RaiaPost

RaiaPost

Share

24/11/2025

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekeza kwam a hakutakuwa na maadhimisho ya sherehe za Uhuru December 09,2025 na badala yake fedha ambazo zilipaswa kutumika katika sherehe hizo zitumike katika kurekebisha miundombinu iliyoharibika kutokana vurugu zilizotokea October 29, 2025.

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amesema hayo wakati akiongea na Wakazi wa Mbezi Luis Jijini Dar es salaam leo November 24,2025.

“Ninaungana na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa pole kwa wote walioathirika na vurugu zilizotokea oktoba 29, 2025, tumuunge mkono Rais na Wajumbe wa Tume iliyoundwa kwa ajili kuchunguza kwenye undani tukio la vurugu zilizotokea Oktoba 29, 2025 ili tujue namna lilivyofanyika na hatua stahiki zitakazochukuliwa

“Nimepitia na kukagua uharibifu wa mali na miundombinu ya umma, huwezi kuamini k**a tukio hili limetokea Tanzania, Watanzania tunapaswa kujua miundombinu hii ni mali ya umma, tunazijenga kwa fedha zetu sisi Watanzania, si pesa za Serikali”

“Wanaoshabikia uharibifu wa miundombinu ya Umma hawapo hapa nchini, wanawaambia mkachome mali za umma, mkifanya hivi mtaishije? huko wanakoishi haya wanayowaambia mfanye huko kwao hauwezi kuyafanya.

“Wanajipa haki kwamba wao wanaipenda Tanzania, mpenda Tanzania hawezi kukwambia uichome Tanzania, msiwasikilize, mkiichoma zaidi Tanzania wao ndio wanalipwa zaidi”

Credit

08/10/2025

07/10/2025

: Jeshi la Polisi limeanza rasmi uchunguzi wa tuhuma za kutekwa kwa Humphrey Polepole kufuatia madai yaliyotolewa na Augustino Polepole kupitia mitandao ya kijamii, ambapo alidai kuwa ndugu yake alitekwa na Afisa wa Polisi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa Oktoba 6, 2025, jalada la uchunguzi lilifunguliwa mara moja siku hiyo hiyo, na hatua za awali zimejumuisha ukusanyaji wa taarifa mbalimbali zinazohusiana na tukio hilo.

Polisi wamesema wanaendelea kumtafuta Augustino Polepole ili aweze kutoa ushirikiano na kufafanua kwa kina madai yake, ikiwa ni pamoja na kutoa uthibitisho kuwa Humphrey alikuwa mkazi au mpangaji wa nyumba aliyodai kuwa tukio hilo lilifanyika.

Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuwa watulivu wakati uchunguzi huu ukiendelea na limeahidi kutoa taarifa zaidi kadri hatua za kisheria zitakavyopigwa.

Credit
ITV

Want your business to be the top-listed Media Company in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Dar Es Salaam