Harakati Media
04/06/2026
FILAMU YA UCHUNGUZI YAIBUA MJADALA WA AMANI NA MAENDELEO AFRIKA
Filamu ya uchunguzi ya mwanahabari David Hundeyin imechochea mjadala kuhusu nafasi ya vijana, wajibu wa vyombo vya habari na umuhimu wa kulinda amani katika jamii za Afrika.
Akizungumza baada ya kuonyeshwa kwa filamu hiyo, mwanasiasa mkongwe Hamad Rashid amesema Waafrika wanapaswa kujenga uwezo wa kufanya tafiti na uchunguzi wa kina kuhusu masuala yanayowahusu huku wakitumia mafunzo yaliyopatikana kuimarisha umoja, amani na maendeleo.
Naye mchambuzi wa maendeleo kutoka Zimbabwe, Joshua Maponga, amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari vya ndani kuripoti kwa kina masuala ya jamii na kuwataka vijana kuelekeza nguvu zao katika ubunifu, uzalishaji na ujenzi wa uchumi.
Kwa upande wake, David Hundeyin amesema filamu hiyo inalenga kuhamasisha uelewa kuhusu namna ushawishi wa nje unavyoweza kuathiri jamii za Afrika kupitia njia mbalimbali.
DavidHundeyin Habari Tanzania
06/05/2026
Jemsi Mbowe atoa wito kwa Vijana, tumieni Mitandao kwa Hekima
Mwanasiasa na aliyekuwa mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Hai, James Mbowe, ametoa rai kwa vijana nchini kuacha kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa sheria kupitia mitandao ya kijamii.
Amesisitiza kuwa majukwaa ya kidijitali yanapaswa kutumika kwa staha, heshima na uwajibikaji, badala ya kuwa sehemu ya matusi, vitisho na lugha chafu dhidi ya viongozi na wananchi.
“Vijana wajikite katika shughuli za kuwaongezea kipato badala ya kushinda mitandaoni wakishambulia watu,” amesema Mbowe.
Aidha, amegusia hatua za Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuwashikilia vijana 37 kwa tuhuma za makosa ya kimtandao, akisisitiza kuwa sheria zinafuatwa na hatua zinaendelea kuchukuliwa kwa wanaokiuka matumizi sahihi ya mitandao.
Ujumbe ni wazi: Mitandao ya kijamii si uwanja wa kuvunja sheria, bali ni fursa ya kujenga maisha, kukuza uchumi na kuleta maendeleo kwa jamii.
Tanzania
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Dar Es Salaam