Watetezitv

Watetezitv

Share

07/07/2026

Na Kenneth Edson, Mbeya

Dereva wa bajaji jijini Mbeya, Samwel Mwakasege, amesema kuwa taarifa za uwepo wa maandamano zimezua hofu miongoni mwa wananchi, hali iliyowafanya wengi kushindwa kutoka kwenda kwenye shughuli zao za kila siku.

Amesema hali hiyo imeathiri sekta ya usafirishaji, kwani idadi ya abiria imepungua kwa kiasi kikubwa na kusababisha madereva wa bajaji kukosa kazi na kipato.

Mwakasege ameitaka serikali kuwasikiliza wananchi kuhusu madai yao ili kupata suluhisho la amani, akisisitiza kuwa amani ndiyo msingi wa maendeleo na ustawi wa jamii.

06/07/2026

Rufaa ya kijana Nasry Lawrence Mkangara, iliyokuwa imepangwa kusikilizwa leo katika Mahak**a Kuu ya Tanzania, imeahirishwa kwa mara ya pili baada ya kubainika kuwa rekodi ya mwenendo wa kesi katika siku ya hukumu haikupandishwa kwenye mfumo wa kielektroniki wa usimamizi wa mashauri wa mahak**a (e-Case Management System).

Rufaa hiyo ilitarajiwa kusikilizwa mbele ya Jaji wa Mahak**a Kuu, Elizabeth Mkwizu, lakini haikuweza kuendelea kutokana na hitilafu hiyo iliyobainika wakati wa maandalizi ya usikilizwaji.

Akizungumza baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo, wakili wa Nasry leo Julai 6, 2026 , Paul Kisabo Paul Kisabo ambaye ni mkuu wa idara ya utetezi Katika Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) THRDC amesema hii ni mara ya pili kwa rufaa hiyo kuahirishwa. Akieleza kuwa mara ya kwanza iliahirishwa Juni 29, 2026 kutokana na hitilafu za kiufundi, huku sababu ya leo ikiwa ni kutokuwepo kwa rekodi ya mwenendo wa kesi ya siku ambayo hukumu ilitolewa katika Mahak**a ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kisabo amesema Mahak**a Kuu imesema haiwezi kuendelea kusikiliza rufaa hiyo bila kuwa na rekodi kamili za mwenendo wa kesi, hususan wa siku ya hukumu, kwani nyaraka hizo ni sehemu muhimu katika uamuzi wa rufaa.

Amefafanua kuwa mfumo wa e-Case Management System hutumika kurekodi mwenendo wa mashauri, kuhifadhi nyaraka za kesi na taarifa mbalimbali pamoja na hoja zinazowasilishwa na mawakili wakati wa usikilizwaji.

Kutokana na changamoto hiyo, Mahak**a imeahirisha usikilizwaji wa rufaa hiyo hadi Julai 8, 2026, saa 8:00 mchana, ambapo shauri linatarajiwa kusikilizwa mbele ya Mheshimiwa Jaji Mkuu katika Mahak**a Kuu ya Tanzania.

Nasry ni miongoni mwa vijana waliok**atwa wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, na baadaye kufikishwa katika Mahak**a ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na makosa mbalimbali, yakiwemo uhaini, wizi, kuvunja duka na kukutwa na mali zinazodaiwa kuwa za wizi.

Kwa mujibu wa taarifa za kesi hiyo, Machi 18, 2026, Nasry alihukumiwa kifungo cha miaka miwili gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kosa la kukutwa na mali zinazodaiwa kuwa za wizi. Baada ya hukumu hiyo, aliwasilisha rufaa katika Mahak**a Kuu kupinga uamuzi huo.

03/07/2026

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche, na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Bara, Amani Golugwa, wameonekana nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Maweni, wakisubiri matokeo ya uchunguzi wa mwili (postmortem) wa aliyekuwa dereva wa Heche, Suez Dani Maradufu.

Maradufu alifariki dunia akiwa katika nyumba ya wageni mkoani Kigoma. Kwa mujibu wa taarifa za awali, alishindwa kupatikana baada ya kutopokea simu wala kuitikia mlango wa chumba alichokuwa amefikia.

Baada ya taarifa kutolewa, askari polisi walifika eneo la tukio na kuvunja mlango wa chumba hicho, ambapo walimkuta Maradufu akiwa amefariki ndani.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma alisema chanzo cha kifo hakiwezi kuthibitishwa hadi uchunguzi wa kitabibu utakapokamilika.

Wakati huo huo, viongozi wa CHADEMA, ndugu wa marehemu pamoja na wanachama na wafuasi wa chama hicho wameendelea kufuatilia kwa karibu mchakato wa uchunguzi, wakisubiri taarifa rasmi zitakazobaini chanzo cha kifo cha Maradufu, aliyekuwa akihudumu kwa muda mrefu k**a dereva wa John Heche.

Want your business to be the top-listed Media Company in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Address


P. O Box 105926
Dar Es Salaam
00225