Mwl Elisha Mathayo

Mwl Elisha Mathayo

Share

02/09/2024

KANUNI YA KUOMBA
Kwa nini lazima tuombe kwenye kila jambo?
1 Thessalonians 5:17
Pray without ceasing. (ombeni bila kukoma)

Maisha tunayoishi hapa duniani ni maisha ya kanuni kila wakati tunapotaka kufanikisha jambo fulani lazima tujikite katika kanuni zake
Katika nyakati hizi za mwisho watu wengi hutaka mambo yatokee bila kufuata kanuni ndio maana kuna wakristo wengi wasio na matokeo kwa sababu hawataki kufuata kanuni za utokeaji wa matokeo

Jambo moja la kufahamu ni kwamba hakuna jambo lisilo na kanuni na Mungu ni Mungu wa kanuni na anaishi na kufanya mambo yake kwa kanuni , kuna mambo mengi ambayo watu wanashindwa kuyafikia kwa sababu hawajaamua kuzifuata kanuni

Kwa nini kila jambo lina kanuni yake?
Kila kitu unachokiona kwa macho ya damu na nyama kina chanzo chake ambacho hakionekani (katika Ulimwengu wa Roho)
Ngoja niseme kidogo kuhusu Ulimwengu wa Roho
Ulimwengu wa Roho ni ulimwengu usioonekana kwa macho ya damu na nyama ila ndio ulimwengu unaoongoza huu unaonekana kwa macho ya damu na nyama kwa sababu vinavyoonekana vyote si vya kudumu na ni matokeo ya vile visivyoonekana
Ulimwengu wa roho una nguvu kuliko huu wa macho ya damu na nyama kila jambo linalotokea hapa duniani huwa limeshatokea katika Ulimwengu wa Roho. Ulimwengu wa roho hauna bahati mbaya wala hauna bahati kila kitu kinaendeshwa kwa kanuni na ni ulimwengu usio tania ulimwengu ambao viumbe wake wako serious na kazi zao kuliko huku duniani.

Ulimwengu wa Roho umetawaliwa na Viumbe wa rohoni ambao ni roho, viumbe hawa wamegawanyika katika maeneo mawili
1: Viumbe wa roho wa Nuru ( Upande wa Mungu)
2: Viumbe wa roho wa Giza ( Upande wa Shetani)

Photos from Mwl Elisha Mathayo's post 03/12/2023

Tunamtukuza Sana Mungu wetu kwa ajili ya jumapili ya leo ..
Tumekuwa na wakati mzuri sana wa ibada ya sikukuu ya vijana CFD's hakika tumemuona Mungu



📸 by IT BENCH

Want your school to be the top-listed School/college in Iringa?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Website

Address


Iringa
Iringa