Initiative for Human Life Development
23/04/2020
Usimamizi wa Vikundi
1. Jipe Moyo Utaweza (JMU) - Segerea
2. Mangumi Youth Group (MY) - Segerea
05/01/2020
Wiki ya Kimataifa ya kunyonyesha mtoto: Zifahamu faida za kunyonyesha
Tamaduni nyingi zisizomruhusu mwanamke kunyonyesha maeneo ya umma pia ni changamoto kwa wanawake wanaonyonyesha
Wakati ulimwengu ukiadhimisha wiki ya kimataifa ya kunyonyesha mtoto na kuelezea faida zake kwa wazazi na taifa, wakazi wa dunia wanahamashishwa kufahamu umuhimu wa maziwa ya mwanzo kabisa ya mama kwa mtoto .
Takriban 40% tu ya watoto wachanga wenye umri kati ya miezi 0 hadi 6 ndio wanaoishi kwa kunyonyeshwa pekee, kulingana na Shirika la Afya duniani.
Kadhalika Shirika hilo linasema kuwa zaidi ya maisha ya watoto 820,000 walio na umri wa chini ya miaka 5 yanaweza kunusurika kila mwaka, ikiwa watoto wenye umri kati ya miezi 0 hadi 23 wangenyonyeshwa kikamilifu.
Ukweli kuhusu umuhimu wa kunyonyesha:
Kunyonyesha ni moja ya njia sahihi ya kuhakikisha mtoto anakuwa mwenye afya na kuendelea kuishi.
K**a viwango vya kunyonyesha vingekuwa vya hali ya juu duniani, takribani maisha 820,000 ya watoto yangenusurika kila mwaka, linasema Shirika la Afya Duniani (WHO).
Unyonyeshaji wa mtoto kwa miezi 6 kuna faida nyingi za kiafya kwa mama na mtoto.
Kumnyonyesha mtoto mara anapozaliwa kwa kipindi cha saa moja, humkinga kwa maambukizi yanayowapata watoto wachanga na kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Maziwa ya mama pia ni chanzo muhimu cha nguvu na virutubisho kwa watoto wa kati ya miezi 6 hadi 23.
Maziwa ya mama yanaweza kuchangia nusu au zaidi ya nguvu za mtoto katika umri wa miaka 6 hadi 12
Watoto na vijana wadogo walionyonyeshwa wakiwa wachanga wana uwezekano mdogo wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia .
Unyonyeshaji wa mtoto humsaidia kuboresha uwezo wa utambuzi wa akili (IQ), mahudhurio ya shule , na pia huhusishwa na mapato ya juu katika maisha yake ya utu uzima.
Kunyonyeshwa kwa muda mrefu pia huchangia afya na maisha bora ya mama kwani humpunguzia hatari ya kupata saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi na matiti.
Kunyonyesha hutengeneza vichocheo vya mwili ( hormone) ambazo humtuliza mama na mtoto
Juma hili linaadhimishwa huku baadhi ya wanawake duniani wakishindwa kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo kutokana na sababu mbali mbali.
Takribani 40% tu ya watoto wachanga wenye umri kati ya miezi 0 hadi 6 ndio wanaoishi kwa kunyonyeshwa pekee, kulingana na Shirika la Afya Duniani
Licha ya juhudi mbali mbali ambazo zimekuwa zikifanyika kuelemisha wakina mama na jamii nzima juu ya umuhimu wa kunyonyesha na maziwa ya mama kwa mtoto, baadhi ya mila na tamaduni hususani za Kiafrika zimekuwa na changangoto kubwa ya kuelewa na kukubali umuhimu wa kunyonyesha kutokana na kukosa elimu ya kunyonyesha.
Miongoni mwa changamoto zinachangia wanawake kushindwa kuwanyonyesha watoto wao ni pamoja na kazi, magonjwa pamoja na tamaduni nyingi zisizomruhusu mwanamke kunyonyesha maeneo ya umma.
Aidha baadhi yao wamekuwa na imani potofu kuhusu suala zima la kunyonyesha na faida zake. Hili limechangia pakubwa katika kudhoofisha jitihada za kuhakikisha kila mama mwenye mtoto mchanga anamyonyesha ipasavyo.
Baadhi ya imani potofu kuhusu kunyonyesha:
Maziwa ya kwanza ya mama si mazuri kwa mtoto yanapaswa kumwagwa
Kunyonyesha humfanya mama anenepe kupindukia
maziwa ya mama pekee hayawezi kumridhisha mtoto wa umri wa miezi 0 hadi 6.
Baadhi ya vyakula si vizuri kwa wanawake wanaonyonyesha
Ni lazima mtoto mchanga anywe maji mara baada ya kuzaliwa
Maziwa ya mama humfanya mtoto ajihisi mwenye kiu
Baadhi ya wanawake hudai wanaponyonyesha matiti yao husinyaa na kuanguka.
Shirika la watoto la Save the Children linasema kuwa watoto wenye utapiamlo unaochangiwa na kutonyonyeshwa ipasavyo unakadiriwa kusabisha vifo vya watoto 2.7 kila mwaka.
Wataalam wanasema mguso wa mwili baina ya mama na mtoto wakati wa kunyonyesha husaidia kuchochea uzalishaji wa maziwa ya mama
Wiki ya kimataifa ya kunyonyesha inaadhimishwa huku Serikali na wakazi wa dunia kwa ujumla wakitolewa wito kuwasaidia wanawake kuwanyonyesha watoto katika kipindi cha saa moja ya kwanza ya uhai wake.
Wataalam wanasema mguso wa mwili kwa mwili pamoja na kunyonya husaidia kuchochea uzalishaji wa maziwa ya mama , yakiwemo maziwa ya mwanzo kabisa ya mama baada ya kujifungua ambayo hutambuliwa k**a''chanjo ya kwanza'', yenye virutubisho vingi pamoja na kinga ya ya mwili.
FURSA
TAASISI YA TEC INAWATANGAZIA VIJANA MANISPAA YA ILALA KUANZIA MIAKA 18-24 KUWA, KUNA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI YANAYOTOLEWA CHINI YA MRADI WA VIA JIANDALIE AJIRA KWA VIJANA, YANATARAJIWA KUANZA TAREHE 18/09/2018. FOMU ZA MAOMBI ZINAPATIKANA OFISI ZA IHLD - SEGEREA. MWISHO WA KURUDISHA FOMU NI TAREHE 24/08/2018.
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA KWA NAMBA+255 758 258 722
& +255 689 429 132
UKIPATA UJUMBE HUU MTAARIFU NA KIJANA MWENZIO
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam
255