EBONY Digital
31/03/2025
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema, amekosoa vikali taarifa iliyotolewa na chama chake kuhusu tukio la shambulio dhidi ya kiongozi wa wanawake taifa wa CHADEMA (BAWACHA). Mrema alionesha masikitiko yake kwa chama kutolaani kitendo hicho cha kikatili na badala yake kudai kuwa ni taarifa zinazozungumziwa mitandaoni. Alieleza kuwa chama hakikuonyesha mshik**ano kwa kiongozi huyo, na hakutoa pole, jambo ambalo linathibitisha kutokuwepo kwa umoja ndani ya chama.
Mrema alilalamikia kauli ya chama inayodai kuwa kinachunguza tukio, wakati huo huo kikitoa vitisho kwa mhanga, jambo ambalo linaweza kuathiri uchunguzi wa tukio. Alikosoa kauli za chama akizilinganisha na za uongozi wa Rais Hayati John Magufuli kuhusu ukandamizaji wa haki za binadamu.
Katika tamko lake, Mrema alisisitiza kulaani vikali ukatili wa kijinsia dhidi ya kiongozi huyo na kusema kuwa matendo k**a haya yanapaswa kupingwa na kila mtu mstaarabu, na kuitaka jamii, pamoja na vyama vya siasa, kuungana kupinga ukatili dhidi ya wanawake.
31/03/2025
Kanye West, mwanamuziki maarufu na mwenye utata, amekiri kwa mara ya kwanza kuwa anajuta kuwa na watoto na mke wake wa zamani, Kim Kardashian, ambaye kwa sasa wametalakiana wakiwa na watoto wanne. Katika mahojiano na DJ Akademiks, Kanye (ambaye sasa anajulikana k**a "Ye") alisema kuwa kumpatia ujauzito Kim ilikuwa kosa kubwa alilowahi kufanya maishani mwake, akidai kuwa hakupaswa kuwa na watoto nae. Aliongeza kuwa hakupata haki ya umiliki wa watoto wao—North, Saint, Chicago, na Psalm—hata katika suala la kutoa matumizi kwa uwiano wa 50-50.
Ye na Kim walikuwa katika ndoa kwa miaka sita, kutoka 2014 hadi 2021. Baada ya talaka, Ye alioa Bianca Censori, na kuna uvumi kwamba yupo mbioni kupata mtoto kutoka kwake ili kuokoa ndoa yao, licha ya tetesi kuhusu uwezekano wa kutalakiana kwao.
29/03/2025
Muimbaji Sean Kingston na mama yake Janice Turner wamekutwa na hatia ya ulaghai na wizi. Wamekabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kugushi nyaraka na utapeli wa vitu vyenye thamani ya $1 milioni (sawa na TSH Bilioni 2.68). Mashtaka yanayowakabili ni pamoja na ulaghai wa vito vya thamani ya $500,000, zaidi ya $200,000 kutoka Benki ya America, $160,000 kutoka kwa muuzaji wa magari ya kifahari, na kiasi kingine kutoka kwa benki na wauzaji wa vitanda. Hukumu yao itatolewa Julai 2025.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Address
Uhindini
Iringa
255