Shamba Fm Radio
VYAMA VYA USHIRIKA VYATAKIWA KUIMARISHA UONGOZI NA UWAJIBIKAJI IRINGA
Vyama vya ushirika vimetajwa kuwa nguzo muhimu ya maendeleo ya kiuchumi katika Mkoa wa Iringa, huku mafanikio yake yakitegemea uwepo wa uongozi bora, uwajibikaji na usimamizi madhubuti wa rasilimali.
Hayo yameelezwa leo Juni 12, 2026, katika Maadhimisho ya Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Iringa yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.
Maadhimisho hayo yaliambatana na kaulimbiu isemayo “Vyama vya Ushirika kwa Dunia ya Amani: Linda Ushirika, Chagua Uadilifu,” na yalikutanisha viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa sekta ya ushirika kujadili changamoto na fursa za kuimarisha vyama vya ushirika.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, ambaye alikuwa mgeni rasmi, alisema kuwa uongozi mbovu ni miongoni mwa sababu zinazochangia kudhoofika kwa vyama vingi vya ushirika.
Amebainisha kuwa baadhi ya vyama vimekuwa vikikopa zaidi ya uwezo wake wa kifedha na hivyo kujikuta vikilemewa na madeni yanayokwaza maendeleo yake.
Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wa jukwaa hilo walisema kuwa vyama kadhaa vya ushirika vimepoteza mwelekeo kutokana na usimamizi usiozingatia maslahi ya wanachama. Hali hiyo imechangia kudhoofika na hata kufa kwa baadhi ya vyama.
Washiriki hao wamesisitiza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya uwajibikaji, kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa shughuli za vyama, pamoja na kuwashirikisha wanachama katika maamuzi muhimu ili kuhakikisha vyama vya ushirika vinakuwa imara, endelevu na vinawanufaisha wanachama wake.
Mahojiano ya moja kwa moja na timu ya Iringa Alla Stars Veterans mepema Juni 11 saa 1:00 jioni kuelekea katika mchezo wao wa kirafiki dhidi ya timu ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.
11/06/2026
AFRIKA KUSINI K**A NI WANA WA MUNGU WAJIOKOE WENYEWE
Kipindi cha pili kinaendelea Timu ya taifa ya Mexico ipo mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya kikosi cha Timu ya taifa ya Afrika ya kusini.
Goli la pili likifungwa na Mshambuliaji namba Moja wa timu hiyo ya Mexico Raul Jemenez.
Endelea kuwa karibu na Mitandao yetu kwa Taarifa zaidi.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Utalii Road
Iringa