MWL. CHUSI

MWL. CHUSI

Share

08/05/2023

SOMO: MUNGU HUJIFUNUA KATIKA KIWANGO HICHO HICHO UNACHOMJUA.🇹🇿🇮🇱

Nakusalimu katika Jina Yesu Kristo, ndugu yangu katika Kristo Yesu.✝️

SALA;
Neema na iwe kwenu ninyi nyote ndugu zangu katika Kristo Yesu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo, na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema Mungu wa faraja yote.
Amina 🙏🙏🙏

UTANGULIZI:

Sikia mpendwa kiwango chako cha kumjua Mungu ndio mpaka wako wa ufahamu juu ya Mungu.

Kiwango chako cha ufahamu juu Mungu ndicho kiwango cha imani uliyonayo. Hakika haiwezi kwenda mbali ya ufahamu katika imani yako.

Kwa namna unavyokuwa karibu sana na Mungu ndivyo unavyomjua zaidi Mungu, alivyo mkuu na wa kuogofya sana. K**a vile ukiwa unaiona ndege/ Meri kwa ukaribu bila shaka unajua ilivyokubwa, ndivyo Mungu alivyo;

Isaya naye kwa kuwa hakuwa karibu sana na Mungu hapo awali, alimuona Mungu wa kawaida sana.
Lakini anasema “ katika mwaka ule aliyokufa mfalme Uzia nalimuona Bwana ameketi katika kiti cha enzi kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu”. 5 Ndipo niliposema, Ole wangu kwa maana nimepotea;

Isaya 6:1-3
[1]Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.

[2]Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.

[3]Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.

Isaya 6:4-5
[4]Na misingi ya vizingiti ikatikisika kwa sababu ya sauti yake aliyelia, nayo nyumba ikajaa moshi.

[5]Ndipo niliposema, Ole wangu! Kwa maana nimepotea; kwa sababu mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya watu wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona Mfalme, BWANA wa majeshi...đź–Š

Ufafanuzi;
Haya yote anayasema nabii Isaya kwa sababu amemkaribia Mungu na kuona UKUU wake, naye anaogopa, kwa nini anaogopa anajiona yeye ni mchafu hastahiri kumtazama Mungu ndio maana anakiri uovu wake akisema, Mimi ni mtu mwenye midomo michafu, nami ninakaa kati ya wenye midomo michafu; na macho yangu yamemwona mfalme.

Lakini pia kumbe, kuna watu ukiwa nao karibu hautakuwa na ufahamu mkubwa juu ya Mungu, Nabii Isaya anasema; katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimuona Bwana.

Lakini pia nabii Habakuki, mwanzo alikuwa akilalamika za juu ya Mungu na kuona mbona hatendi vile alivyotaka yeye, lakini baada tu ya kumjua Mungu,amebadilika.
Anasema katika sara yake 2

“Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa”.


Lakini ukiwa mbali sana na Mungu ndivyo unavyo muona Mungu mdogo na hawezi kutatua shida zako.

Na wakristo wengi wako mahali hapa, ndio maana kunabaadhi ya wakristo wakipata shida kubwa hao hao wanakwenda kwa waganga wa kienyeji, Je! Ni kweli Mungu hawezi kutatua changamoto yako uliyonayo? Au umemuona Mungu mdogo na mganga mkubwa zaidi kuliko Mungu?

Ni kweli maisha yako yana vikwazo vingi uchumi ni mgumu Je! Umeona Mungu hawezi? Mpaka umeenda kwa miungu mingine? Nikwambie tu! Katika mambo ambayo ni chukizo sana mbele za Mungu ni kuomba msaada na kuabudu miungu mingine.

Ni kweli haujapata mchumba na umekuwa ukimngoja Bwana, mwishowe ukachoka na kwenda kutafuta msaada mahali pengine, je! Ni sawa?

