Real Life In Christ Ministries.

Real Life In Christ Ministries.

Share

16/02/2026
04/01/2026

NEXT ELECTION VS NEXT GENERATION

UCHAGUZI UJAO VS KIZAZI KIJACHO
Tunashuhudia tatizo hatari la Kimfumo Katika Bara letu na ulimwenguni kote. Kwa kipindi sasa tumejifunza ushindi wa uchaguzi, lakini tumeacha sanaa ngumu ya kujenga taifa. Matokeo yake ni tunashinda vita vya kisiasa kwenye sanduku la kura, lakini tunapoteza vita ya kujenga kizazi kijacho.

Tumeelimisha kizazi kilicho na elimu zaidi, mitandao zaidi, na ndoto kubwa zaidi. Lakini tumewaachia vyeti bila masoko, sauti bila viti vya maamuzi. Hii ni chembechembe ya misukosuko ya kisiasa.

Kuinuka kwa vijana a.k.a Gen Z ni matokeo ya kujisahau kwa muda mrefu kwa vyama vya siaasa na selikali. Kwa kuweka kipaumbele katika kushinda kila uchaguzi ujao na sio kushida trust na confidence ya kizazi kijacho.
Chaguo ni letu:
KuShinda uchaguzi ujao, lakini kupoteza kizazi.
Au ujenge kizazi, na kulinda mustakabali wa taifa.
Maendeleo ElimuNaAjira

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Address


Dar Es Salaam
Dar Es Salaam
0768027086