Chama Cha Mapinduzi

Chama Cha Mapinduzi

Share

Photos from Chama Cha Mapinduzi's post 15/05/2026

MICHANGO MASHULENI IKOMESHWE- KIHONGOSI
MUSOMA: Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Kenani Kihongosi ameelekeza suala la michango mashuleni likome, na kuhakikisha wananchi wanatendewa haki kwa kupata huduma kwa mujibu na maelekezo ya serikali ili kuepuka kutengeneza mazingira ya kuonekana wanaweka vikwazo kwa wananchi wao.

Kihongosi ameeleza hayo leo Aprili 14,2026 alipokuwa akizungumza na kusikiliza kero za wananchi katika viwanja vya Mkendo Musoma Mjini mkoani Mara, ikiwa ni mwanzo wa ziara yake ya kikazi katika mkoa huo.

Kihongosi ametoa maelekezo hayo baada ya kupokea changamoto ya mama mmoja ambaye hakujitambulisha kwa majina yake alidai kuwa na changamoto ya uwezo na kushindwa kusomesha watoto wake akieleza kuwa moja ya watoto hao yupo kidato cha nne lakini ameshindwa kwenda shule kwa sababu hana uwezo wa kumlipia fedha ya kambi ambayo ni zaidi ya Sh 600,000.

Baada ya kusikia Changamoto hiyo Kihongosi alimuita Afisa Elimu Sekondari wa Mkoa wa Mara, Aviti Malya ili kutoa ufafanuzi wa suala hilo alidai kuwa ni kweli kuna utaratibu huo lakini ni kwa wazazi wenye uwezo na kiasi kinachotakiwa kulipwa ni Sh 680,000 kwa ajili ya kulipia umeme, maji na mahitaji mengine muhimu wawapo kambini hapo.

Baada ya kusikiliza hilo Kihongosi alisema suala hilo bado ni changamoto na linaleta ukakasi kwa sababu k**a ni watoto wa darasa moja na ni masomo sawa, hakukuwa na ulazima wa kufanya hivyo na badala yake wangewaambia wazazi wachangie chakula ili kuwasaidia watoto hao kuliko kutoa kiasi hicho cha fedha.

โ€œKwanini hamkwenda na utaratibu wa kuchangia chakula na sio fedha labda
Mpeleke mahindi au maharage au mchele, wa sababu la Sh 600,000 haina tofauti na shuke binafsi na k**a serikali tunahubiri kwamba tunatoa elimu bila malipo sasa hoja k**a hii sioni uhalali wake mimi binafsi,โ€ amesema Kihongosi.

15/05/2026

๐—–๐—–๐—  ๐—ฌ๐—”๐—ช๐—”๐—ง๐—”๐—ž๐—” ๐—ช๐—”๐—ญ๐—”๐—ช๐—” ๐—ž๐—จ๐—ฆ๐—œ๐— ๐—”๐— ๐—œ๐—” ๐— ๐—œ๐—ฅ๐—”๐——๐—œ ๐—ž๐—ช๐—” ๐—ช๐—˜๐—Ÿ๐—˜๐——๐—œ

๐™ˆ๐™ฌ๐™š๐™ฃ๐™š๐™ฏ๐™ž ๐™†๐™š๐™ฃ๐™–๐™ฃ๐™ž ๐™–๐™๐™ž๐™ข๐™ž๐™ฏ๐™– ๐™‘๐™ž๐™Ÿ๐™–๐™ฃ๐™– ๐™ ๐™ช๐™จ๐™๐™ž๐™ง๐™ž๐™ ๐™ž๐™จ๐™๐™ฌ๐™– ๐™ž๐™ก๐™ž ๐™ ๐™ช๐™ฃ๐™ช๐™›๐™–๐™ž๐™ ๐™– ๐™ฃ๐™– ๐™›๐™ช๐™ง๐™จ๐™– ๐™ฎ๐™– ๐™–๐™Ÿ๐™ž๐™ง๐™– ๐™ ๐™–๐™ฉ๐™ž๐™ ๐™– ๐™ช๐™ฉ๐™š๐™ ๐™š๐™ก๐™š๐™ฏ๐™–๐™Ÿ๐™ž ๐™ฌ๐™– ๐™ข๐™ž๐™ง๐™–๐™™๐™ž.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. ๐—ž๐—ฒ๐—ป๐—ฎ๐—ป๐—ถ ๐—ž๐—ถ๐—ต๐—ผ๐—ป๐—ด๐—ผ๐˜€๐˜‚ ametembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji wa barabara zenye urefu wa kilometa 3.364, Kituo cha Mabasi cha Bweri na soko la kisasa Nyasho, leo tarehe 14 Mei 2026.

Katika ukaguzi huo Mwenezi Kenani amewataka wafanyakazi wazawa wanaosimamia miradi mbalimbali ya maendeleo kuwa wazalendo na kuhakikisha wanailinda kuepuka hujuma na kuhakikisha kazi zinafanyika kwa weledi ili wananchi waliokusudiwa kunufaika na miradi hiyo.

โ€œTunawatakia kila la heri kikubwa tu ninyi wazawa muwe wazalendo katika kusimamia hii miradi msije mkaungana na wakandarasi, mkahujumu miradi,โ€ Alisema Kenani.

Akisomewa taarifa ya mradi huo na Mkandarasi Aloyce Kadokado, alisema mradi huo wa uboreshaji wa barabara unahusisha barabara ya Shabani, Mukendo , Musoma Bus hadi Saa Nane zenye jumla ya kilometa 3.364 na ujenzi wa Stendi ya Bweri na Soko la Nyasho ambao unatarajiwa kufharimu zaidi ya Sh bilioni 21.537.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa hadi kufikia sasa mradi umekamilika kwa 21.90% na muda wa mradi uliopita ni 32.33% ambapo Mwenezi Kenani alibaini ucheleweshaji wa utekelezaji wa mradi huo.

Kutokana na hilo, Mwenezi Kenani alihoji ili kufahamu ni changamoto gani iliyosababisha kuchelewa kwa utekelezaji wa mradi huo na katika majibu ilielezwa kuwa changamoto cha mvua ni moja ya sababu zilizopelekea kuchelewa kukamilika kw amradi huo.

Pamoja na changamoto hizo zilizoelezwa, Mwenezi Kenani alimtaka mkandarasi kuongeza kasi ya utekelezaji wa mradi huku akisisitiza kuwa kuna vijana wanaohitaji ajira na ni

14/05/2026

Kazi na Utu, Tunasonga Mbele โœ…

Photos from Chama Cha Mapinduzi's post 13/05/2026

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndugu Asha-Rose Migiro, ameshiriki dhifa ya jioni iliyoandaliwa na Mheshimiwa Rais Yoweri Kaguta Museveni pamoja na Chama cha National Resistance Movement (NRM), ikiwa ni sehemu ya shughuli za uapisho wa Rais wa Uganda.

Kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi, Vyama vya Ukombozi na Vyama-rafiki vilivyoshiriki katika hafla hiyo, Katibu Mkuu Migiro alitoa salamu za pongezi kwa Rais Museveni na Chama cha NRM kufuatia kuaminiwa tena na wananchi wa Uganda kuendelea kuiongoza nchi hiyo.

Katika salaam zake, Ndugu Asha-Rose Migiro alisisitiza umuhimu wa kuendeleza mshik**ano, ushirikiano na urafiki wa kihistoria kati ya vyama vya ukombozi barani Afrika katika kuimarisha maendeleo, amani na ustawi wa wananchi wake.

Want your organization to be the top-listed Government Service in Dodoma?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


Dodoma
0000