Ni kweli unachangamoto ya ndoa lakini ndo uchukue maamuzi magumu na mabaya yenye kuthiri wengine, kweli utasema unamjua Mungu wewe!

Je! Ni kweli kuwa pombe ndio suruhisho la matatizo yako na stress ulizonazo, angalia vizuri mpendwa maana wakati mwingine mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe.

Ni kweli una madeni sana, ndio uamue kujirahisi k**a wewe mama au binti kwa sababu ya pesa kweli unamjua na kumpenda Mungu wewe?

Unaweza ukamjua Mungu, kwa udogo, ukawaida au kwa ukubwa, itategemeana na vile Ufahamu ulionao juu ya Mungu.

Ni kweli hauna kazi sasa ndio udhurumu wengine na kuwa tapeli na kuiba,unadhani ni sawa!. Sikia mpendwa akipandacho mtu ndicho atakacho kivuna.

Ukipanda uzinzi utavuna magonjwa.
Ukipanda ulevi utavuna laana na uharibifu.
Ukipanda wizi utavuna laana na kutangatanga.
Ukipanda uzurulaji utavuna umasikini.
Maana mshahara (malipo) ya dhambi ni mauti.

Mpenzi katika kristo Yesu panda mbegu njema .

Ni kweli una uhitaji na hiyo kazi, sasa ndio utoe rushwa ili uipate hiyo kazi! Sasa utakuwa na utofauti gani kati yako wewe uliyeokoka na asiyeokokoka? Ikiwa nawe unaenenda k**a mataifa waenendavyo, Biblia inasema wala tusienende k**a mataifa.

Wapenzi katika kristo Yesu, tuache kumuahibisha kristo Yesu, kwa kuyafanya yasiyompendeza Mungu tunamfanya Yesu kana kwamba hakufanya chochote msalabani, ninaandika ujumbe huu nikiwa na uchungu sana na huku machozi yakinitiririka moyoni mwangu, maana katika kazi ambayo Bwana Mungu ameniitia ni kuwaambia watu juu ya nyakati za mwisho na amenipa kazi ya kuwalilia watu juu ya maovu yao...đź–Š

Ushuhuda;
Siku moja nilikuwa katika maono ya usiku, nikachukuliwa na kupelekwa mahali fulani, nami nikaona bara bara Nzuri sana ya rami,

kisha nikaona watu wakipita na wote walikuwa wakielekea mwelekeo mmoja, na walikuwa wakielekea kusini, wengine walikuwa wakitembea kwa miguu na wengine walikuwa kwenye magari yao, na kati wa watu niliowaona niliwaona, mabinti wawili ambao ninawafahamu nilishawahi kuwaambia juu habari za Mungu.

Nao pia walikuwa katika safari hiyo na mikononi mwao walishika fimbo ambazo walizitembelea na walioneka k**a wazee sana na walitembea k**a wazee.

Nikauliza nini maana yake? Ndipo, Neno la Bwana likanijia kusema hii ndio njia walioichagua watu wengi sana, ambayo machoni inaonekana kuwa ni njema sana lakini kumbe ni njia za mauti.

Nilisikia hivi nikajikuta ninalia kilio kisicho cha kawaida, na wakati ninalia nilikuwa nikimwita binti mmoja kati ya wale ninaowafahamu, lakini alikuwa akigeuka na kunitazama halafu anaendelea na safari, nilimwita mara tatu, lakini haikusaidia.

Kulipokucha asubuhi, nilianza kutafakari maono hayo nikajikuta nina uchungu na ninalia tu moyoni,
ikaja mistari kutoka kitabu cha mithali 14:12 iliyosema masikioni mwangu kuwa “ 12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, lakini mwisho wake ni njia za mauti”
Ni kwa sababu hauoni....đź–Š

ZINGATIA MAHUSIA YA BWANA.

