EK.com

EK.com

Share

11/01/2024

🌹🌷MPINGA KRISTO ANAIONGOZA DUNIA🌹
SIRI MOJA TU LEO NAKUPA
Leo nataka nikukumbushe na utambue kitu kimoja kwamba hii DUNIA /UMLIMWENGU huu unaendeshwa na mfumo wa MPINGA KRISTO yaani ufalme wa mpinga kristo ndio unao drive ulimwengu huu.....
MATH 4:8 - 9
KIVIPI.?
👉Nimekuja kugundua kua zaidi ya 90% ya hiki kitu tunaita UTANDAWAZI nyuma yake kuna huu mfumo, yaani kila kinacho anzishwa ulimwenguni, kwa hali ya kawaida ya kibinadamu huonekana kua ni chema na kina tusaidia lakini nyuma ya kile kinaanzishwa huwa na kusudi la pili ambalo ni kumtenganisha huyu binadamu kwa habar ya kiroho na Mungu. Na hii ndio sababu wakristo wengi tuko makanisani lakini kwa upande wa rohoni hatuna NGUVU yoyote ya kumpinga shetani na hatimaye tunaishia kukimbilia kwa MANABII ambao wakati mwingine wala hata hatujui ni wana mtumikia Mungu gani na mwishowe tunafungamanishwa na hiyo miungu wanayo iabudu. Na kwa bahati mabaya sana hata wakitokea watumishi wenye uelewa juu ya mambo flani kuonya juu ya mambo flani na kutokana na watu kuyapokea na kuyaishi basi huwageukia watumishi hao na kuwaona ni maadui.
YOH 16:32 - 33
MAANA YAKE NI NINI...?.....Maana yake nikwamba k**a ulimwengu huu utaendeshwa na watu walioko kwenye huu mfumo yaani hawamjui Mungu na wala hawana hofu ya Mungu ndani yao, tafsiri yake ni kwamba taifa haliwezi kua salama na pia ulimwengu hauwezi kua salama, kwani kila mfumo, yaani uanzilisho wa vitu ulimwenguni au ndani ya taifa utakua ni kwa shinikizo la utawala huo wa mpinga kristo (mfano: mitindo ya maisha, wearing style, economic style, democratic style etc) yaani taifa ni lazma lita ongozwa tu kwa kufuata sheria ya mwenye nguvu yaani mpinga Kristo. Ndio maana tunaona uanzilisho wa SHERIA tofauti tofauti ambazo wala haziwi na sura ya Mungu na wala sio za lazma lakini hutengenezewa mazingira ya kua za lazima.
Hivyo usiishi kwa kufuatisha namna ya ulimwengu huu,
WARUMI 12:1 - 2
👉kwani ufalme wa mpinga kristo unapambana kuhakikisha kila binadamu alie hai ulimwenimguni ni ana enende katika mfumo wa maisha ambayo kwa namna moja au nyingine tu ni anamkufuru au kumkosea Mungu
SIO KILA AINA FLANI YA MAISHA AU MFUMO UNAO ANZISHWA UMLIMWENGU unapaswa kuufanya, HAPANA, soma BIBLIA kwani ina mwongozo wote wa ni jinsi gani mkristo unapaswa kuishi, na niyapi yakupasayo kutenda.

11/08/2020

Quality....

Want your business to be the top-listed Business in Dodoma?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Mwanjerwa
Dodoma