Dr Ramo
Wanaume wengi huingiwa na hofu wanapoambiwa wana changamoto ya mbegu za uzazi. Lakini katika hali nyingi, changamoto za uzazi kwa mwanaume huwa na mwelekeo wa matibabu unaoeleweka zaidi pale chanzo kinapojulikana.
Ikiwa tatizo lipo kwenye idadi ya mbegu, ubora wake au uwezo wake wa kusafiri, matibabu mara nyingi hulenga eneo hilo moja kwa moja. Hali huwa tofauti kwa mwanamke, ambapo mara nyingi huhitajika kushughulikia mambo kadhaa kwa pamoja k**a homoni, ovulation, afya ya mirija ya uzazi, maambukizi na sababu nyingine zinazoweza kuathiri uwezo wa kupata ujauzito.
Ndiyo maana mwanaume hapaswi kuona changamoto ya uzazi k**a mwisho wa matumaini. Mara nyingi kinachohitajika ni kuanza kushughulikia tatizo lililobainika kwa wakati sahihi badala ya kuendelea kuishi na wasiwasi au kusubiri hali ibadilike yenyewe.
Kila siku tunakutana na wanaume ambao walidhani nafasi yao ya kuwa baba imepotea, lakini baada ya kupata matibabu yanayofaa wakaendelea na safari yao ya uzazi kwa mafanikio.
This content is for educational purposes only. Diagnosis and treatment outcomes vary depending on an individual’s medical condition and assessment.
27/05/2026
Katika safari yoyote ya uzazi kwa mwanamke, kinachoumiza zaidi ni Mwenza wake kutokuwa upande wake kihisia, kiakili, na hasa inapotokea amechelewa kupata matokeo.
Je, kwako hii hali imewahi kukutokea?
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the public figure
Telephone
Website
Address
Ilala
Dar Es Salaam
Opening Hours
| Monday | 09:00 - 18:30 |
| Tuesday | 09:00 - 18:30 |
| Wednesday | 09:00 - 18:30 |
| Thursday | 09:00 - 18:30 |
| Friday | 02:30 - 18:30 |
| Saturday | 09:00 - 18:30 |
| Sunday | 09:00 - 18:30 |