Mpendwa weka shauku ndani yako ya kumpenda Yesu naye ataonekana kwako.

kuna wakati tunampa Mungu wakati mgumu sana, hapendi tuangamie,

Maombolezo 3 32 “Maana moyo wake (Mungu) haupendi kuwatesa wanadamu wala kuwahizunisha”

Kuna wakati Mungu anataka kutuangamiza kwa sababu ya dhambi lakini anaona wasiomjua Mungu na shetani watatucheka na kusema, tazama Mungu wao yuko wapi mbona amewatelekeza na kuwaacha katika uharibifu? Na uharibifu umewapata.

Na ndio maana Mungu alileta neema na kuachana na sheria kwa maana kwa sheria aliona hakuna mwadamu angeweza kustahiri na kuokoka kutoka katika dhambi, tazama kitabu cha;

Waebrania 10:16
[16]Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana,
Nitatia sheria zangu mioyoni mwao,
Na katika nia zao nitaziandika;
ndipo anenapo.

Mpendwa kuna saa inakuja wala si mbali bali karibu.

UJUMBE HUU NI KWA AJIRI YAKO MPENDWA.

Leo kwa neema na kibari cha Mungu napenda tujifunze namna Mungu anajifunua/ anadhirika kwenye maisha yetu.

Watu wengi hawafahamu siri hii, lakini ni ukweli usiopingika kuwa kiwango chako cha kumjua Mungu ndicho kiwango hicho hicho Bwana Mungu atajifunua kwako.

Je! Unamjua Bwana Mungu k**a nani?

Kwanza kabisa tambua ya kuwa;

Mungu ni Roho,
Yohana 4:24 Biblia inasema “ Mungu ni Roho nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika Roho na kweli”

Ufafanuzi;
Na k**a Mungu ni Roho basi unapaswa kumjua Mungu katika namna ya kiroho na si namna ya kimwili.

Hivyo basi hata kumjua Mungu ni tendo la kiimani, maana Mungu ni Roho, Biblia inasema.

katika Waebrania 11 : 1-3 “ Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. 2 Maana kwa hiyo wazee wetu walishuhudiwa. 3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu. Hata vitu visivyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.

Ufafanuzi;
sasa tunajifunza kuwa, kumbe kuwa na ufahamu wa kimungu inakuhitaji uwe na imani kwa maana haya ni mambo yasiyoonekana lakini ni bayana yaani yapo, na pia kumbe kuwa na imani kubwa kwa Mungu aliyezifanya mbingu na nchi inakuhitaji uwe na ufahamu wa kimungu na ufahamu unapatikana katika neno lake yaani Biblia takatifu.

Sasa kuna watu wana imani lakini wamekosa ufahamu wa kimungu na wengine wana ufahamu tu k**a mafarisayo lakini wamekosa imani kumbuka haya ni mambo ya kiroho kabisa.

Ndio maana neno la Mungu linasema mna macho lakini hamuoni na mna masikio lakini hamsikii, hii ina maana ya macho ya kiroho na masikio ya kiroho na sio haya ya nyama yaani ya mwili.

Ezekieli 12:1-2
“ Neno la Bwana likanijia tena, kusema 2 Mwanadamu wewe unakaa kati ya nyumba iliyoasi, watu ambao wana macho ya kuona, ila hawaoni, wana masikio ya kusikia, lakini hawasikii; kwa maana ni nyumba iliyoasi.

Ufafanuzi;
Kumbe dhambi ina leta giza katika macho, masikio na ufahamu.

Sasa ili kukua kiroho na kumjua Mungu zaidi ya vile tunavyomjua, tunapaswa kuwa na imani pamoja na ufahamu wa kimungu.

Biblia inasema imani pasipo matendo imekufa, na mimi k**a mtumishi wa Mungu, ninasema kuwa imani pasipo ufahamu wa kimungu imekufa pia.

