Dodoma MPYA

Dodoma MPYA

Share

Oparesheni “Kupika na Kupakua” kuondoka na watu Dodoma Jiji 05/09/2018

https://youtu.be/EDW5r3ibj8Q

Oparesheni “Kupika na Kupakua” kuondoka na watu Dodoma Jiji Mkuu wa wilaya ya Dodoma Patrobas Katambi ameanza ziara ya kutatua kero na matatizo mbalimbali katika kata za jiji la Dodoma huku akiapa kusimamia haki za wa...

Wavamizi wa eneo la Barabara jijini Dodoma wavunjiwa kupisha ujenzi wa Lami 18/08/2018

https://youtu.be/Xvfg1ynEECc

Wavamizi wa eneo la Barabara jijini Dodoma wavunjiwa kupisha ujenzi wa Lami Maandalizi ya kufungua barabara ya mzunguko wa nje (Mlimwa Outer Ring Road), Wavamizi wa eneo la barabara mitaa mbalimbali ya jiji waondelewa.

Photos from Dodoma MPYA's post 25/06/2018

MATIBABU YA KIBINGWA HOSPITALI TEMBEZI YAANZA LEO JUNI 25 JIJINI DODOMA

Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeanza rasmi zoezi la siku 5 la kutoa huduma ya matatibu kwa wagonjwa mbalimbali kwa mfumo wa Hospitali Tembezi linalofanyika katika Hospitali Teule ya Wilaya Mtakatifu Gemma iliyopo Kata ya Miyuji Jijini humo.

Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma Hamad Nyembea amesema huduma ya Hospitali Tembezi ni jukwaa linalowakutanisha madaktari Bingwa wa fani mbalimbali za utabibu k**a mgonjwa ya akina mama na watoto, Figo, Moyo, Koo na Pua, Kinywa na Meno, Shinikizo la Damu, Sukari, Tezi Dume, Shingo ya Kizazi, Macho, Masikio, pamoja na upasuaji wa mifupa na wa kawaida.

Ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la Dodoma na Wilaya za jirani hususan wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali kutumia fursa hiyo vizuri.

"Kuna wagonjwa wengine ambao wameandikiwa rufaa kwenda Hospitali za mbali k**a Muhimbili Dare es Salaam na hawana uwezo, hii ni fursa kwao kwani hapa kuna madaktari Bingwa wa fani zote na watahudumia kwa muda wa siku tano kuanzia leo, mpaka Ijumaa Juni 29.

Alifafanua kuwa utaratibu wa matibabu ni wa kawaida ambapo wagonjwa wenye Bima za Afya za NHIF na CHF watatibiwa kwa kutumia kadi zao na wale wasio na Bima watachangia Shilingi elfu 5 k**a gharama ya kuonana na Daktari, na kwa huduma ya upasuaji mgonjwa atachangia Shilingi elfu 30 tu.

Want your business to be the top-listed Advertising & Marketing Company in Dodoma?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Website

Address


Iringa Road
Dodoma
123

Opening Hours

Monday 09:00 - 15:00
Tuesday 09:00 - 15:00
Wednesday 09:00 - 15:00
Thursday 09:00 - 15:00
Friday 09:00 - 17:00