Scripture Union Tanzania
20/05/2026
Katika Shule ya ST Merry Secondary school tulipata nafasi ya kufundisha somo la usafi likilenga si tu mazingira na miili yetu, bali pia usafi wa kiroho mbele za Mungu.
Usafi wa mwili hutulinda dhidi ya magonjwa na hutuwezesha kujifunza kwa bidii, lakini usafi wa kiroho hututengeneza kuwa na mioyo safi, tabia njema, na uhusiano mzuri na Mungu na wengine.
Tukumbuke: mwili safi + moyo safi = maisha yenye baraka na mafanikio.
Tujitahidi kuwa mfano wa usafi kila siku katika vitendo, mawazo, na roho zetu.
07/05/2026
Scripture Union Tanzania Kanda ya Kati tulibarikiwa kuwa na Semina ya Watumishi na Wachungaji yenye somo lililosema “Umuhimu wa Maombi”
Kupitia semina hiyo, watumishi wa Mungu walikumbushwa nguvu, nafasi, na umuhimu wa maombi katika huduma na maisha ya kila siku. Tunaamini Mungu ataendelea kuwatia nguvu na kuwajaza hekima katika kulitumikia kanisa lake.
Asanteni wote mliohudhuria na kuungana nasi katika semina.
07/05/2026
Kujenga kizazi kinachoishi katika ukweli!
Timu ya Scripture Union Tanzania Kanda ya Kati ikiongozwa na Mwalimu Dinna Mremi walitembelea Shule ya Msingi Iyumbu kwa ajili ya kufundisha somo la Ukweli
Kupitia mafundisho hayo, wanafunzi walihimizwa kuwa waaminifu, kusema kweli, na kuishi maisha yenye maadili mema katika jamii. Tunamshukuru Mungu kwa nafasi ya kuwafikia watoto na kupanda mbegu njema za tabia.
07/05/2026
SCRIPTURE UNION TANZANIA – KANDA YA KASKAZINI
Watoto ni hazina ya taifa na msingi wa kesho iliyo bora
Karibu katika Kambi ya Watoto kwa watoto wenye umri wa miaka 5–15, mahali pa kujifunza, kukua kiroho, na kujengwa katika maadili mema.
Masomo yatakayofundishwa ni pamoja na:
✓Self-control
✓Forgiveness
✓Purity of Heart
✓Truth
✓Academic Excellence
✓Career Guidance and Counseling
Kupitia michezo, mafundisho, ushauri, na ushirika wa pamoja, watoto watapata nafasi ya kujifunza na kufurahia mazingira salama na yenye kujenga maisha yao ya sasa na ya baadaye.
Usikose kumleta mtoto wako kwenye kambi hii yenye baraka na mafundisho yenye kujenga tabia na kumkaribisha karibu na Mungu.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the place of worship
Telephone
Website
Address
Kalenga Street Upanga Dar Es Salaam Tz
Dar Es Salaam