Truly In Him

Truly In Him

Share

07/05/2020

USHINDI JUU YA DHAMBI
Sehemu ya 8

Ushindi juu ya dhambi

Bwana Yesu asifiwe, tunaendelea na somo letu, katika sehemu hii tutakuwa tunahitimisha mfululizo huu.

Kila aliyemwamini Yesu Kristo, ametolewa katika ufalme wa giza na kuingizwa katika ufalme wa nuru. Mtu huyo anakuwa ndani ya Yesu, na Yesu anakuwa ndani yake. Mambo yote ya nyuma yanakuwa wamebatilika, anaanza maisha mapya ndani ya Kristo. Biblia inasema katika 2 Wakorintho 5:17 "Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya, ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya"

Yesu alipokuja kutukomboa alitukuta tukiwa hatuwezi kuamua kufanya mema, kwa sababu tulikuwa watumwa wa dhambi. Alitutoa katika utumwa kwa nguvu na uweza wake. Sasa sisi si watumwa tena, bali tumekombolewa, tupo huru, na tena tumeupokea uzima wa milele ndani yetu.

Baada ya kuwa tumekwisha kuwekwa huru, Mungu anatuacha tuendelee kutumia nguvu ya maamuzi aliyotupa. Sasa ni sisi wenyewe kuamua kuendelea kutenda mema au kufanya maovu. Nguvu ya kuamua ipo kwetu, dhambi haina mamlaka juu yetu hata kidogo. Haina nguvu kisheria, kwa sababu tulishanunuliwa kwa damu ya Yesu.

Tunasoma habari za wana wa Israeli, Mungu alipowakomboa kutoka utumwani kule Misri, alitumia nguvu na uweza wake kuwatoa katika utumwa.
Lakini walipokuwa huru, wakapewa uhuru kuchagua, kumfuata Mungu au kuendelea na uovu. Kumbukumbu la torati 30:19 " Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako uzima na mauti, baraka na laana, basi chagua uzima ili uwe hai, wewe na uzao wako" Mungu aliwaambia 'wachague', hakuwalazimisha. Tunasoma pia katika Yoshua 24:14-15 "Basi sasa mcheni BWANA mkamtumikie kwa unyoofu wa moyo na kwa kweli, na kuiweka mbali miungu ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, na huko Misri, mkamtumikie yeye BWANA 15 Nanyi k**a mkiona ni vibaya kumtumikia BWANA, chagueni hivi leo mtakaye mtumikia, kwamba ni miungu ile ambayo baba zenu waliitumikia ng'ambo ya Mto, au kwamba ni miungu ya wale Waamori ambao mnakaa katika nchi yao, lakini mimi na nyumba yangu tutamtumikia BWANA"

Huu ni uhuru ambao mtu anapewa ili achague cha kufanya, Mungu halazimishi.

Tunao uwezo wa kuikataa dhambi, kwa sababu haitumiliki tena, na ni juu yetu kuchukua hatua, biblia inasema katika Warumi 6:12-14 "Basi dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti hata kuzitii tamaa zake, 13 wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu k**a walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha ya haki.14 Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema"

Sisi tunao uwezo wa kuzuia viungo vyetu visitumike kwa dhambi, tunao uwezo wa kutokuzitii tamaa za mwili, kwa sababu dhambi haitawali tena, bali tuko chini ya neema ya Mungu.

Zipo dhambi zinazotuzinga /kutupata kwa upesi. Dhambi k**a hizi pia hazina nguvu ya kututawala, tunatakiwa kuziweka pembeni, tuziache. Uwezo wa kufanya hivyo uko katika maamuzi yetu.
Waebrania 12:1 "Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi, na tupige mbio kwa saburi katika yale mashindani yaliyowekwa mbele yetu."

Pamoja na uhuru tulio nao, ni muhimu kufahamu kwamba shetani yupo na anafanya kazi ya kushawishi na kuhadaa. Mashambulizi yake ameyaelekeza katika fahamu zetu, ili tuamini kuwa dhambi ina nguvu ya kututumikisha, na hata tukijiona kuwa hatuwezi kuikataa. Huo ni uongo wa shetani. Hii ni mbinu kubwa anayoitumia kwa watu waliomwamini Yesu, anawafanya wasitambue kuwa hakuna dhambi ya kuwashinda. Huu ndo ukweli ya kuwa tunao ushindi juu ya dhambi zote, biblia inasema tutaifahamu kweli na hiyo kweli itatuweka huru. Mungu anataka tuujue huu ukweli ili tuwe huru katika fahamu zetu, na kuchukua nafasi zetu.

Sasa, ushindi juu ya dhambi umefanywa na Bwana Yesu, sisi tukiwa ndani yake ndipo tunaweza kuwa na huo ushindi. Nje ya Yesu hakuna ushindi juu ya dhambi.
Tunasoma katika Yohana 15:4-5" Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. K**a vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu 5 Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana, maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote"

Ni muhimu kuzingatia kukaa ndani ya Yesu, ndipo tutaweza kuishi maisha ya ushindi juu ya dhambi.

Mungu akubariki.

06/05/2020

VICTORY OVER SIN
Part 7

Shalom, we continue to look on the remaining two things that Jesus did during redemption of man from sin. These are; Setting men free, and restoring godly life (eternal life)

John 3:16 "For God so loved the world, that he gave his only Son, that whoever believes in him should not perish but have eternal life."

Jesus paid the price through His blood for our reconciliation with God. He defeated sin and death, and has all the authority. If any man believes Jesus, he will be forgiven of his sins and be reconciled with God, he will be set free from sin and will have eternal life (godly life) in him.

The Bible says in Romans 10:9 "because, if you confess with your mouth that Jesus is Lord and believe in your heart that God raised him from the dead, you will be saved."
Everyone who is born again, is freed from sin, and has eternal life in him.
Jesus is calling all people to come to him, to believe him and to be set free from sin and get eternal life.

Will continue to part 8

06/05/2020

USHINDI JUU YA DHAMBI
Sehemu ya 7

Shalom,

Tunaendelea kuangalia mambo mawili ya mwisho ambayo yalifanyika katika ukombozi wa mwanadamu, ambayo ni: Kumuweka huru mwanadamu, na kumrudishia mwanadamu uzima wa kimungu (uzima wa milele)

Yohana 3:16 "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele."

K**a tulivyoona katika sehemu za nyuma, Yesu alikuja kumpatanisha mwanadamu na Mungu, akaishinda dhambi na mauti. Hii yote ni ili mwanadamu aupate uzima wa milele, ambao ni uzima wa kimungu unaokuja kukaa ndani yake.

Yesu alilipa gharama kwa ajili ya dhambi ya mwanadamu. Ili mwanadamu apate msamaha wa dhambi, na kupatanishwa na Mungu, apate kurudishiwa uzima wa kimungu, na kuwa huru mbali na dhambi ni lazima amwamini Yesu Kristo kuwa mkombozi wake.
Huku ndiko kunaitwa kuokoka, maana yake kukombolewa kutoka katika utumwa wa dhambi na katika hatari ya moto wa milele.

Biblia inasema katika Warumi 10:9 "Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka"

Wokovu ni kwa kila mtu anayemuini Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake. K**a mtu hajamuini Yesu, na anataka kutoka katika kifungo cha dhambi, na kuokolewa kutoka katika adhabu ya moto wa milele, nafasi bado ipo, Yesu anawaita watu wote waje kwake.

Itaendelea sehemu ya 8

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Dodoma?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Website

Address


Dodoma