BAKIIF Islamic

BAKIIF Islamic

Share

13/10/2022

Swalah ya Ijumaa ni wajibu kwa kila Muislamu aliyebaleghe

Enyi mlioamini! Kukinadiwa Swala kwa siku ya Ijumaa, endeni kwa haraka kwenye utajo wa Mwenyezi Mungu, na muache kufanya biashara.

Hawatoacha watu kuhudhuria Ijumaa, au Mwenyezi Mungu Atapiga mihuri juu ya nyoyo zao, kisha wawe ni miongoni mwa walioghafilika.

BAKIIF-ISLAMIC
+255755351262

19/07/2022

KWENYE DINI YA KIISLAMU HAKUNA KITU KINAITWA "KUOKOKA"

Sababu kubwa ni kwamba uislamu haukatazi kufanya madhambi bali uislamu unakataza kufikiria kufanya dhambi.

Yaani uislamu unashinikiza fikra zako zisijikite wala kupata nafasi kufikiria kunako kufanya dhambi. Mfumo mzima wa maisha ya mwislamu kwake ni ibada. Kila jambo alifanyalo muislamu kwa nia nzuri kwake ni ibada.

Fikra ni sawa sawa na Nia. Hivyo uwislamu unaipigania fikra yako nasio matendo yako, kwasababu fikra ndio Nia na ndio mzizi mkuu wa wewe kufanya madhambi na mema.

Hakuna tendo lolote litafanywa bila kulifikiria kwanza (kuliwekea nia) liwe baya au zuri ni lazima ufikirie kwanza yaani uwe na nia nalo. Sasa Uislamu unaipigania nia yako yaani ile fikra yako nasio matendo yako.
Tendo linaweza kuwa baya lakini nia yake ilikuwa ni zuri. Kwa mfano: Askari wa nchi kujiunga na kundi la ujambazi ili kuwafahamu hao majambazi na kubaini mipango yao na njia zao kwa kuwa nao pamoja ili baadae kuweza kuwadhibiti: Hapo utakuta tendo hilo kimtazamo ni baya kabisa na halifai lakini nia yake ni nzuri kwasababu inakuja kuilinda jamii hapo baadae isiweze kudhurika.

Pia tendo linaweza kuwa zuri lakini nia yake ilikuwa ni mbaya: Mfano; ibada za ria (kufanya ibada ili watu wakuone) hii ibada haitapokelewa na MUNGU kwasababu nia yako wewe ni watu wakuone, wakusifie na kukutukuza lakini kiuhalisia hukufanya kwa ajili ya MUNGU. Kwa hiyo unakuta hapo tendo ni zuri kimtazamo lakini nia ya muhusika ni mbovu na wala haifai.

HIVYO BASI, KWENYE UISLAMU HAKUNA "KUOKOKA" Kwasababu uislamu haupambani na matendo yako bali uislamu unapambana na nia yako. Kwani hata huko kuokoka bado kunaweza kukawa na nia mbaya. Pia ili uwokoke lazima ufikirie kunako kuokoka yaani lazima kuwe na nia hiyo. Sasa nia ni jambo kuu ambalo uislamu hulitazama, yaani ile fikra yako kunako kufanya jambo fulani.

Kwanini uislamu unakataza fikra mbovu.? Hii ni kwasababu kadiri fikra mbovu unapoipa nafasi kichwani kwako ndivyo inaelekea kutekelezeka kimatendo. Hivyo uislamu unakataza kabisa kufikiria kunako kufanya dhambi.

YESU Alisema kuwaambia watu wake "Hakika Musa aliwakataza msizini, lakini mimi ninawakataza msifikirie kunako zinaa"

Want your place of worship to be the top-listed Place Of Worship in Dar es Salaam?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Telephone

Address


P. O. BOX 55185 Kam College Road, Kivulini Street, House No: 36, Ubungo District, Dar Es Salaam
Dar Es Salaam