni sikio k**a hataki kusema!" Alisikika Prince Johnson akitamka kwa hasira…
Askari wale wakamtupa Samuel Doe sakafuni, wakamkata sikio moja…
"Mkateni sikio lingine!", alisikika tena Prince Johnson akitamka…
Baada ya hapo, Rais Doe aliuawa kikatili Jumapili hiyo jioni, Septemba 9, 1990 baada ya kukatwa masikio yake, sehemu zake za siri na baadhi ya vidole vya miguu na mikono na hatimae mwili wake ulitembezwa mitaa mbalimbali ya jiji la Monrovia…
Huo ndio ulikuwa mwisho wa Dikteta Samuel Kanyon Doe wa Liberia.

Want your school to be the top-listed School/college in Iringa?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Iringa