Hivyo basi;
Msingi wa kukua kiroho na kutembea na Mungu katika roho na kweli inakuhitaji kuwa na;





Vinakwenda sambamba, utasema unaamini nini ikiwa hauna ufahamu wa mambo hayo, watu wengi sana wamekwama hapa, wakiamini kuwa na imani na matendo inatosha kabisa lakini leo nataka nikwambie mtu wa Mungu, tafuta maarifa pia ili namna yako ya kumjua Mungu ikue.

Biblia inasema Hosea 4:6-7
“watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe usiwe kuhani kwangu mimi, kwa kuwa umesahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako”

Ukiwa una maarifa na ufahamu wa kimungu utakuwa huru.

“Ifahamu kweli nayo kweli itakuweka huru”

Ndio maana Yesu aliwaambia wanafunzi wake akisema mngalikuwa na imani japo punje ya haradari (yaani japo kidogo) mngaliweza kuamuru mlima huu ng’ooka nao ukatupwa baharini nao ungalitii,

Ufafanuzi;
Sasa hapo Yesu alikuwa anawaambia wanafunzi wake juu ya “Nguvu ya imani” (The power of faith) lakini ndani yake kuna ufahamu wa kujua kuwa ndani yetu kuna nguvu ya kuamlisha vitu na vikawa, k**a vile Baba yetu Mungu alivyo na nguvu hii na sisi pia tunayo, Maana sisi ni warithi wake na ni wana wa agano, ila tatizo kubwa hatuna ufahamu.

Waefeso 3:20 “ Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo, kwa kadri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;”

Kumbe ndani Yetu kuna nguvu kubwa sana, lakini ni ngumu kuamini kwa sababu ya kukosa ufahamu.

Biblia inasema “ kumcha Bwana ni chanzo cha maarifa. Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu”

Mpendwa jitathimini kiwango chako cha kumjua Mungu ndicho unachomwamini Mungu.

Kuna watu huwasema baadhi ya watumishi wa Mungu kwa miujiza inayofanyika wakitilia shaka (doubt) kuwa sio Mungu ni kweli wengine sio, maana Biblia inasema katika Ezekia 13:1-10 wako manabii ambao wamefanya ambayo Mungu hakuwatuma, kifupi wamesema uongo, na kutaniri uongo, hivyo basi ni manabii wa uongo.

Lakini wapo wakristo wengi ambao wanashaka na kila mtumishi, hususani manabii na mitume, wakiamini kabisa wanatumia nguvu za giza katika miujiza hiyo.

Si dhambi kuchunguza yupi ni mtumishi wa Mungu wa kweli, maana Biblia inasema zichunguzeni hizo roho.

Lakini jambo lingine la kujifunza ni kwamba watu wanashaka na Mungu kutokana tulivyomfahamu, au kukosa ufahamu wa kutosha juu ya Mungu. ukitia tu ufahamu juu ya Mungu imani yako inaongezeka papo hapo.

KUWA KIELELEZO BORA CHA KRISTO YESU.

ANGALIA UKRISTO WAKO USIWE KIKWAZO KWA WENGINE, WASIPATE KUMJUA MUNGU, MAANA SISI NI NURU YA ULIMWENGU HIVYO TUNAPASWA KUANGAZA NA WENGINE WAMJUE MUNGU BILA HATA KUWAAMBIA HABARI ZA MUNGU.
ILA KWA MATENDO YETU TU WAONE HAKIKA WATU HAWA WANAMWAKILISHA MUNGU WA MBINGUNI HAPA DUNIANI.

Kwa maana matendo yetu sisi wakristo yanamuhubiri Kristo zaidi kuliko hata kusema kwetu.

Ni maombi yangu kwa ajiri ya siku hii ya leo,
Mungu akupe ufahamu na umtazame Mungu kwa namna mpya.

MUNGU AKUBARIKI SANA.

By Mwl. Chusi Steven.
+255742874709
08/05/2023
Manyara - Tanzania
Stay Blessed.

Want your business to be the top-listed Realtor/realty Service in Iringa?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address


Mkwawa
Iringa
CHUSI1444