Machinga Tv
Mjadala mkali kuhusu Kombe la Dunia uligeuka burudani baada ya gwiji wa soka Zlatan Ibrahimoviฤ na staa wa mitandao IShowSpeed kukutana kwenye kipindi cha FOX Sports.
IShowSpeed alisisitiza kwa kujiamini kuwa Portugal itatwaa Kombe la Dunia kwa msaada wa Cristiano Ronaldo, lakini Zlatan hakukubaliana naye hata kidogo. Kwa utani wake wa kawaida, Zlatan alimkatisha Speed na kuzua vicheko vikubwa kwa watazamaji.
Video ya tukio hilo imeenea kwa kasi mitandaoni, ikikusanya mamilioni ya watazamaji huku mashabiki wakibishana k**a Portugal kweli ina nafasi ya kutwaa ubingwa au Zlatan alikuwa sahihi kuipinga kauli hiyo.
๐โฝ Nani unaamini? Portugal kubeba Kombe la Dunia au Zlatan alikuwa anatania tu?
Imamu Mkuu Masjid Mtambani Sheikh Shabani Pembe amewataka Waislamu na Watanzania wote kwa ujumla kuendelea kudumisha na kuilinda amani ya Tanzania, akisisitiza kuwa ikiwa serikali ingeruhusu kufanyika kwa kile kilichokuwa kimepangwa, kuratibiwa na kuhamasisha Oktoba 29, 2025 basi Tanzania isingeweza kukalika tena kutokana na uvunjifu wa amani ambao ungetokea wakati ule wa Uchaguzi.
Sheikh Shabani Pembe amebainisha hayo wakati akitoa hotuba yake kwa waumini wa Dini ya Kiislamu Mkoani Dar Es Salaam na kuwataka Waislamu kuhukumu kile kilichotokea kwa uadilifu pamoja na kupima athari ambazo zingeweza kujitokeza ikiwa serikali ingewaaacha wale waliokuwa wamejitokeza barabarani kuendelea na matukio yao ya uvunjifu wa amani Nchini.
"Kituo chetu cha mwendokasi tumeshuhudia kikichomwa, Vituo vya Polisi vilichomwa, ATM pale Manyanya imechomwa na hata maduka ya watu yamechomwa na kuibiwa, hawa watu wangeachiwa wafanye wanavyotaka hii Nchi ingekuwa wapi? Ndugu zangu tunapohukumu tuhukumu kwa uadilifu, kwamba lengo lilikuwa waachiwe wafanya wanavyotaka? Au ilikuwa nini? Baadae wale wote waliowachochea wanaanza kuiona dola mbaya, Tunapohukumu mambo tuhukumu kwa uadilifu." Amesema Sheikh Pembe.
"Tunapohukumu mambo tuhukumu kwa uadilifu, amani ni tunu ndugu zangu, ikiondoka hii hata sisi hatuwezi kukusanyika. Ile Ijumaa ile kutoka Tegeta mpaka hapa nililipa Elfu sitini kwa bodaboda na nimefika hapa naambiwa M***i ametangaza hakuna ibada hapa, sasa waislamu niwaombe kuipenda Nchi yako ni katika Imani. Wale wote waliokuwa wanahamasisha yale ya Oktoba 29 hakuna hata mtoto wao aliyeguswa na kiwembe, tafsiri yake ni kuwa wao na familia zao zilibaki salama, kinyume chake familia za maskini na fukara ndio waliotolewa kafara." Ameongeza kusema.
Sheikh Pembe amewakosoa vikali pia wale wanaokosoa Tume zilizoundwa kuchukua matukio hayo ya wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, akisisisitiza kuwa Tanzania ni huru na Watanzania wanapaswa kuunga mkono busara na hekima za Viongozi wao katika kupata muafaka na suluhu ya kudumu dhidi ya kile kinachotajwa k**a sababu ya matukio ya Oktoba 29, 2025.
Simanzi na majonzi makubwa vimetanda katika Chuo Kikuu cha St. John kilichopo Jijini Dodoma wakati wa ibada ya kuaga mwili wa mwanafunzi huyo, tukio lililohudhuriwa na wanafunzi, walimu, familia na ndugu wa karibu.
Kwa mujibu wa taarifa, Rebeca Misungwi alipata ajali ya moto usiku wa kuamkia Jumapili ya Juni 6, 2026 katika eneo walilokuwa akiishi pamoja na rafiki yake Felister Peter Francis. Ajali hiyo ilisababisha majeraha makubwa yaliyomfanya kulazwa hospitalini kwa matibabu ya dharura.
Baada ya kupatiwa matibabu kwa muda, Rebeca alifariki dunia Juni 11, 2026 akiwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, ambapo pia rafiki yake Felister alikuwa akipatiwa matibabu.
Mwili wa marehemu umefanyiwa ibada ya kuaga chuoni hapo St. John University Dodoma, kabla ya kusafirishwa kuelekea Mkoa wa Mwanza kwa ajili ya mazishi.
Akizungumza kwa niaba ya familia, kaka wa marehemu, Pascal Kapote, amesema familia imepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo hicho na kuomba Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi wa kina ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo na hatua za kisheria zichukuliwe kwa wote watakaobainika kuhusika.
Familia imethibitisha kuwa ratiba kamili ya mazishi itatolewa mara baada ya mwili kuwasili mkoani Mwanza.
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Website
Address
Dar Es Salaam