AFYA ROOM

AFYA ROOM

Share

07/03/2026

πŸ”₯ WIKI YA 35 YA UJAUZITO – SASA NI KARIBU SANA! πŸ€°πŸ½πŸ‘ΆπŸ½
Mamaaa… tukubaliane kitu πŸ˜„
Kuanzia wiki ya 35, kila mtu anaanza kukuuliza:
β€œBado hujajifungua?”
Lakini ukweli ni kwamba safari bado inaendelea kidogo 🀍
πŸ‘ΆπŸ½ Mtoto wako wiki ya 35:
βš–οΈ Uzito: takribani 2.4 – 2.6 kg
πŸ“ Urefu: karibu 45 – 46 cm
🍈 Ukubwa: sawa na tikitimaji dogo
Ndani ya tumbo:
🫁 Mapafu yako karibu kabisa kukomaa
🧠 Ubongo unaendelea kukua kwa kasi
🦴 Mifupa inaendelea kuimarika
πŸ‘‡πŸ½ Wengi wao tayari wanakuwa kichwa chini wakijiandaa kuzaliwa

🀰🏽 Kwa mama wa wiki ya 35:
β€’ Tumbo linaweza kushuka kidogo
β€’ Maumivu ya mgongo yanaweza kuongezeka
β€’ Haja ndogo mara kwa mara 🚽
β€’ Usingizi kuwa changamoto πŸ˜…
β€’ Braxton Hicks (uchungu wa mazoezi) unaweza kuongezeka

πŸ’‘ Ushauri wa wiki hii:
βœ”οΈ Andaa begi la hospitali πŸ‘œ
βœ”οΈ Hakikisha una namba ya hospitali karibu
βœ”οΈ Endelea kufuatilia movement za mtoto
βœ”οΈ Usikose kliniki

πŸ˜„ SWALI LA SIKU (tuseme ukweli kidogo):
Ni swali gani linakukera zaidi watu wanapokuuliza ukiwa na tumbo kubwa?
1️⃣ β€œBado hujajifungua?”
2️⃣ β€œNi mapacha?”
3️⃣ β€œUtajifungua lini?”
4️⃣ β€œMbona tumbo kubwa sana?”
Andika namba yake kwenye comment tuone ni lipi linaongoza πŸ€£πŸ‘‡πŸ½
πŸ‘ Like
πŸ’¬ Comment
πŸ” Share kwa mama mwingine

Want your practice to be the top-listed Clinic in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Address


Dar Es Salaam
255