Milingoti mitatu
07/02/2022
FRANCIS BARAZA - Kocha Bora wa Ligi Kuu ya NBC mwezi Januari, 2022.
07/02/2022
#
///
Nimeona mjadala wa VAR 👏👏 ni wazo zuri naamini nia ni kuufanya mpira wa nchi hii uendelee kuwa bora zaidi.
Lakin kwangu VAR sio tatizo la msingi la mpira wetu.
Tatizo la msingi la mpira wetu ni sehemu ya kuchezea (PITCH).
Tuna pitch mbovu sana nchi hii ukitoa Taifa, Azam Complex na Kaitaba, viwanja vingi vilivyosalia ni changamoto.
Mpaka leo viwanja vyetu vinapakwa chokaa kabla ya mechi na baada ya muda chokaa inafutika uwanja unakua hauna mistari.
Mvua zikinyesha kidogo tuu mpira hauchezeki
Mechi nyingi zinachezwa kwa kulazimishwa mfano mechi ya Mbeya City Vs Ruvu Shooting haikupaswa kuchezwa pale Sokoine.
Ushauri wangu kabla ya ku invest kwenye VAR tungejikita kuboresha viwanja..
Europe walianza kuboresha viwanja ndo wakaja kwenye VAR.
Na kabla ya kufika kwenye VAR mamlaka husika waendelee kuboresha viwango vya waamuzi wetu wapate seminar za kutosha na wapate mechi kubwa za Afrika ili kuongeza uzoefu na kujiamini kwao.
Tukishamaliza kuwekeza kwenye Pitch ndio tutakuja kwenye VAR.
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Website
Address
Dar Es Salaam