Christ Embassy Tanzania - Virtual Church
30/05/2026
RHAPSODI YA UHAKIKA
Jumamosi, May 30, 2026
Mchungaji Chris

MAFANIKIO, USHINDI NA ONGEZEKO
Naye atakuwa k**a mti uliopandwa imara [na kutunzwa] kando ya vijito vya maji, tayari kutoa matunda yake kwa majira yake; jani lake halitanyauka wala kukauka; na kila afanyalo litafanikiwa [na kukomaa] (Zaburi 1:3 AMPC).
Mungu hazai mapooza. Mtu anapoungana na Kristo, anaingia katika maisha yaliyopangiliwa kwa ajili ya mafanikio, ushindi na ongezeko pekee. Asili ya Mungu ndani yako huzaa ubora, maendeleo, na ukuu. Ni uhalisia wa maisha ya kiumbe mpya.
Nilipata ufahamu huu mapema sana. Nilizaliwa mara ya pili kabla sijafikisha umri wa miaka tisa na nikaanza kuhubiri Injili muda mfupi baadaye. Nilianza kuwaleta marafiki zangu kwa Kristo, na muda mfupi baada ya kufikia umri wa miaka kumi, nilianzisha ushirika wa waliomjua Kristo. Nikiwa na umri wa miaka kumi na tano, nilikuwa tayari nikifanya mikutano ya injili. Nimetembea katika njia hii kwa muda wa kutosha kiasi cha kujua zaidi kupita hoja yoyote ile kuwa Neno linafanya kazi.
Mungu anapokuweka kwenye njia sahihi na akili yako ikakaa kwake, Neno linatangaza kwamba atakuweka katika amani kamilifu kwa sababu unamwamini. Amani hiyo ni amani ya ustawi, maisha yanayokufanya usonge mbele daima. Maandiko pia yanasema kuhusu mtu aliye ndani ya Kristo: Lolote afanyalo litafanikiwa.
Hiyo ndiyo hatima ya yule anayeishi kwa Neno; tuliona hilo katika andiko letu la ufunguzi. Yule ambaye hafuati ushauri wa wasiomcha Mungu amebarikiwa. Baadhi ya watu huruhusu marafiki, jamaa, au majirani wasiomcha Mungu kuunda maamuzi yao; hapana!
Mtu aliyebarikiwa hufurahia Neno la Mungu na kulitafakari mchana na usiku. Analizingatia Neno, na Neno huumba maisha yake. Matokeo yake huwa ya ajabu: Anakuwa k**a mti uliopandwa kando ya mito ya maji, huzaa matunda kwa majira yake, na jani lake halinyauki; hiyo ina maana kwamba hakuna kushindwa kwako. Ni Maisha ya kipekee namna gani!
Unapojiweka kikamilifu katika Neno, linakupangilia kukaa katika safari ya njia moja maishani, ambayo ni safari ya—kupanda juu tu na kusonga mbele pekee. Neno ni mbegu, na kulitafakari hufanya liweke mizizi yake ndani ya roho yako na kutawala mawazo yako kiasi kwamba utakuwa unafikiria mafanikio, ushindi, na utukufu pekee. Maisha yako yanakuwa udhihirisho wa Neno, na kukufanya uwe na mafanikio mema (Yoshua 1:8). Haleluya.
SALA
Mpendwa Baba, nakushukuru kwa maisha ya mafanikio yasiyo na mwisho ambayo umenipa katika Kristo. Neno Lako hufanya kazi kwa nguvu ndani yangu, likizalisha ubora, ustawi, na ushindi; Nina rundo la mafanikio juu ya mafanikio. Ninalifikiria Neno, ninalinena Neno, na kutembea katika nuru ya Neno kila siku, katika Jina la Yesu. Amina.
MASOMO ZAIDI:
Yoshua 1:8 AMPC; 3 Yohana 1:2; Mithali 4:20-22
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MWAKA 1:
Yohana 15:1-17; 1 Mambo ya Nyakati 3-4
MPANGO WA KUSOMA BIBLIA KWA MIAKA 2:
1 Wakorintho 14:20-30; Mithali 26
Sala Ya Wokovu
“Ee Bwana Mungu, ninamwamini kwa moyo wangu wote Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai. Ninaamini kuwa alikufa kwa ajili yangu na kuwa Mungu alimfufua kutoka kwa wafu. Ninaamini kuwa yu hai leo hii. Ninakiri kwa kinywa changu kuwa Yesu Kristo ni Bwana wa maisha yangu kuanzia leo. Kupitia Yeye na katika Jina Lake, nina uzima wa milele; nimezaliwa upya. Ahsante Bwana, kwa kuiokoa nafsi yangu! Sasa, mimi ni mwana wa Mungu. Haleluya!”
Imetolewa kutoka: Rhapsody of Realities Daily Devotional
Weka maoni kuhusu Rhapsodi ya leo kwenye https://www.rhapsodyofrealities.org
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Address
Christ Embassy Tanzania, Loveworld Arena Near Songas Ground , Salasala
Dar Es Salaam