Makutano Tv
08/06/2026
MAPOGORO "B" SHULE YA MSINGI WILAYA YA MBARALI , MBEYA.
Makabidhiano ya Mradi wenye mafanikio ( SWASH) katika Shule ya Msingi Mapogoro B Mbarali.
Mradi huu uliotekelezwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Afya Plus kwa msaada wa Nawiri Foundation katika kuboresha miundombinu ya maliwato, chumba cha kujihafadhia kwa wasichana ( kuzingatia hedhi salama) matanki ya kuhifadhia maji safi na salama lita 10, 000 pamoja na program saidizi ili kuwezesha uelewa na ujuzi wa maarifa mapya katika mabadiliko ya tabia kwa wanafunzi.
@santation@hygiene@mbaralidistric
21/05/2026
Jeshi la Polisi kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Iringa kwa kushirikiana na wadau wakiwemo viongozi wa dini, leo wametoa elimu ya kujitambua na motisha kwa wanafunzi wasichana wanaosoma Shule ya Sekondari Mlamke iliyopo Manispaa ya Iringa.
Katika elimu ya hamasa kwa wasichana Inspekta Lidya Sospeter kutoka Dawati amehimiza wasichana kutambua mbinu sahihi za kukabili mabadiliko hasi ya kimwili yanayokinzana na tabia na maadili mema.
" nawapa mbinu bora ambayo inaweza kuwasaidia kukabili vichocheo vya mabadiliko ya mwili ni pamoja na kufanya mazoezi, kupanga ratiba na kuisimamia kwa ustadi" anasema Insp. Lidya
Aidha amewaasa mabinti kujidhatiti katika ufaulu wa masomo yao na kuwahakikishia kufikia ndoto zao iwapo watakuwa tayari kuwa mfano wa mabadiliko katika maadili mema na kuongeza kuwa kupitia Dawati la Jinsia Jeshi la Polisi limesogeza huduma rafiki kwa vijana hadi ngazi ya Kata ili kuweza kuwapatia msaada wa ushauri na kupokea taarifa katika changamoto wanazozipitia.
Pamoja naye Inspekta Lydia aliambatana na Polisi Kata ya Ilala/Makorongoni A/Insp Magreth Laizer na Afisa Ustawi
wa Kata
17/05/2026
JUMAPILI NJEMA
IRINGA
Watoto KKKT Mtwivila wamejitokeza kusaidia kazi ya usogezaji tofali ktk ujenzi wa Kanisa jipya.
Je hapo ulipo watoto wanashiriki vipi katika shughuli za kijamii? Je wanazo taarifa za maendeleo katika Kijiji/Kata/Mtaa?
TUPE MAONI YAKO
-MMMAM
Click here to claim your Sponsored Listing.
Telephone
Website
Address
Iringa
255